Kamati Kuu CCM kukutana kujadili Rasimu ya Katiba

M

mecy

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2012
Messages
422
Likes
0
Points
0
M

mecy

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2012
422 0 0
Rasimu ya katiba mpya inaonekana kuitesa sana Ccm kwa kuhofia ndo mwiba kwao,wameahidi kutoipitisha kwa 100%.nadhan kwa katiba hi endapo vurugu itatokea basi ni ccm watakuwa ndo waanzilishi hakika,wananch tusikubali ccm kutuandalia katiba ya nch yetu,Kamati kuu ya ccm kukaa jumatatu kujadili,mtajiju,
Chama cha Mapinduzi kimeitisha kikao cha dharura cha Kamati kuu kujadili rasimu ya katiba.

  • Kufanyika Jumatatu ijayo
  • Kinana: Hatuungi mkono rasimu kwa asilimia 100

=======

*Yaitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu
*Mapendekezo ya Serikali tatu yazua jambo

HATUA ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutangaza rasimu ya Katiba mpya siku chache zilizopita, imeibua fukuto jipya la kisiasa lenye mwelekeo wa kuipinga.

Tayari baadhi ya wanasiasa kutoka vyama mbalimbali hususan wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamekwishakaririwa wakieleza kutokubaliana nayo kwa madai kuwa haiendani na mfumo wa siasa za kileo na kwamba imelenga kuongeza mzigo wa uendeshaji wa Serikali.

Mbali na wanasiasa mmoja mmoja, waliokwishatoa maoni yao yenye mwelekeo wa kutokubaliana na baadhi ya vipengele katika rasimu hiyo, CCM kimetangaza kuitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu (CC) kwa ajili ya kuijadili.

Tangazo la kuitishwa kwa CC ya CCM, lilitolewa mjini Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wake, Abdulrahaman Kinana, mbele ya waandishi wa habari ambaye alieleza kuwa itakutana Jumatatu ya wiki ijayo, kwa ajenda moja tu ya kupitia kwa undani rasimu ya Katiba mpya.

Taarifa kutoka vyanzo vya ndani ya chama hicho, zimeeleza kuwa mjadala unatarajiwa kuwa mkali wakati wa kujadili suala la Serikali tatu, ambalo tangu kutangazwa kwa rasimu hiyo ikipendekeza hivyo, baadhi ya vigogo waliokwishatangaza au kuonyesha nia ya kuwania urais wamekuwa katika sintofahamu ya nini cha kufanya.

Ni sintofahamu hiyo, inayoonekana kukikumba pia CCM ambacho kupitia kwa Kinana kimeeleza kuwa CC itakayoketi Jumatatu, itaangalia kwa undani iwapo rasimu ya Katiba mpya, itakidhi matakwa halisi ya wakati huu.

"Siwezi kuzungumzia msimamo wa chama kuhusu rasimu hiyo kwa sasa hadi Kamati Kuu ya chama, itakapokuwa imekaa Jumatatu ijayo.

"Si busara kuharakisha kuzungumzia suala hilo kabla chama hakijakaa na kuichambua kipengele kwa kipengele, kuona kama inakidhi hali halisi ya matakwa ya kisiasa tuliyo nayo sasa," alisema Kinana.-Wakati Kinana akieleza hayo, duru za kisiasa kutoka ndani ya CCM, zinaeleza kuwa Rasimu ya Katiba mpya imeibua hali na wasiwasi kwa vigogo wa chama hicho wanaohofia chama chao kupoteza nguvu za mamlaka ya dola kutokana na upepo wa kisiasa unavyovuma sasa nchini.

Wadadisi na wafuatiliaji wa mambo walio ndani ya CCM, wanaeleza iwapo muundo wa Serikali tatu za Zanzibar, ya Tanzania Bara na ile ya Jamhuri ya Muungano kama zilizopendekezwa na Tume ya mabadiliko ya Katiba utaridhiwa, CCM kinaweza kuambulia ukuu wa Serikali ya Muungano pekee.

Imani hii ya wadadisi na wafuatiliaji wa mambo, inajengwa katika msingi wa uungwaji mkono na wananchi kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa upande wa Tanzania Bara na Chama cha Wananchi (CUF) kwa upande wa Zanzibar.

Kwa msingi huo, haina shaka kuwa CUF ambacho kina nguvu kubwa ya kisiasa kwa upande wa Zanzibar, kinaweza kuibuka kidedea katika kinyang'anyiro cha urais, huku Chadema kinachoendelea kujipatia umaarufu na uungwaji mkono mkubwa wa wananchi kikichukua udhibiti wa Serikali ya Tanzania Bara na kukiacha CCM kikibaki na udhibiti wa Serikali ya Muungano ambayo kinaweza kushinda kutokana na historia yake ya kusaka ushindi wa jumla.-

Wakati wadadisi na wafuatiliaji wa mambo wakitoa tathimini hiyo kwa upande wa vyama, wachambuzi wa siasa za ndani ya CCM wameeleza kuwa, iwapo chama hicho kitapoteza nguvu ya udhibiti za Serikali za Tanzania Bara na ile ya Zanzibar na kubaki na Serikali ya Muungano pekee, hilo linaweza kuwa anguko lake la kiuchumi.

Inaelezwa CCM kikiwa na udhibiti wa Serikali ya Muungano, hakitakuwa na ardhi ambayo kimekuwa kikiitegemea zaidi kwa ajili ya kujiendesha kiuchumi jambo ambalo litakifanya kitegemee zaidi misaada ya wahisani.

Baadhi ya wataalamu wa uchumi, waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la majina yao kuhifadhiwa kuhusiana na mwenendo huo wa mambo, walieleza kuwa CCM kikiwa na udhibiti wa Serikali ya Muungano, hakitaweza kujiendesha na pia kitashindwa kuwahudumia wananchi kwa sababu kitakuwa tegemezi kwa wafadhili kama vilivyo vyama vya upinzani hivi sasa.Vyama vitavyonufaika na mfumo mpya wa uundwaji wa Serikali kama ilivyopendekezwa kwenye rasimu, ni kile ambacho kitakuwa na udhibiti wa dola ya Zanzibar, ambacho kitadhibiti ardhi, rasilimali na uchumi wa jumla na kile ambacho kitashika dola Tanzania Bara ambacho pia kitakuwa na ardhi na kumiliki rasilimali za nchi.

Mambo haya ndiyo yanayoonekana kuwaumiza vichwa wanasiasa na vyama ambavyo vimekuwa vikipambana kuwania ukuu wa dola, ambapo tangu Juni 3, siku ambayo Jaji Joseph Warioba, alitangaza rasimu ya Katiba mpya iliyokuwa ikipendekeza kuwepo kwa muundo wa Serikali tatu, fukuto la kisiasa kwa wanasiasa walioonyesha tamaa ya urais na vyama vinavyoiwinda Ikulu, limepanda.Ndani ya CCM, kuna vigogo kadhaa ambao wameonyesha nia ya kugombea urais mwaka 2015, ambao Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano), Stephen Wassira, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.

Kwa upande wa Chadema, watu ambao wanatajwa kuonyesha nia ya kugombea urais ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Lakini Chama cha Wananchi (CUF) nacho hakiko nyuma, kwani Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba amekwisha tangaza nia ya kugombea urais kwa mara ya nne mwaka 2015.

Mtanzania
 
M

mecy

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2012
Messages
422
Likes
0
Points
0
M

mecy

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2012
422 0 0
Rasimu ya katiba mpya inaonekana kuitesa sana Ccm kwa kuhofia ndo mwiba kwao,wameahidi kutoipitisha kwa 100%.nadhan kwa katiba hi endapo vurugu itatokea basi ni ccm watakuwa ndo waanzilishi hakika,wananch tusikubali ccm kutuandalia katiba ya nch yetu,
hakika wananch tusikubali kamwe ccm watupangie katiba.
 
M

mecy

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2012
Messages
422
Likes
0
Points
0
M

mecy

JF-Expert Member
Joined Jul 16, 2012
422 0 0
mtajiju ccm.huo ndo mwanzo tu,tunashukuru anguko la ccm sasa tunaliona dhahiri.
 
Shine

Shine

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2011
Messages
11,498
Likes
27
Points
0
Shine

Shine

JF-Expert Member
Joined Feb 5, 2011
11,498 27 0
Rasimu ya katiba mpya inaonekana kuitesa sana Ccm kwa kuhofia ndo mwiba kwao,wameahidi kutoipitisha kwa 100%.nadhan kwa katiba hi endapo vurugu itatokea basi ni ccm watakuwa ndo waanzilishi hakika,wananch tusikubali ccm kutuandalia katiba ya nch yetu,Kamati kuu ya ccm kukaa jumatatu kujadili,mtajiju,
Weka source tujadili ucjekuwa umekurupuka
 
Mtali

Mtali

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2011
Messages
2,527
Likes
521
Points
280
Mtali

Mtali

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2011
2,527 521 280
Chenga ya mwili hiyo. Mtaona linalofuata.
 
Capt Tamar

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2011
Messages
9,035
Likes
7,108
Points
280
Capt Tamar

Capt Tamar

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2011
9,035 7,108 280
Nani kakwambia ni rasimu nzuri?
 
M

Mr.Busta

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2011
Messages
672
Likes
3
Points
35
M

Mr.Busta

JF-Expert Member
Joined Mar 24, 2011
672 3 35
Alisema hawawezi kupinga asilimia 100 na hawawezi kuikubali asilimia 100,kwasababu hawajaisoma hivyo wataijadi kwenye kikao kitakacho keti hivi karibuni na mwenyekiti wao JK.source ITV
 
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Messages
18,936
Likes
1,608
Points
280
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2013
18,936 1,608 280
mkuu hongera kwa kupotosha lakini kwa vile wote tulimsika kinana wakati anazungumzia huwezi kutudanganya hata kidogo alisema kwa sababu alisema hawataipinga kwa asilimia zote wala hawataikubali kwa asilimia zote mpaka watakapo kaa kamati kuu ambayo inakaa j3 baada ya hapo ndipo watatoa maoni yao kama chama ila kwa sasa si wakati mwafaka wa kutoa tamko juu ya rasimu.
 
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Messages
18,936
Likes
1,608
Points
280
Simiyu Yetu

Simiyu Yetu

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2013
18,936 1,608 280
Weka source tujadili ucjekuwa umekurupuka
mkuu huyu jamaa muongo jana kinana alihojiwa na wandishi wa habari juu ya hiyo rasimu,akasema hivi hatuwezi kusema ni mbaya au nzuri kwani hatujapata mda wa kuichambua ila j3 watakuwa na kikao cha nec watapta mda wa kuijadili ndipo watoe maoni ya chama.
 
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
2,274
Likes
14
Points
0
Luteni

Luteni

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
2,274 14 0
Chama cha Mapinduzi kimeitisha kikao cha dharura cha Kamati kuu kujadili rasimu ya katiba.

  • Kufanyika Jumatatu ijayo
  • Kinana: Hatuungi mkono rasimu kwa asilimia 100

=======

*Yaitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu
*Mapendekezo ya Serikali tatu yazua jambo

HATUA ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutangaza rasimu ya Katiba mpya siku chache zilizopita, imeibua fukuto jipya la kisiasa lenye mwelekeo wa kuipinga.

Tayari baadhi ya wanasiasa kutoka vyama mbalimbali hususan wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamekwishakaririwa wakieleza kutokubaliana nayo kwa madai kuwa haiendani na mfumo wa siasa za kileo na kwamba imelenga kuongeza mzigo wa uendeshaji wa Serikali.

Mbali na wanasiasa mmoja mmoja, waliokwishatoa maoni yao yenye mwelekeo wa kutokubaliana na baadhi ya vipengele katika rasimu hiyo, CCM kimetangaza kuitisha kikao cha dharura cha Kamati Kuu (CC) kwa ajili ya kuijadili.

Tangazo la kuitishwa kwa CC ya CCM, lilitolewa mjini Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wake, Abdulrahaman Kinana, mbele ya waandishi wa habari ambaye alieleza kuwa itakutana Jumatatu ya wiki ijayo, kwa ajenda moja tu ya kupitia kwa undani rasimu ya Katiba mpya.

Taarifa kutoka vyanzo vya ndani ya chama hicho, zimeeleza kuwa mjadala unatarajiwa kuwa mkali wakati wa kujadili suala la Serikali tatu, ambalo tangu kutangazwa kwa rasimu hiyo ikipendekeza hivyo, baadhi ya vigogo waliokwishatangaza au kuonyesha nia ya kuwania urais wamekuwa katika sintofahamu ya nini cha kufanya.

Ni sintofahamu hiyo, inayoonekana kukikumba pia CCM ambacho kupitia kwa Kinana kimeeleza kuwa CC itakayoketi Jumatatu, itaangalia kwa undani iwapo rasimu ya Katiba mpya, itakidhi matakwa halisi ya wakati huu.

“Siwezi kuzungumzia msimamo wa chama kuhusu rasimu hiyo kwa sasa hadi Kamati Kuu ya chama, itakapokuwa imekaa Jumatatu ijayo.

“Si busara kuharakisha kuzungumzia suala hilo kabla chama hakijakaa na kuichambua kipengele kwa kipengele, kuona kama inakidhi hali halisi ya matakwa ya kisiasa tuliyo nayo sasa,” alisema Kinana.-Wakati Kinana akieleza hayo, duru za kisiasa kutoka ndani ya CCM, zinaeleza kuwa Rasimu ya Katiba mpya imeibua hali na wasiwasi kwa vigogo wa chama hicho wanaohofia chama chao kupoteza nguvu za mamlaka ya dola kutokana na upepo wa kisiasa unavyovuma sasa nchini.

Wadadisi na wafuatiliaji wa mambo walio ndani ya CCM, wanaeleza iwapo muundo wa Serikali tatu za Zanzibar, ya Tanzania Bara na ile ya Jamhuri ya Muungano kama zilizopendekezwa na Tume ya mabadiliko ya Katiba utaridhiwa, CCM kinaweza kuambulia ukuu wa Serikali ya Muungano pekee.

Imani hii ya wadadisi na wafuatiliaji wa mambo, inajengwa katika msingi wa uungwaji mkono na wananchi kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa upande wa Tanzania Bara na Chama cha Wananchi (CUF) kwa upande wa Zanzibar.

Kwa msingi huo, haina shaka kuwa CUF ambacho kina nguvu kubwa ya kisiasa kwa upande wa Zanzibar, kinaweza kuibuka kidedea katika kinyang’anyiro cha urais, huku Chadema kinachoendelea kujipatia umaarufu na uungwaji mkono mkubwa wa wananchi kikichukua udhibiti wa Serikali ya Tanzania Bara na kukiacha CCM kikibaki na udhibiti wa Serikali ya Muungano ambayo kinaweza kushinda kutokana na historia yake ya kusaka ushindi wa jumla.-

Wakati wadadisi na wafuatiliaji wa mambo wakitoa tathimini hiyo kwa upande wa vyama, wachambuzi wa siasa za ndani ya CCM wameeleza kuwa, iwapo chama hicho kitapoteza nguvu ya udhibiti za Serikali za Tanzania Bara na ile ya Zanzibar na kubaki na Serikali ya Muungano pekee, hilo linaweza kuwa anguko lake la kiuchumi.

Inaelezwa CCM kikiwa na udhibiti wa Serikali ya Muungano, hakitakuwa na ardhi ambayo kimekuwa kikiitegemea zaidi kwa ajili ya kujiendesha kiuchumi jambo ambalo litakifanya kitegemee zaidi misaada ya wahisani.

Baadhi ya wataalamu wa uchumi, waliozungumza na gazeti hili kwa sharti la majina yao kuhifadhiwa kuhusiana na mwenendo huo wa mambo, walieleza kuwa CCM kikiwa na udhibiti wa Serikali ya Muungano, hakitaweza kujiendesha na pia kitashindwa kuwahudumia wananchi kwa sababu kitakuwa tegemezi kwa wafadhili kama vilivyo vyama vya upinzani hivi sasa.Vyama vitavyonufaika na mfumo mpya wa uundwaji wa Serikali kama ilivyopendekezwa kwenye rasimu, ni kile ambacho kitakuwa na udhibiti wa dola ya Zanzibar, ambacho kitadhibiti ardhi, rasilimali na uchumi wa jumla na kile ambacho kitashika dola Tanzania Bara ambacho pia kitakuwa na ardhi na kumiliki rasilimali za nchi.

Mambo haya ndiyo yanayoonekana kuwaumiza vichwa wanasiasa na vyama ambavyo vimekuwa vikipambana kuwania ukuu wa dola, ambapo tangu Juni 3, siku ambayo Jaji Joseph Warioba, alitangaza rasimu ya Katiba mpya iliyokuwa ikipendekeza kuwepo kwa muundo wa Serikali tatu, fukuto la kisiasa kwa wanasiasa walioonyesha tamaa ya urais na vyama vinavyoiwinda Ikulu, limepanda.Ndani ya CCM, kuna vigogo kadhaa ambao wameonyesha nia ya kugombea urais mwaka 2015, ambao Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano), Stephen Wassira, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta.

Kwa upande wa Chadema, watu ambao wanatajwa kuonyesha nia ya kugombea urais ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willbrod Slaa, Naibu Katibu Mkuu, Kabwe Zitto na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Lakini Chama cha Wananchi (CUF) nacho hakiko nyuma, kwani Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba amekwisha tangaza nia ya kugombea urais kwa mara ya nne mwaka 2015.

Mtanzania
 
Tuko

Tuko

JF Bronze Member
Joined
Jul 29, 2010
Messages
11,192
Likes
435
Points
180
Tuko

Tuko

JF Bronze Member
Joined Jul 29, 2010
11,192 435 180
Kama hawaungi mkono, ina maana hawaungi mkono matunda ya kazi waliyoianzisha na kuiongoza. Sasa hapa nadhani wananchi tusiahanhaike na hii rasimu tena, bali tuwaondoe CCM madarakani, tuweke hapo watu wenye uwezo wa kusimamia upatikanaji wa katiba mpya...
 
M

mageuzi1992

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2010
Messages
2,511
Likes
18
Points
0
M

mageuzi1992

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2010
2,511 18 0
Nashukuru kwamba kwa ishara hizi wanazotuonyesha tunawatambua wakoje.......na kama tutawaaachia mchakato nini kitatokea!!!
 
Mvaa Tai

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2009
Messages
6,177
Likes
2,230
Points
280
Mvaa Tai

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2009
6,177 2,230 280
Kama hawaungi mkono, ina maana hawaungi mkono matunda ya kazi waliyoianzisha na kuiongoza. Sasa hapa nadhani wananchi tusiahanhaike na hii rasimu tena, bali tuwaondoe CCM madarakani, tuweke hapo watu wenye uwezo wa kusimamia upatikanaji wa katiba mpya...
Kuna tetesi kwamba Warioba kawa-surprise ameenda kinyume kabisa na maelekezo ya Usalama wa Taifa, kuna habari kwamba kuna maelekezo walimpatia Warioba jinsi ya kuiandaa hiyo Rasimu, ikiwa ni kuhakikisha hakuna mazingira yatakayo fanya kuwe na Tume ya Taifa ya uchaguzi iliyo huru, kuweka mazingira ambayo hayataathiri namna Bunge letu linavyo endeshwa na kutokuweka mazingira yatakayopelekea kuvunjwa kwa Muungano. Huenda walijisahau walidhani Warioba ni Jaji Lewis Makame au Lubuva
 
masanjasb

masanjasb

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Messages
2,364
Likes
21
Points
135
masanjasb

masanjasb

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2011
2,364 21 135
Rasimu ya katiba hii imegusa mitaji yao,deal zao,wizi wao,uonevu wao,pamoja na kwamba haijawabana sana kwa vile wanapenda kuchukua vyote vilivyo mbele yao na nyuma yao,but kwa rasimu hii sisi wananchi tunapakupumulia.

Rasimu hii inamapungufu kiasi,kama swala la rasimali zetu hasa madini.gesi,wanyama,na hata ardhi na haki ya msingi ya kila raia havijawekwa hadharani plus swala linaloangusha uchumi wa Taifa letu"RUSHWA" nalo halijawekwa bayana.

Na swala la tume huru itakayodhibitishwa na Rais mmmh hili nalo no
pili jaji mkuu asiteuliwe na Rais na hata mkuu wa majeshi nae atokane na sera za jeshi na taratibu za jeshi,ccm hawajui kuwa haya yatakuja kuwasaidia siku za usoni kwani upinzani utakuja shika madaraka na ili kumzibiti rais kama atafanya usanii kama sasa ni rahisi zaidi kuliko sasa ambapo kuna kinga ya Rais kutoshitakiwa,ngoja kazi hii tuyaachie mabaraza ya katiba japo robo 3ya mabaraza hayo niya chama kipya cha kina juliana
 
Polisi

Polisi

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Messages
2,090
Likes
40
Points
145
Polisi

Polisi

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2010
2,090 40 145
Mimi nawaunga mkono na nawapongeza sana. Hii inatuonesha kwamba Tume ya KATIBA ilikuwa huru na ilifanya kazi yake bila kushurutishwa na mtu. Lakini pia CCM kama mdau katika rasimu ya katiba ana haki ya kutoa maoni kama ambavyo tunategemea vyama vingine kutoa msimamo wake ingawa naona vyama vingine vimeshafungwa midomo kwa aibu kwani walitegemea baadhi ya mambo wanayoyataka wao hayatakuwepo, bahati nzuri yamewekwa. LABDA waje na lingine
 
S

Sometimes

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2010
Messages
4,562
Likes
370
Points
180
S

Sometimes

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2010
4,562 370 180
Katiba yetu mpya ni kwa ajili wa watanzania milioni 45 na siyo kikundi cha watu milioni5!
 
only83

only83

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2010
Messages
5,342
Likes
531
Points
280
only83

only83

JF-Expert Member
Joined Oct 15, 2010
5,342 531 280
CCM ni wanafiki sana, ni hawa waliokuwa wakisema mazuri ya kamati, na walienda mbali kuwatukana watu waliokuwa wanahoji baadhi ya udhaifu wa Tume. Leo baada ya kuona maslahi yao yameguswa ndani ya Rasimu wanakuja juu. Huu ndio umangimeza tunaosema kila siku. Wanapaswa kufahamu kuwa mabadiliko uwa ni ngumu sana kuyazuia, yanakuja kama upepo na yoyote ambaye yuko mbele kwa lengo ya kuyapinga atasukumwa mbali na upepo huo.
 
P

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2012
Messages
12,498
Likes
2,646
Points
280
P

Precise Pangolin

JF-Expert Member
Joined Jan 4, 2012
12,498 2,646 280
Hii Rasimu imekuwa kama kaburi la CCM inawafanya wa weweseke kama wameshikwa na degedege
 
Tuko

Tuko

JF Bronze Member
Joined
Jul 29, 2010
Messages
11,192
Likes
435
Points
180
Tuko

Tuko

JF Bronze Member
Joined Jul 29, 2010
11,192 435 180
Kuna tetesi kwamba Warioba kawa-surprise ameenda kinyume kabisa na maelekezo ya Usalama wa Taifa, kuna habari kwamba kuna maelekezo walimpatia Warioba jinsi ya kuiandaa hiyo Rasimu, ikiwa ni kuhakikisha hakuna mazingira yatakayo fanya kuwe na Tume ya Taifa ya uchaguzi iliyo huru, kuweka mazingira ambayo hayataathiri namna Bunge letu linavyo endeshwa na kutokuweka mazingira yatakayopelekea kuvunjwa kwa Muungano. Huenda walijisahau walidhani Warioba ni Jaji Lewis Makame au Lubuva
Kwa kiasi kikubwa Warioba amejitahidi kumalizia ngwe yake ya kulitumikia taifa hili kwa heshima. Naamini hata siku akiondoka atastahili heshima zote. Nilikuwa na wasiwasi the wat alivyoendasha suala la uundwaji wa mabaraza ya katiba, nikawa namhurumia kuwa kwa miaka yote aliyotumikia taifa hili, leo anakubali kuja kuhitimisha kwa aibu!!!
 
Feedback

Feedback

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2011
Messages
7,997
Likes
475
Points
180
Feedback

Feedback

JF-Expert Member
Joined Mar 14, 2011
7,997 475 180
Mimi nawaunga mkono na nawapongeza sana. Hii inatuonesha kwamba Tume ya KATIBA ilikuwa huru na ilifanya kazi yake bila kushurutishwa na mtu. Lakini pia CCM kama mdau katika rasimu ya katiba ana haki ya kutoa maoni kama ambavyo tunategemea vyama vingine kutoa msimamo wake ingawa naona vyama vingine vimeshafungwa midomo kwa aibu kwani walitegemea baadhi ya mambo wanayoyataka wao hayatakuwepo, bahati nzuri yamewekwa. LABDA waje na lingine
Wewe ni wa ajabu hebu soma tena nilipo bold uone ulichoandika, hivi wewe ukipata ulichokitaka hata kwa 80% aibu itatoka wapi tena, au ulikuwa unamaanisha ndivyo sivyo.
 
Forum statistics

Threads 1,274,224
Members 490,637
Posts 30,505,510