Kamati kumhoji waziri kuhusu operesheni Loliondo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamati kumhoji waziri kuhusu operesheni Loliondo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Oct 3, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 28,281
  Likes Received: 3,191
  Trophy Points: 280
  Kamati kumhoji waziri kuhusu operesheni Loliondo

  Exuper Kachenje


  WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Shamsa Mwangunga, atalazimika kutoa ufafanuzi mbele ya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, kuhusu operesheni ya kuhamisha wananchi huko Loliondo, wilayani Ngorongoro.


  Hatua hiyo inafuatia taarifa zinazohusu mkanganyiko kuhusu operesheni hiyo ya kuwahamisha wananchi kutoka katika pori tengefu ambalo linadaiwa kuwa sasa amepewa mwekezaji wa kigeni.


  Pia kuna madai kuwa mwekezaji huyo amekuwa akiendesha vitendo vya unyanyasaji dhidi ya wananchi wa eneo hilo, vikiwemo vinavyokiuka haki za binadamu, bila kuchukuliwa hatua.


  Ratiba ya vikao vya Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira iliyotolewa na ofisi ya Bunge Ijuma lililopita, inaonyesha waziri amepangiwa kutoa ufafanuzi wa opersheni hiyo.


  Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Mwangunga amepangiwa kufanya hivyo Oktoba 10 mwaka huu wakati kamati hiyo itakapokutana katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam.


  "Ijumaa 09/10/09, Waziri kutoa ufafanuzi kuhusu operesheni inayoendelea Loliondo," inaonyesha ratiba hiyo ambayo Mwananchi ina nakala yake.


  Hivi karibuni waziri Mwangunga alikaririwa akisema kuwa waliohamishwa katika pori hilo si Watanzania na kwamba jamii ya Wamasai kutoka Kenya.


  Kwa mujibu wa waziri huyo, watu hao walifuata malisho, kufuatia ukame uliikumba nchi yao na kusababisha mifugo kukosa malisho.


  Waziri wa Maliasili na Utalii, pia alisemahakuna ukiukwaji wa haki za ubinadamu uliofanyika katika operesheni hiyo.


  Alisema wizara yake kwa kushirikiana na Tume ya Upangaji wa Matumizi ya Ardhi, imeazimia kutenga maeneo ya pori tengefu, ardhi ya vijiji kwa njia shirikishi.  Katika eneo hilo kuna zaidi ya taasisi 30 zinazofanya kazi huku baadhi zikitajwa kuhusika na mvutano uliopo.


  Mwangunga amezielezea tatsisi hizo kuwa zinashindana kibiashara.


  Alisema wafugaji wana haki ya kuendelea kuishi katika maeneo mengine ya pori la Loliondo, ambayo si tishio kwa usalama wao.
   
 2. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wakishamuhoji na kugundua ana hatia atachukuliwa hatua gani??????
  Ndio danganya toto kama kawaida kwa wananchi wa Loliondo wanaoitwa wamasai wa kenya. funika kombe mwanaharamu apite.
  Huko manyara na kwingineko watu wanakufa njaa ilhali serikali yao na JK wanafanya sherehe za kifahari kila hoteli hapa Arusha.
  Waache ujinga kabisa.
   
 3. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 673
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Hivi hii hotel anayoitumia sana JK ni ya serikali au ni ya mtu binafsi? Nchi ilishauzwa siku nyingi na ndo maana wamasai wa loliondo wanapo jitetea na kudai haki yao wanahitwa wakenya.
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,235
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Hakuna cha kamati wala nini!

  Kama kuna maswali atahojiwa, basi ashapewa yote tayari na hiyo kamati-uchwara.
   
Loading...