Kamati inayochunguza mauaji yaongezewa siku 7, ni yale ya Mtwara, Tanga

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameridhia kuongeza muda wa siku saba kwa kamati maalum iliyopewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, Tanga.

Kamati hiyo iliyoanza kazi Februari 4, 2022 ilipaswa kukamilisha ripoti yake ndani ya siku 14, zilizoishia Februari 17, 2022, lakini kutokana na ukubwa wa kazi na mahitaji ya kujiridhisha na baadhi ya masuala, kamati imeomba kuongezewa siku saba kuanzia Februari 17 hadi Februari 23, 2022.

Kamati hiyo iliundwa na Waziri Mkuu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan, alilolitoa Februari 4, 2022 mjini Magu, Mwanza akiwa njiani kuelekea Musoma, Mara kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.

Aidha, Waziri Mkuu ametoa wito kwa mamlaka husika kuendelea kutoa ushirikiano kwa kamati ili iweze kuikamilisha kazi hiyo kwa wakati na ufanisi.
 
... binafsi nilishangaa kamati inayochunguza jambo zito kama hilo kupewa wiki 2 hadi kukamilisha ripoti! Isingewezekana hata kama wangefanya kazi 18 hrs a day! Hata hiyo wiki moja iliyoongezwa bado ni muda mfupi sana.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameridhia kuongeza muda wa siku saba kwa kamati maalum iliyopewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, Tanga.

Kamati hiyo iliyoanza kazi Februari 4, 2022 ilipaswa kukamilisha ripoti yake ndani ya siku 14, zilizoishia Februari 17, 2022, lakini kutokana na ukubwa wa kazi na mahitaji ya kujiridhisha na baadhi ya masuala, kamati imeomba kuongezewa siku saba kuanzia Februari 17 hadi Februari 23, 2022.

Kamati hiyo iliundwa na Waziri Mkuu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan, alilolitoa Februari 4, 2022 mjini Magu, Mwanza akiwa njiani kuelekea Musoma, Mara kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.

Aidha, Waziri Mkuu ametoa wito kwa mamlaka husika kuendelea kutoa ushirikiano kwa kamati ili iweze kuikamilisha kazi hiyo kwa wakati na ufanisi.
Hivi ni kamati gani ya Majaliwa imewahi kutoa taarifa ikawekwa wazi? Hii soko la Kariakoo vipi kwa mfano?
 
  • Thanks
Reactions: MCN
Mwisho wa siku nahisi hili jambo litapotea kimya kimya, hizi za Majaliwa ni mbwembwe tu.
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameridhia kuongeza muda wa siku saba kwa kamati maalum iliyopewa jukumu la kuchunguza mauaji yaliyofanyika Mtwara na Kilindi, Tanga.

Kamati hiyo iliyoanza kazi Februari 4, 2022 ilipaswa kukamilisha ripoti yake ndani ya siku 14, zilizoishia Februari 17, 2022, lakini kutokana na ukubwa wa kazi na mahitaji ya kujiridhisha na baadhi ya masuala, kamati imeomba kuongezewa siku saba kuanzia Februari 17 hadi Februari 23, 2022.

Kamati hiyo iliundwa na Waziri Mkuu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan, alilolitoa Februari 4, 2022 mjini Magu, Mwanza akiwa njiani kuelekea Musoma, Mara kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya CCM.

Aidha, Waziri Mkuu ametoa wito kwa mamlaka husika kuendelea kutoa ushirikiano kwa kamati ili iweze kuikamilisha kazi hiyo kwa wakati na ufanisi.
Hizi Kamati za huyu Majaliwa hazijawahi kuleta mrejesho hata siku moja watu wanakuka pesa ya Vikao tu. Kama kuna mahali pana kosa na wahusika wanajulikana nini haja ya kamati? Hivi ni wapi viongozi wanakosea? JPM hakulea huu ujinga.
 
Back
Top Bottom