Kamati ilipendekeza tanzanite ikatwe nchini


BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
80,664
Likes
117,953
Points
280
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
80,664 117,953 280
Posted Date::12/17/2007
Kamati ilipendekeza tanzanite ikatwe nchini
Na Mwandishi wetu
Mwananchi

WAKATI serikali imeshindwa kusimamia utekelezaji wa agizo lake la kupiga marufuku usafirishaji nje ya nchi madini ya tanzanite ghafi, Kamati ya Madini ya Mkuu wa Majeshi Mstaafu, Jenerali Robert Mboma nayo ilipendekeza madini hayo yakatwe nchini ili kuongeza ajira kwa watanzania.

Ili kutekeleza suala hilo, kama ti ilipendekeza kuanzishwa kwa eneo huru la uzalishaji wa bidhaa za kuuza nje (EPZ) moja mjini Arusha au Mererani mkoani Manyara ili kuongeza thamani ya madini ya tanzanite ili kuongeza pato la serikali na udhibiti wa madini hayo.

Ripoti ya kamati hiyo ya mwaka 2001, ilipendekeza kuwa madini yaongezwe thamani hapa nchini ili kuongeza ajira, ujuzi na upatikanaji wa fedha za kigeni.

Kamati ya Mboma pia ilipendekeza kwamba sheria ya Mamlaka ya kodi irekebishwe ili kuruhusu kuwapo wakaguzi wa uchimbaji wa madini na maafisa wa kudumu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenye maeneo ya madini watakaokuwa wakithibitisha kiasi cha madini alichozalisha mchimbaji.

Aliyekuwa Waziri wa Nishati na madini, Daniel Yona mwaka 2003 wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara yake bungeni alisema serikali imepiga marufuku usafirishaji wa madini ya tanzazite ghafi kwenda nje ya nchi. Hata hivyo, mpaka sasa agizo hilo halijatekelezwa.

Nakala ya ripoti hiyo ambayo Mwananchi inayo inaeleza kwamba katika marekebisho hayo, wakaguzi wa madini wawe na madaraka ya kuingia eneo la mgodi unaozalisha madini na kufanya ukaguzi wakiwa wamefuatana na maafisa wa TRA, ili kujua kiasi cha madini kilichozalishwa na kiwango anachostahili kulipa mwekezaji.

Kuhusu kitalu C kupewa mwekezaji mkubwa wa kigeni yaani Merelani Minging Ltd ambalo hivi sasa linamilikiwa na kampuni ya Tanzanite One, kamati hiyo ilipendekeza kwamba ni vyema wachimbaji wadogo wa Tanzania waruhusiwe kuchimaba madini hayo ambayo hayana ushindani katika soko la kimataifa ili waweze kuinua vipato vyao.

Katika mapendekezo yake ya jumla kamati hiyo ilipendekeza kwamba Sheria ya madini Namba 5 ya mwaka 1998 ifanyiwe marekebisho ili watanzania waweze kunufaika na madini.

Tume ya hivi sasa ya madini iliyoteuliwa na Rais Kikwete pamoja na mambo mengine, ina kazi ya kuchambua mfumo wa kodi unaotumika katika sekta ya madini na kupitia mfumo wa usimamizi wa shughuli za uchimbaji mkubwa wa madini unaofanywa na serikali.

Kamati hiyo iliyopewa kipindi cha miezi mitatu kukamilisha kazi yake pia inajukumu la kukutana na taasisi zinazosimamia madini na wadau wengine na kutakiwa kutoa taarifa yenye mapendekezo pamoja na kupitia mikataba ya madini na nyaraka nyingine zitakazohusu migodi mikubwa nchini.

Kuundwa kwa Kamati hiyo kunafuatia hoja binafsi ya Zitto Kabwe aliyoitoa bungeni kutaka kuundwa kwa Kamati Teule ya kuchunguza mazingira ya kusainiwa kwa mkataba wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi huko Uingereza na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi Februari mwaka huu.

Baada ya kuwasilisha hoja hiyo, Kabwe alifungiwa kuhudhuria vikao vya Bunge hadi hapo Januari mwakani, hatua ambayo iliibua mjadala mkubwa miongoni mwa makundi mbalimbali wakihoji sababu za kumfungia mbunge.

Kamati hiyo yenye jumla ya wajumbe kumi na mmoja itakuwa chini ya uenyekiti wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu, Jaji Mark Bomani. Wengine Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishina wa Sera Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa na Mbunge wa Kyela (CCM), Dk. Harrison Mwakyembe.

Wengine ni Mbunge wa Msalala (CCM),Ezekiel Maige, Peter Machunde kutoka Soko la Hisa, Dar es Salaam (DSE), Mkaguzi wa Mahesabu kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Mahesabu, PriceWater Coopers, David Tarimo ambaye ni mtaalam wa masuala ya kodi, Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kejo na Iddi Simba

Kamati nyingine za madini ambazo serikali imewahi kuziunda ni pamoja na ile Brigedia Jenerali Mang'enya ya mwaka 2003, Dk Kipokola kati ya mwaka 2003 na 2004 na ya Lawrence Masha. 


 
Alpha M.

Alpha M.

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2015
Messages
1,041
Likes
1,567
Points
280
Alpha M.

Alpha M.

JF-Expert Member
Joined May 15, 2015
1,041 1,567 280
Haya mambo ya kamati za madini kumbe yalianza miaka dahali
 
Copenhagen DN

Copenhagen DN

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2014
Messages
6,071
Likes
8,351
Points
280
Age
29
Copenhagen DN

Copenhagen DN

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2014
6,071 8,351 280
Kagame na Sizonje nyinyi endeleeni tu.
 
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Messages
22,879
Likes
26,929
Points
280
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2007
22,879 26,929 280
Mkuu umepotea kweli hapa JF!!
 
D

DrLove69

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2018
Messages
2,539
Likes
2,807
Points
280
D

DrLove69

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2018
2,539 2,807 280
Kuna majitu yanafaa kunyongwa kabisa mpaka kifo na historia yao ipotee katika kizazi hiki ili Taifa hili liweze kukiepuka hiki kikombe cha laana kinachotuandama Watanzania na vizazi vyetu.
 
M

Maharo

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2016
Messages
2,829
Likes
1,748
Points
280
M

Maharo

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2016
2,829 1,748 280
Kuna majitu yanafaa kunyongwa kabisa mpaka kifo na historia yao ipotee katika kizazi hiki ili Taifa hili liweze kukiepuka hiki kikombe cha laana kinachotuandama Watanzania na vizazi vyetu.
shindwa wengine hatujalaniwa.
 
D

DrLove69

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2018
Messages
2,539
Likes
2,807
Points
280
D

DrLove69

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2018
2,539 2,807 280
shindwa wengine hatujalaniwa.
Kama haujalaaniwa ungepita kimya. Kwa kuninukuu umedhihirisha pasi na shaka laana iliyo juu yako na ndio maana ukajiita MAHARO.
 
M

Maharo

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2016
Messages
2,829
Likes
1,748
Points
280
M

Maharo

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2016
2,829 1,748 280
Kama haujalaaniwa ungepita kimya. Kwa kuninukuu umedhihirisha pasi na shaka laana iliyo juu yako na ndio maana ukajiita MAHARO.
hizo laana ubaki nazo mwenyewe na wanao SHINDWA NA ULEGEE KUJUMUISHA WOTE;)
 
jmushi1

jmushi1

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2007
Messages
19,121
Likes
5,005
Points
280
jmushi1

jmushi1

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2007
19,121 5,005 280
Ikakatiwe Rwanda
 

Forum statistics

Threads 1,238,954
Members 476,289
Posts 29,337,891