Kamata kamata ya viongozi wa CHADEMA: Jeshi la polisi linaihujumu CCM?

fundimchundo

JF-Expert Member
Jul 23, 2010
609
898
Kila viongozi na wanachama wa Chadema wanapokamatwa na polisi, umaarufu wa CDM unaongezeka, huku CCM ikiporomoka.
Viongozi wakuu wa Polisi wanalijua hili. Kwa nini wanaliendeleza?

Kuwakamata Nassari, aka DogoJanja, Heche na wengine ni kuzidi kuipaisha CDM na kuizika CCM.
Lengo la Kamanda Mwema kwa CCM ni lipi? KUIUA KABLA YA 2015?
 
Unajua sasa hivi magamba hawajui wanalo lifanya.Wame kuwa vipofu na huo ni mpango wa MUNGU.Kila wanalo wafanyia magwanda linawapa credits. Vyombo wanavyo tegemea kuwalinda ni polisi na mahakama ambavyo sasa hivi vimekuwa "LIMPING GROUND" YA MAGWANDA. Hao polisi na mahakama ndio wata wapigia kura 2015?
 
Kikwete anarahisisha kuiua ccm. Anatamani isifike hata 2015.

Najiuliza lakini sipati picha.
Yote yanayofanyika nchini ambayo Rais Kikwete anayaona na kuyasikia (kupitia vyombo vya dola), huku akiyafumbia macho, yanakididimiza Chama cha Mapinduzi!
Je, JK naye anajivua gamba kimya kimya?
 
Kila viongozi na wanachama wa Chadema wanapokamatwa na polisi, umaarufu wa CDM unaongezeka, huku CCM ikiporomoka.
Viongozi wakuu wa Polisi wanalijua hili.
Kwa nini wanaliendeleza?
Kuwakamata Nassari, aka DogoJanja, Heche na wengine ni kuzidi kuipaisha CDM na kuizika CCM.
Lengo la Kamanda Mwema kwa CCM ni lipi? KUIUA KABLA YA 2015?

Hizo ni salamu rasmi za Emmanuel Nchimbi ....Huyu kada mafioso wa ccm ...amepelekwa wizara ya mambo ya ndani ya nchi kwa kazi mkaa um..
 
Ukiitwa Polisi maana yake ni kwamba umefunguliwa jalada, huko kunaitwa kukamatwa. Usipoenda utapelekwa unatembelea vidole huku umekamatwa mkanda wa suruali.

Basi tunaomba update ya huko kukamatwa kwao. Vema tujuzane makamanda hawa wako wapi maana ccm wametufanya tuone kila kitu ktk giza la mashaka ya hujuma.
 
Usijali wanaongeza umaarufu wa chama. Ukitaka angalia Rais wa Uganda Yoweri mu7 anavyomtesa mpinzani wake mkuu Dr KIZA BESIGE' mpinzani huyu kupigwa na kukamatwa na Polis wa Uganda ni jambo la kawaida, lakini mu7 hajui ni kiasi gani anamuongezea mpinzani wake huyo umaarufu na ujasiri zaid wakutetea haki za watu wa Uganda.

Kinachofanywa na Polis wa Tz ni kuiongezea CDM nguvu ikachukue dola kirahisi 2015 coz hata hao Maafande wamechoka balaa. MUNGU IBARIKI TANZANIA PAMOJA NA VIONGOZI NA WAFUASI WOTE WA 'CHADEMA'.
 
wamemkamata kwa sababu alisema juzi kua yeye ni waziri mkuu wa arusha...sa hapo polisi wanataka kumhoji huo uwaziri mkuu wa arusha kapewa na nani:argue:
 
Kila viongozi na wanachama wa Chadema wanapokamatwa na polisi, umaarufu wa CDM unaongezeka, huku CCM ikiporomoka.
Viongozi wakuu wa Polisi wanalijua hili. Kwa nini wanaliendeleza?

Kuwakamata Nassari, aka DogoJanja, Heche na wengine ni kuzidi kuipaisha CDM na kuizika CCM.
Lengo la Kamanda Mwema kwa CCM ni lipi? KUIUA KABLA YA 2015?
Isije wakamwakyembe hao, tabia ya kuua watu TZ imekithili na sijui kama Polisi wanachukua hatua zozote???? Usa River, Nduruma, Mandela maeneo yote hayo yamekuwa seen of dumped bodies sijui kama kuna uchunguzi wowte wa maana umefanyika!!!

wamemkamata kwa sababu alisema juzi kua yeye ni waziri mkuu wa arusha...sa hapo polisi wanataka kumhoji huo uwaziri mkuu wa arusha kapewa na nani:argue:

Nimesikia mara kadhaa Wakuu wa Wilaya wakijiita ma-Rais wa Wilaya na sijawahi kusikia wakiitwa Polisi kujieleza huo U-Rais wamepewa na nani.
Kumkamata Mheshimiwa Mbunge kwa kujiita Waziri Mkuu ni kumuongezea publicity!
Katika siasa, publicity is everything, na hili linaendelea kuididimiza CCM huku CDM ikipaa chati.
Huoni hili linakiondoa CDM kwenye orodha ya vyama vya msimu na kukifanya chama cha muda wote?
Kwa nini Polisi wanaididimiza CCM?
 
Kama wanavunja sheria halali za nchi ni lazima wakamatwe, hakuna cha kuogopa kama umaarufu unapanda au unashuka.
 
Kama wanavunja sheria halali za nchi ni lazima wakamatwe, hakuna cha kuogopa kama umaarufu unapanda au unashuka.

Wamevunja sheria ipi? Kama hawajavunja sheria yoyote na bado wanakamatwa unashauri nini kifanyike?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom