vampire_hunter007
JF-Expert Member
- Jul 25, 2015
- 1,034
- 2,599
Habari wakuu,
Mimi mgeni humu naomba ruhusa yenu nipost.
Ndani ya wiki hii na iliyopita kumekuwa na kamata kamata kubwa sana ya waendesha bodaboda, wengi wakinyang'anywa pikipiki zao na kulazimika kutoa hadi laki na nusu kuipata, au kutoa rushwa ya elfu 30 mpaka 50.
Nilikuwa nikiongea na mmoja wa hawa madereva ananiambia hata kama mtu ana vibali vyote na kakutwa kapaki sehemu (kisingizio hakitakuwa kuendesha kasi) bado wanakamatwa na bila kupewa maelezo yoyote
Na kama tunavyojua polisi wa nchi yetu, wapo radhi kumgonga huyo dereva wa bodaboda aumie lakini wao wapate pikipiki.
Huu uonevu unafanywa kwa kisingizio gani? Yaani serikali imetoa sababu zipi haswa za kuwakamata na kuwanyanyasa hawa ndugu zetu wanaotafuta rizki ya halali?