Kamari ya kumtosa Lowassa na kumpitisha Makongoro

Travelogue_tz

JF-Expert Member
Sep 28, 2010
848
1,212
CCM wapo katika nyakati ngumu katika kupitisha mgombea wa Urais ambaye anakubalika na Wananchi kwa upande mmoja na watawala kwa upande mwingine. Tathmini inaonesha kuwa wagombea ni wawili tu Yaani anayekubalika na watawala ambao ni Membe, Sitta Mwandosya, Sumaye, Kigwangala, Mwigulu,Wasira Muhongo na Makongoro ambao hawa wanaweza kuunganisha nguvu zao dhidi ya EL ambae sio chaguo la watawala.

Kwa hali hii na utashi wa kimazingira wajumbe karibia wote wa CCM hauwaamini katika dhana ya kupambana na rushwa kwa sababu ni sehemu ya maisha yao, kwa kifupi mgombea atakayeweza kuhonga zaidi wajumbe ndie mwenye nafasi ya kushinda na kupitishwa ambapo EL anabeba ushindi katika hili ukilinganisha na Mgombea wa watawala Makongoro N.

Kumpitisha EL kutahatarisha uhai wa CCM kwa kuwa kundi la wapinga ufisadi halitakuwa salama, like wise kumtosa EL na kumpitisha Makongoro kutaibua vita kubwa na kupelekea CCM kuvunjika vipandevipande, lakini pia kupoteza ushawishi kwa voters, hii inatokana na EL kuwaandaa kisaikolojia Wananchi na wana CCM kuwa yeye ndie mgombea pekee wa CCM anayefaa. Hii ni kamari ambayo vyoyote vile utakavyoicheza lazima kuliwa.
 
Kama ccm wana akili, kete yao pekee dhidi ya upinzani ni Lowasa. Tatizo ni woga wa viongozi kwamba huyu jamaa atawalipizia kisasi kwa yale waliyomtendea akiwa nje ya madaraka maana hawakujua kwamba angeendelea kuwa na nguvu hivi mpaka leo.
 

Lowassa,Lowassahadi kero
Kila kukichaLowassa, Lowassa, oooo mtu mawazo yake binafsi tu anakujana kusema ametumwa na wanainchi katikaeneo lake mfano mkoa au kanda amshauri lowassa agombee Urais.
Lowassa jamani hafai, mtu anayejitajirishakwa kutumia wadhifa wake katika utumishi wa umma hafai kuwa kiongozi kwa sababusiyo mfano wa kuigwa, yaani kuiba mali za umma siyo sifa ambayo inafaa mtumwingine aige.
Lowassa kuwa kiongozi wa ofisi ya juukutavutia wezi wenzie kuinajisi ofisi hiyo, yaani kama ukifuga fisi tegemeafisi wenzie kumtembelea fisi mwenzao hawezi kutembelewa na swala.
Jamani Lowassahafaiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
Kikwete, Mangula hebu mwambieni huyo mtu kwamba hanasifa za kiti cha urais, anaweza mambo mengine na siyo urais, ni nyie mnamlealeamnamchelewesha mpeni makavu ya moja kwa moja na wala siyo mafumbo mafumbo
CC.

  1. Jajaya Mrisho Kikwete
  2. Jack Zoka
  3. Philip Mangula
  4. Abdrahiman Kinana
  5. Benjamin Mkapa- Uliwakemea maaskofuukasema na majoho yao haiwezekani serikali tatu kwa sababu baba wa taifaalikataza mbona Lowassa humkemei? Mnafiki mkubwa wee.
  6. Ali Hassan Mwinyi
  7. Nape Nnawiye
  8. Delvis Adolf Mwamunyange
  9. Ernest Hamis Mangu
  10. JohnKomba-na unafiki wako, kama Lulu Michael kakukomba mali zote usitegemee uibukiekatika kumpigia dabe fisadi Lowassa, kufa na lywako
  11. RostamAzizi –ikulu siyo pango la walanguzi unatumia mapesa yako ya wizi ili umwekeLowasaa ikulu ili uwe ndio uchochoro wako.
 
pamoja na kuwa ni wazi ukawa inaenda ikulu October kuwasaidia magamba kwenye hii kamari angalau mbaki cha cha upinzani imara option ni mbili. moja tangazeni safari hii ni zamu ya mwanamke au pili tangazeni hii ni zamu ya Zanzibar kutoa mgombea hapo mtabaki salama kama chama cha upinzani
 
Si Kweli, EL anakubalika na kundi dogo sana la wananchi nje ya CCM,kumptisha ni kukiua chama. Ngoja wampitishe, wapinzani washangilie..
 
CCM sio wajinga kiasi hicho, unaowaona wote watia nia wanaishi maisha yao kutegemea ccm kuwa madarakani, Kwa akili ya kawaida tu nani ampitishe makongoro ambae hauziki? Wanajua kuanguka kwa ccm ndio kuanguka kwa family zao,
Hao wote wanaomponda lowasa ndio watakuja kumshangilia baadae, hakuna anaeuzika ccm zaidi ya Lowassa na wao wanalijua hilo,
 
"Katika hali ya kunishangaza, nilikuwa nabadilishana mawazo na mzungu mmoja raia
wa Ujerumani kwenye N.G.O yake. Katamka maneno yaliyonistaajabisha.
Tumeongea mambo mengi lakini baadae tukaanza kuongelea siasa. Akasema kuna
yule aliekuwa waziri mkuu anaitwa Lowasa, nimeona sasa mnampenda sana. Mimi
nikamjibu inaonekana kuna Watanzania wanampenda awe Rais. Yule Mzungu
akaniuliza, si yule aliejiuzuru kwa sababu ya Corruption?, nikamjibu ndie huyo.
Akasema, wakati ule alionekana amekula Rushwa, sasa anataka kuwa Rais na watu
wanamuunga mkono!, akaongezea kwa kusema how can you easily forget?, how can
you easily change your mind?, yaani mnawezaje kuwa wasahaulifu namna hii,
mnawezaje kubadili fikra zenu haraka hivi juu yake?, hapo mimi nikabaki na
kigugumizi. Akaongeza, au Lowasa amewahi kuwaelezea uhusika wake na hizo
corruption?, mimi nikamjibu hapana. Akasema tena, Or was he cleared by the court?
yaani, je Mahakama iliona hana hatia?, nikamjibu kesi haijawahi kwenda Mahakamani.
Akauliza, then which criteria do you use to support him? Nikamjibu kwakweli sijui wananchi wanatumia kigezo gani.
Yule mzungu akasema, anyway, you are such amazing country, with this style it may
take you so many years to change."

Sent as received.
 



Ila kumbuka kuwa CCM ilishakumbana na kizungumkuti kama hiki mara nyingi sana toka miaka ya 60s na kila mara ndani ya miaka kumi kumi [10] ya awamu CCM upita kwenye hatua hizi, mfano wa haya ni Salim A. Salim,David Msuya, Malechela.Hakika tunaweza kuona zama hizi kama Mtajwa Lowasa kama ana nguvu sana [Ngoma ikilia sana mwisho wake upasuka] na hakika kwa wanaojua chaguzi zilizopita kwenye decades [2] zilizopita Mzee Msuya, Malechela na Bilal kila mmoja kwa namna yake walishapata kuungwa mkono na watu wengi sana kwenye utendaji na chama lakini ajabu mwishoni waligeuka na kuludi ndani ya chama na kuwa watiifu mpaka tunavyoowaona hivi sasa wakiwa na heshima za kuamua mambo ya msingi ya kitaifa na ya chama chao.

Hakika kwa hili la CCM kucontrol mushkeri zinazo anzishwa na watu ndani ya chama chao ni mabingwa tena sio wa Tanzania au Afrika ni mabingwa wa Dunia.Uwa naamini hiki chama pia kina mambo ya ziada ambayo upelekeamimi niliye nje nikitizame kwa jicho la ndani zaidi.Naijifunza mengi sana jinsi CCM inavyopeleka mambo yao.

Kuna Mwanaccm mmoja mtu mzima hivi alipata kuniambia UNAJUA MAANA YA NENO MAPINDUZI... nikamwabia ndio akanimabia nimwambie najua nini kwa neno hilo nikamwambia akaniambia NIJIFUNZE jambo kwa uwepo wa neno ilo hapo na kutamkwa hapo.Na kweli kina kinapoibuka vulugu mechi, sakata , vulumai, songombingo, mtafaruku, kutokueleweka, sintofahamu, mushkeri, patashika, kama viama tunavyo viona vya ishara za kudondoka CCM imeendelea kusimama na kuendelea Kuendesha Nchi.

Hii ngoma inayolia sana ITAPASUKA NA CCM wataendelea na kuongoza Nchi kama ambavyo siku zote wamefanya hivyo.Kuna siku zingine watu waliingia kwenye makao makuu zao huko DODOMA wakiwa viongozi wa Serikali au Wachama lakini wakaondoka kama raia wa kawaida.

Hao ndio CCM ila kwa hili linanipa udadisi mdogo ni nani atashinda safari hii Je ni Mkulima na Mfanyakazi au ni Wafanyabishara.


[h=2]Leo ni mwanzo wa hatima ya Chama cha Mapinduzi, ama kiwe cha matajiri au makabwela[/h]Kuanzia leo tarehe 3/06/2015, chama cha mapinduzi kinaanza safari ya ama kiwe chama cha matajiri [baba benzi] au chama cha wakulima na wafanyakazi [makabwela].

Majaribio haya ya ukinzania ndani ya ccm yalipata kutokea miaka ya 60s yakiwa na sura ya aina hii...lakini kwa uthubutu na uwezo wa kusimama na kusema hapana makabwela waliweza kuandika historia ya aina yake na taifa likasimama kwa sura ambayo leo tunasema ni sura ya taifa la amani na mshikamano.

Kwa ushindi ule ni tanzania ambako watu wa makabila tofauti yapatayo 128 yameweza kuishi pamoja na kuunda taifa unique ambako hakuna ubaguzi wa kubaguana kwa sababu ya dini, kabila, elimu, utajiri ama rangi.

Sasa kwa kuanzia leo hii safari ama matajiri [wafanyabiashara]au wafanyakazi na waakulima mmoja wapo kuibuka mshinid [kidedea] na kuchukua nafasi ya umilki wa chama kilichoasisiwa na wafanyakazi na wakulima ambao kwa jasho lao na umoja wao wameshirikiana na kuifikisha nchi hapa ilipofika sasa.

Leo ndio mwanzo wa chama kupata ceo mpya watake binafsisha chama hicho kwa wafanyabishara au kiongozi atakae kiludisha rasmi mikononi mwa waasisi wake yani wakulima na wafanyakazi.

Swali langu ni kwamba kama chama hiki kuanzia leo mchakato wake ukianza kutayalishwa kuelekea kubinafshwa kwenda mikononi mwa wafanyabishara je wakulima na wafanyakazi wataondoka na bendera yao yenye nyundo na jembe kama alama yenye uthibitisho ya umilki wao?......

Mgombea mtia nia urais charles makongolo nyerere yeye ameshajitokeza na kusema yuko tayari kukipereka chama kwa wakulima na wafanyakazi [makabwela] kama ilivyokuwa tangu zamani za kuasisiwa kwake.wakati huo huo mtia nia edward ngoyai lowasa yeye kasema wazi kuwa itikadiya utajili ndio mlengo na kuwa maskini si mtaji wake kuongoza nchi.

Mtizamo wako mwanajf nani ataibuka mshindi ni nyundo na jembe [alama ya wakulima na wafanyakazi] dhidi ya pesa [alama ya utajili na ufisadi-wafanyabishara] and vice versa is true.


 
CCM sio wajinga kiasi hicho, unaowaona wote watia nia wanaishi maisha yao kutegemea ccm kuwa madarakani, Kwa akili ya kawaida tu nani ampitishe makongoro ambae hauziki? Wanajua kuanguka kwa ccm ndio kuanguka kwa family zao,
Hao wote wanaomponda lowasa ndio watakuja kumshangilia baadae, hakuna anaeuzika ccm zaidi ya Lowassa na wao wanalijua hilo,
Are you serious of what you are commenting?

Kuwa Lowassa ndiye anauzika kuliko wanaccm wote waliotangaza nia?

Hivi hujawahi kusikia ule msemo unaosema kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza?

Hivi EL alikuwa na sababu ipi ya msingi kwa tukio lile la kutangaza nia tu ya kuwania kupeperusha bendera ya CCM kwa nafasi ile ya Urais ateketeze zaidi ya shilingi bilioni moja?

Hivi kwa nchi ambayo watoto wengi wanakaa chini madarasani kwa kukosa madawati.

Hivi kwa nchi ambayo familia nyingi masikini zinashindia mlo mmoja kwa siku.

Hivi kwa makundi hayo ya wananchi wanajisikiaje wanapoona mgombea mmoja kwa kutangaza nia tu ya Urais, anafanya 'kufuru' kwa kikao chake hicho cha kutangaza nia anatumia mabilioni ya shilingi?

Ni dhahiri mtu kama EL anapigana.kufa na kupona ili aingie Ikulu, ili akawapatie 'dili' wapambe wake wafanyibiashara ili 'wajilipe' mabilioni ambayo wamemkopesha mzee wa mamvi kwa ajili ya safari yake ya matumaini!

Ndiyo maana Nyerere alituusia kuwa kwa kuwa Ikulu hakuna biashara yoyote ya kumwezesha mgombea yeyote aliyewekeza mabilioni kwa ajili ya kuingia Jumba hilo kubwa kuzirejesha, mtu huyo anapaswa kuogopwa zaidi ya UKOMA/UKIMWI!
 
ebaeban unakusudia JohnKomba huyu huyu marehemu au kaibuka mwingine tena?
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu, hii si woga, el akiingia tu magogoni kuna vigogo watakao tumia vyoo vya ndoo bila kupitishwa mahakamani nanakuhakikishia. Iwapo alijito au alitoswa ili kuokoa kundi zima katika ile kashfa, alistahili walau kuthaminiwa lakini shukrani aliyopata ni kuitwa fisadi! Walahi nakwambia haendi magogoni kutafuta rizki bali kuadabisha wasaliti!! Na wasaliti wake wanalitambua hilo ndio maana wanatafuta njia ya kuuzima huu moto au njia ya kutorokea iwapo atapenya kule kule magogoni!!
 
CCM wakitaka kutokana na Crisis hii lazima wamshawishi mzee Warioba agombee uraisi..na hii wawe open kabisa kumwomba radhi kwa matusi yote yale yote na mengine waliomkosea…hakika huyu ataunganisha CCM na wapinzani wengi tutampa kura huyu Mzee Warioba…lakini kura yangu hata siku moja haitakwenda kwa wabunge hawa maintarahamwe(CCM) isipokuwa kwa Deo Filikunjombe!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom