Kamanda wa Polisi mstaafu nchini Tanzania, Zolothe Steven amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama tawala (CCM) Mkoa wa Arusha

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
RPC mstaafu achaguliwa mwenyekiti CCM Arusha

Inamaanisha alikuwa na kadi toka akiwa polisi, then hawa na waliopo watatendaje haki kwa upinzani?

===

RPC mstaafu achaguliwa mwenyekiti CCM Arusha

Kwa ufupi

Aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi (RPC) amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuchukua nafasi ya Loota Sanare ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuchukua nafasi ya Dk Stephen Kebwe ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Arusha. Kamanda wa Polisi mstaafu nchini Tanzania, Zolothe Steven amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama tawala (CCM) Mkoa wa Arusha.

Zelothe amechaguliwa leo Jumanne Desemba 17, 2019 na wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa uchaguzi uliosimamiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Hamphrey Polepole.

Akitangaza matokeo, Polepole amesema Zolethe amepata kura 468 dhidi ya kura 339 za waziri wa zamani wa mazingira, Dk Batilda Burian na Bakari Msangi amepata kura 42 kati ya kura zilizopigwa ni 850

Polepole amesema kura iliyoharibika ilikuwa moja huku kura halali zikiwa 849.

Zolothe anachukua nafasi ya Loota Sanare ambaye hivi karibuni aliteuliwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kuchukua nafasi ya Dk Stephen Kebwe ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

RPC mstaafu achaguliwa mwenyekiti CCM Arusha
 
Ningumu kwa hawa wazee waliopo kwenye idara yoyote ile nchini na CCM,labda miaka kadhaa ijayo hii kitu itapungua maana wengi wao wamekuzwa kwenye mfumo wa chama kimoja kwa miaka ile ya chama kimoja.......sasa mtu aliyezaliwa nyuma ya mwaka1965 unategemea nn
 
Huyu Kamanda amewahi kuwa DC huko Musoma na baadaye RC wa Rukwa kipindi cha awamu ya nne
 
Back
Top Bottom