Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza naomba Mwenyekiti wa Waendesha Daladala Jijini Mwanza awekwe ndani mara moja

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
Jana nimemsikia Mwenyekiti wa Waendesha Daladala jijini Mwanza anaitishia serikali kwamba wasipowaondoa Waendesha Bajaji eneo la Buzuruga ataitisha mgomo mara moja!

Ni ajabu sana huyu mtu kubaki uraiani mpaka sasa, anaitishia serikali yeye kama nani?

Kuna watu wameanza kuleta dharau za kipumbavu baada ya JPM kufariki hizi dharau hazikuepo

Unataka waendesha bajaji waondolewe eneo la buzuruga ili wapelekwe wapi? kwako au?

Halafu jamaa anaongea kwa dharau kabisa eti anatoa masaa 72, unatoa saa72 kwa serikali? RPC upo tu umeangalia? OCD upo tu?

Huyu mtu awekwe ndani hata miezi miwili apate adabu.
 
Wana hoja ya msingi kuwekwa ndani sio suluhu ya kudumu, zikutane pande zote upande wa Bajaji na Daladala wayazungumze Serikali isimamie, unachokifanya ni kuifundisha kazi Serikali Mzee, wote wanatafuta.
 
Wana hoja ya msingi kuwekwa ndani sio suluhu ya kudumu, zikutane pande zote upande wa Bajaji na Daladala wayazungumze Serikali isimamie, unachokifanya ni kuifundisha kazi Serikali Mzee, wote wanatafuta.
Alafu ukute daladala wanalipa mapato lakini bado wananyanganyana abiria na bajaj
 
Ina maana kipindi cha meko, wenye malalamiko walikuwa hawatoi??acheni hizo kuna mwingine juzi kuna tukio la ujambazi lilitokea akasemaa jamaani tumekwisha tayari wameanza!!kwani shujaa hayupo!!

kama vile tulikuwa peponi!!kuhusu suala la bajaji ki ukweli ni kero ya mikoa yote!!wao utaratibu wao wa kubeba abiria ni tofauti na daladala, sasa unapoachia bajaji ziwe kama daladala , ni makosa, lazima daladala aumie tu.muulize RC, mbeya ilibidi awe mpole tu alipotaka kutumia ubabe, LATRA, wakampa elimu akaelewa, na kuzipiga marufuku bajaji kutumia route za daladala.
 
Back
Top Bottom