Tetesi: Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala aliyezuia mkutano wa Lipumba "kushughulikiwa"

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,576
217,939
Inasemekana jeshi la Polisi lilishaelekezwa kumlinda Lipumba pamoja na wajumbe wake kwa udi na uvumba , jeshi la polisi lilitakiwa kuhakikisha " MKUTANO MKUU " Unafanyika ili kumvua ukatibu mkuu Maalim Seif pamoja na kuwepo kesi Mahakamani kuhusu uhalali wa uenyekiti wa Lipumba , ambayo hukumu yake ni March 18.

Sasa viongozi wa juu wanashangazwa na Kiherehere cha Polisi kuzuia mkutano huo ( ambao hata hivyo unafanyika kibabe baada ya wakubwa kuubariki ) , inasemekana ni lazima Maalim Seif avuliwe uongozi kabla ya hukumu .

Kamanda aliyeidhinisha katazo hilo atarudishwa makao makuu

Tutaendelea kuwaletea hujuma zote zinazofanyika kwa kadiri ya wajumbe waadilifu watakavyokuwa wanatuvujishia

Profesa Ibrahim Lipumba akiwa ameshika kiuno haamini mara baada ya Mkutano Mkuu .jpg
 
Kiherehere sio kizuri nadhani alifanya kuzuia mkutano ili amfurahishe jiwe dah

Nimegundua kuwa mambo mengine kumbe sio maagizo ya jiwe Bali ni viherehere vya polisi wasaka vyeo

Kumbuka jiwe alisema Kamanda atakae boronga asipelekwe makao makuu Bali ashushwe cheo

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
huyu alijaribu kutumia weredi baada ya kupata malalamiko kutoka kwa Maalim Seif .
 
Hao waliomzunguka Lipumba wote ni Tiss. Kilichopo wazi ni kuwa mamlaka zinavutana. Mahkama inanajisiwa. Lipumba anafanya kazi ya maagizo kila wakati anapata hakikisho la kulindwa.
 
Nimeweka picha hiyo makusudi ili watu wote wajionee .

Wananchi siyo wajinga sana - Magufuli
 
Inasemekana jeshi la Polisi lilishaelekezwa kumlinda Lipumba pamoja na wajumbe wake kwa udi na uvumba , jeshi la polisi lilitakiwa kuhakikisha " MKUTANO MKUU " Unafanyika ili kumvua ukatibu mkuu Maalim Seif pamoja na kuwepo kesi Mahakamani kuhusu uhalali wa uenyekiti wa Lipumba , ambayo hukumu yake ni March 18.

Sasa viongozi wa juu wanashangazwa na Kiherehere cha Polisi kuzuia mkutano huo ( ambao hata hivyo unafanyika kibabe baada ya wakubwa kuubariki ) , inasemekana ni lazima Maalim Seif avuliwe uongozi kabla ya hukumu .

Kamanda aliyeidhinisha katazo hilo atarudishwa makao makuu

Tutaendelea kuwaletea hujuma zote zinazofanyika kwa kadiri ya wajumbe waadilifu watakavyokuwa wanatuvujishia

View attachment 1043975
Wazee wa propaganda....siasa za nyuma ya keyboard.
 
Dunia inafuatikia kwa karibu mno. Huu ni ushahidi mwengine kuwa utawala huu unavuruga nchi na miiko. Mahakama inajaribu kuibeba nchi kama muhimili wa dola. Serikali inamfadhiki Lipumba na kuharibu taswira ya nchi. Huko ndani mamlaka zinabishana. Mara RPC anakuja na maagizo, mara Lipumba anapiga simu kwa waluomtuma. Mara anarudi tena Aibu tuu.
 
Tena niwaambie hapa. Waliontuma Lipumba Kuna kitu kinawatisha kuhusu maalim Seif. Huu mradi wa Lipumba unapitwa na muda na ndio maana hawaana aibu kuharibu bahati Yao hata kama mahkama imezuiya ili lengo la kunvua maalim Seif kwa njia yoyote ile ifanikiwe hata Kama ni haramu. Athari kwa nchi hapa haitazamwi kinachotazamwa ni maslahi. Huu mwiba wa maakin Seif Ni mkali kuliko sindano. Iwe isiwe inatakiwa maalim avuliwe ukatibu.
 
Ni aibu sana kwa nchi !
 
Back
Top Bottom