Kamanda wa Polisi Kinondoni: Sina taarifa ya kukamatwa kwa Gwajima

gasto genaro

JF-Expert Member
Oct 15, 2014
780
554
Dar es Salaam. Wakili Peter Kibatala amesema polisi wamepiga picha nyumbani kwa Askofu wa Kanisa la Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima.

Kibatala ambaye ni wakili wa Askofu Gwajima amesema jana kuwa mbali na kupekuwa na kupiga picha kila kona walikwenda katika kanisa lake lililopo Ubungo.

“Waache wafanye yao na sisi tutafanya yetu kisheria. Kwani hatuwezi kuwazuia Polisi kufanya shughuli yao na baada ya kumaliza na sisi tutajua nini cha kufanya,” amesema Kibatala.

Msemaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, David Mngongolwa amesema Gwajima alikwenda jana kuripoti kama alivyoamriwa kufanya hivyo.

Mngongolwa amesema baada ya kuripoti askari walimchukua na kwenda naye nyumbani kwake wakakaa kwa dakika zisizozidi sita na kuondoka naye.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda amesema hana taarifa za kukamatwa kwa Gwajima kwa maelezo kuwa alikuwa katika kikao.

“Naomba uumtafute Sirro (Simoni-Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam. Gwajima awali alishikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam hivyo ni vema ukamtafuta kamishna,” amesema Kamanda Kaganda.

Source : mwananchi
 
Halafu Magufuli aache kulitaja hovyo jina la Mungu, "Msema kweli ni mpenzi wa MUNGU "Magufuli ana ukweli gani?
roho yake imejaa chuki na hila dhidi ya wapinzani, Yasije kumtokea ya mfalme Belshazzar aliyekuwa kalewa madaraka hadi anamkufuru Mungu.
 
Tanzania Tanzania Tanzania. Nchi iliyokuwa imejaa amani, imekumbwa na jinamizi gani? Sasa hivi Tanzania si sehemu salama tena, tunashindwa kuzungumza hisia za mioyo yetu kwa kuogopa kudhulumiwa uhuru wetu. Wananchi tunahitaji maji safi, elimu bora na huduma za afya bora. Badala serikali ihangaike na kuboresha miundo mbinu hii, inahangaika na mtu mmoja mmoja kama kina gwajima, Lema na wengineo. Je tutafika?
 
Si alisema mwenyewe amealika wazee toka kolomije? We unadhani wakifunguka atakuwa salama? Lzm ibada ya kesho isitishwe kwa wahusika wakuu kutohudhuria.

Hafu kwa wasio faham, neno kolomije, lilipatikana wakati mzungu anajitambulisha akasema call me J, ndo likawa jina la kijiji hadi leo
 
Waacheni Polisi wafanye Kazi waliyotumwa ila wasisahau Na mwenye vyeti feki ni vema haki itendeke Kwa watanzania wote
Sarakasi nyingi mara kamata weka ndani!!
Fainaly Daud Bashite alete vyeti original vya Form Four.
Vinginevyo ni sanaa mnalinda wenye vyeti fake!!
 
Nchi hii kwa sasa inafanana na ile nchi iliyowahi ya kifasihi iliyoongozwa na Mfalme juha kwa kutumia unga wa ndele,hivyo tunawahitaji akina Mtolewa wafanye kazi ya ziada kupandikiza unga wa rutuba kwa wananchi ili kuleta ukombozi wa fikra
 
Jamhur wana complicate maisha. Kama vip gwajima alete ushahid.. na makonda alete ushahid. Kama kuna ambaye atakuwa amedanganya basi huyo ndio ashtakiwe...
 
Waacheni Polisi wafanye Kazi waliyotumwa ila wasisahau Na mwenye vyeti feki ni vema haki itendeke Kwa watanzania wote

Polisi kibao wana vyeti feki... Hivyo hili suala la Gwajima na DAB hata bila maelekezo toka juu watapambana lisivuke mipaka..
 
Kiongozi sampuli ya Gwajima atawatesa mno. Ukicheza na koki mbovu lazima ulowe tu. Gwajima anajua kuwa ni msafi na uovu wao anaujua wote mwisho wakichoka wataenda kupata kitubio kwake. Huwezi kusimamia haki ukiwa na mikono michafu. Kwa Gwajima ujue akitoka atamlipua mwingine tena.
 
Back
Top Bottom