Kamanda wa polisi Dodoma: Hatuna mpango wa kumkamata Zitto, hajafanya kosa la jinai, anajishtukia tu

Kansigo

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
2,670
2,156

Ruttashobolwa said
Moja ya tarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii jioni ya leo February 7 2017 ni kuhusu Polisi Dodoma kumtafuta kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe ili wamkamate.

AyoTV na millardayo.com imempata Kamanda wa Polisi Dodoma Lazaro Mambosasa na amesema yafuatayo >>> “Hiyo taarifa yeye mwenyewe ndio anajitangazaia akamatwe lakini sisi hatumkamati kwasababu hatuna ishu nae”

“Unajua watu wanafikia mahali wanatafuta umaarufu wakamatwe ili wapige mayowe… hatuna mpango wowote wa kumkamata kwasababu hajatenda kosa la jinai” – Kamanda Mambosasa
 
Hawa watu wanatia kinyaa sana mpaka inafikia hatua tunaukufuru uumbaji wa ngozi nyeusi!!

Huyo kamanda awali anambeza Zitto kuwa anataka kutafuta umaarufu kwa kupiga mayowe then mwishoni anakiri hawana uthibitisho kama kweli Zitto katoa hizo taarifa!!

Sio siri kwa mwendo huu wa awamu hii najisikia aibu kuu na mwenye laana kuzaliwa mweusi!!
 
"uchochezi" wa Zitto na wa ule wa Tundu Lissu upi zaidi? Nashindwa kuwaelewa polisi.
 
Kumbe kuna wakati wengine kabla ya kumkamata mtu wanaomba ruhusa kutoka kwa mtu kabla ya kumkamata mhusika. Au je ana maanisha kuomba ruhusa kutoka kwenye chombo husika mfano Bunge? Je, suala la Lissu waliliomba Bunge au mtu yeyote?

Mbona anasisitiza sana bila kuomba ruksa kwa mtu yoyote wakati huo huo anasisitiza wanazingatia sheria na wanakamata yeyote. Je, kuna wakati wanaomba ruksa kutoka kwa mtu au watu?
 
Tundu lisu wamemkata kwa kosa gani ???? Sisi sote tunatambua kazi ya polis ni kulinda raia na mali zake na siku zote anapokuja kukukamata lazima akuambie kosa lako then akwambie na kituo unachotakiwa kupelekwa baada ya hapo ndipo utaenda kituoni kwa mujibu wa sheria ...sasa inakuwaje mtu kama Tundu Lisu anakamatwa na polisi katika mamlaka iliyo chini ya mhimili wa serikali ambao upo tofauti na hakuna taarifa iliyotolewa bungeni kabla ya kukamatwa kwake?
 
"Sisi hatutaki na hatutamkamata..."

Ahahahah kweli maigizo hayataisha nchi hii, Zitto si mwendawazim kama kamanda anavyofikiria!
Anajua anachokifanya, pia kamanda aelewe tu kwamba kukamata wapinzani sio kiki ingekua ni umaarufu kwa jinsi navyoyajua maCCM yote yangejitangazwa kukamatwa!
 
Hawa watu wanatia kinyaa sana mpaka inafikia hatua tunaukufuru uumbaji wa ngozi nyeusi!!

Huyo kamanda awali anambeza Zitto kuwa anataka kutafuta umaarufu kwa kupiga mayowe then mwishoni anakiri hawana uthibitisho kama kweli Zitto katoa hizo taarifa!!

Sio siri kwa mwendo huu wa awamu hii najisikia aibu kuu na mwenye laana kuzaliwa mweusi!!

Wengi wao ni wale waliofali na kutumia vyeti vya watu. Uwezo wao wa kifikiri uko chini sana.
 
Kwa maelezo ya kamanda mwishoni hata mtoto wa chekechea ataelewa wanataka kumkamata. Kesho atasema yeye kama kamanda wa Dodoma hana issue naye isipokuwa ni kamanda wa Shinyanga.
 
Hii kamata kamata ya wapinzani kunawaongezea umaarufu sana.
Kila siku wanatangazwa na vyombo vya habari,mitandao ya kijamii, Polisi wanawasaidia sana kuwatangaza upinzani viongozi wa CCM hawasikiki wanasikika wa upinzani, Polisi imekuwa Kama idara ya uenezi ya vyama vya upinzani.
Wangejishughulisha na mambo makubwa kama mapapa wa madawa ya kulevya,majangili,majambazi waache hivi vitu vidogo vidogo kama kutangaza njaa.
 
Cammandar jasema hajatenda kosa lq jinai jinai c kosa kubwa...pengine ametenda kosa lakin c la jinai
 
Hawa watu wanatia kinyaa sana mpaka inafikia hatua tunaukufuru uumbaji wa ngozi nyeusi!!

Huyo kamanda awali anambeza Zitto kuwa anataka kutafuta umaarufu kwa kupiga mayowe then mwishoni anakiri hawana uthibitisho kama kweli Zitto katoa hizo taarifa!!

Sio siri kwa mwendo huu wa awamu hii najisikia aibu kuu na mwenye laana kuzaliwa mweusi!!
Hakuna adhabu kubwa duniani kama kuzaliwa mweusi ni shida na matatizo tupu mkuu.
 
Zitto itakuwa alipotea kama ilivyotokea Kahama, mwisho wa siku kama uwanja wa ndege na kuelekea Uingereza bila kuonwa na mtu.
 
Back
Top Bottom