Kamanda wa Polisi Arusha kanisikitisha

Anatamba saana,kuna siku pia walikuta silaha kwa mwalim mmoja huko manyara,alitamba utazan kamkamata osama
Yaani huyu kamanda utadhani ana undugu na Manara wa Simba. Anatukama mamba woote wakati hajakanyaga maji. Manara jifunze kuongea kwa kutumia kichwa.
 
Komando kipensi alikalisha kikosi kizima cha jeshi, au Rambo Bloodsport 1 porini alisumbua zaidi ya mwezi kuanzia jeshi hadi polisi. Japo ni sanaa ila huwa zinauhalisia.

Yule mzee hajasema kama kile kikosi chote kimetoka kupambana na adui hao usimsingizie mkuu.
Labda ila mzee anajua kutamba bana
 
toka yale ya jamaa wa madini wa sinza mi siwaamini tena hawa jamaa. uchunguzi ufanyike sio watu wanatamba kwenye matv kumbe hamna cha jambazi ni sanaa.
 
yuko wa kilimanjaro ana tambo huyu wa chuga aende shule akasome,nkikumbuka cku anatoa tambo kuhusu jamaa mmoja wa KB kukamatwa,utafikir n USA anatoa taarifa za kukamatwa kwa kiongoz wa IS
 
Mkuu risasi zinaua. Jambazi mmoja aliyejitoa mhanga ana nguvu zaidi ya polisi 100 ambao wameaga familia zao kwenda kazini na wakitegemewa kurudi kwenye familia zao wakiwa wazima. Wanastahili pongezi kubwa, hata jambazi akiwa mmoja.

Katika taarifa ya habari ITV ya sa2 ,nmekutana na habari kwamba kikosi cha polisi kimepambana na majambazi piga nikupige kwa dakika 70 yani lisaa limona na dakika 10.kazi nzuri

Kilichonisikitisha ni kamanda kuongea kwa mbwembwe na kujitapa sana kuwa ile piga nikupige,nikupige piga kwa dakika 70.

Cha ajabu jambazi mwenyewe ni mmoja na amekamatwa na silaha moja na risasi 26 tu.yani muda wote huo kumbe kamtu kalikua kamoja tu halafu kamanda anatamba
 
Ilikuwaje mkuu kwa hao wafanya biashara??? Uzi wake upo huku unisaidie link nikausome???
!
!
Utakuwepo. Jamaa Walikuwa Wafanyabiashara Wa Madini Walikuwa Na Hela Na Madini. Jamaa Wakawakamata Mitaa Sinza Wakawapeleka Chaka Wakawakili Wakachukua Madini Na Pesa Zao
 
Back
Top Bottom