Kamanda wa Israel: Kwa sasa hatuna uwezo wa kuingia kwa vita nyengine

pWazayuni wakiri: Jeshi la Israel halina ubavu wa kuingia katika vita vipya
Afisa mmoja mwandamizi wa jeshi la utawala wa Kizayuni amekiri kuwa Israel haina uwezo wa kuingia kwenye vita vyengine vipya.
Katika mahojiano na gazeti la Maariv, Brigedia Jenerali Moshe Tamir, kamanda wa zamani wa jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza amekiri kuwa, jeshi la Israel haliwezi katu kuingia kwenye vita vyengine na kufafanua kwa kusema: Utendaji dhaifu wa jeshi kuhusiana na njia za chini kwa chini katika mipaka ya kaskazini umesababisha kudhoofika Israel.
Tamir ameashiria kushindwa kwa vikosi vya nchi kavu vya jeshi la Israel katika vita vya karibuni dhidi ya Ukanda wa Gaza na kutoa indhari kuhusu athari za kuendelea kuchimbwa njia za chini kwa chini na wana muqawama wa Palestina wanazotumia kwa malengo yao ya mbinu za kivita.
Afisa huyo mwandamizi wa utawala wa Kizayuni wa Israel vilevile amewaomba wale wanaokosoa ripoti iliyotolewa na Meja Jenerali Yitzhak Brick, walitafakari vizuri wazo la kuanzisha vita vipya kwa kuzingatia hali ngumu inayolikabili jeshi la utawala huo haramu na akamtaka kamanda mpya wa jeshi la utawala wa Kizayuni Aviv Kochavi afikirie namna ya kutatua tatizo hilo.
Siku ya Alkhamisi, Yitzhak Brick alikiri kuwa: Jeshi la Israel halina utayari wa kuingia vitani katika mazingira ya hali ya hatari.
Kauli hiyo ya ungamo la Meja Jenerali Brick iliibua hasira na lawama za msemaji wa jeshi la Israel Ronen Manelis, ambaye kwa mtazamo wake amesema, haikupasa Brick kulitangaza jambo hilo hadharani mbele ya vyombo vya habari.../
Tags
ISRAEL JESHI VITA
Upo kishabiki sana kulko uhalisia hadi unaboa
 
Jamaa kwa fix ni hatari....Israel anavyochukiwa na waarabu hiyo ishu unayowaza ingekuwa kweli dk 0 Israel angeshapigwa vibaya sana hicho Chuma wataishia kukiona na kukichukia tu...kwa taarifa tu ndo inchi inayopakana na maadui zake pande zote
 
SIKU IZI SHAMBULIO 1 TUNAJIBU MAKOMBORA 450, UPANDE B TUMEFUNGA ANGA S-300 NA TUNAJIBU CHANZO, UKIJA HIZBU HATUTANIWI KABISA MZIKI WETU TUNAJIBU KULIKO 2006 , mzee wa mivita labda aje ashambulie Dar
Israelii wanahali mbaya kwa sasa

Syria..
.wamewekeea s300.5 wakala kona
Wakajaribu kwa Hamas huku
Palestine...wamepoteza makomando na waziri wao wa ulinzi kajiuzuru na wakala nmaroketi kama 400+
Wakaja huku Lebanon
Lebanon ....wamekuta mahandaki kibao yamechimbwa yanasubir vita ianze HEZBOLLAH wazamie telaaviv fasta.
Hawa jamaa lazima akili iwakae sawa safar hii
 
Jamaa kwa fix ni hatari....Israel anavyochukiwa na waarabu hiyo ishu unayowaza ingekuwa kweli dk 0 Israel angeshapigwa vibaya sana hicho Chuma wataishia kukiona na kukichukia tu...kwa taarifa tu ndo inchi inayopakana na maadui zake pande zote

Hakuna kisichokuwa na mwisho bwana, kwani wamekuwa Mungu wao!!! itakuja tu kufikia nao watapotezwa...
 
WAHUNI WA KIHAMAS HAWATAKI UJINGA SIKU IZI.
Screenshot_20181217-131313.jpeg
 
Back
Top Bottom