Kamanda wa IRGC: Uingereza na Marekani zitajuta kwa kuizuilia meli ya mafuta ya Iran

kimsboy

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Messages
4,440
Points
2,000
kimsboy

kimsboy

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2016
4,440 2,000
Kamanda wa IRGC: Uingereza na Marekani zitajuta kwa kuizuilia meli ya mafuta ya Iran
Jul 12, 2019 02:26 UTC
Naibu Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) ameonya kuwa, Uingereza na Marekani zitajuta kutokana na hatua ya London ya kusimamisha na kuzuilia meli ya mafuta ya Iran katika Lango Bahari la Jabal Tariq (Gibraltar).
Admeri Ali Fadavi alisema hayo jana Alkhamisi katika mkoa wa Isfahan, katikati ya Iran na kuongeza kuwa, "Kitendo chao (Uingereza na Marekani) cha kuzuia meli ya mafuta ya Iran ni cha kipuuzi na karibuni hivi watajuta na kuomba msamaha."
Ameeleza bayana kuwa, hatua ya kuzuia meli ya mafuta ya Iran ni ukiukaji wa kanuni na sheria za kimataifa na kamwe kitendo hicho hakitapita hivi hivi bila kupewa jibu mwafaka.
Naibu Kamanda wa SEPAH amesisitiza kuwa, maadui hawana ujasiri na uthubutu wa kufyatua japo risasi moja dhidi ya Iran na wenyewe wamekiri mara kadhaa kuwa njama zao dhidi ya taifa hili zimegonga mwamba.
Katika kuhalalisha hatua yake hiyo ya Alkhamisi ya wiki iliyopita, Uingereza ilidai kwamba inaiuzuilia meli hiyo ya mafuta ya Iran kwa kuwa imekiuka vikwazo vya Marekani na vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Syria vilivyowekwa mwaka 2011. London ilidai kuwa meli hiyo ya mafuta ilikuwa inaelekea Syria.
Hata hivyo, Brigedia Jenerali Amir Hatami, Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hivi karibuni aliashiria hatua hiyo ya askari wa Jeshi la Wanamaji la Uingereza ya kuisimamisha meli ya mafuta ya Iran katika Lango Bahari la Jabal al Tariq (Gibraltar) na kueleza bayana kuwa, Tehran kamwe haitafumbia macho uharamia huo wa London.
Tags
IRAN MAREKANI UINGEREZA
 
Ugiligili

Ugiligili

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2014
Messages
2,578
Points
2,000
Ugiligili

Ugiligili

JF-Expert Member
Joined Jun 20, 2014
2,578 2,000
Vita vya maneno..sawa.
 
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Messages
3,158
Points
2,000
M

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined May 24, 2018
3,158 2,000
Waingereza na Wamarekani wana Maslahi makubwa mno Iraki
Irani ina influence kwa mashia wenzake huko Iraki akina Muktada Sadri, ina uwezo wa kuwaamrisha wazifanye investments za Wamarekani na Waingereza kitu mbaya then vita nzima ya kuiba mafuta ya Iraki ya mwaka 2003 itakuwa haina maana, ndiyo maana Mmarekani na Muingereza kila wakipiga mahesabu wanaona Irani haingiliki kirahisi!
 

Forum statistics

Threads 1,315,675
Members 505,292
Posts 31,866,470
Top