Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Profesa Lipumba, Abdul Kambaya
Dar es Salaam. Watu saba wamekamatwa kwa kusababisha vurugu katika mkutano wa CUF uliofanyika Mabibo hivi karibuni, akiwamo mfuasi wa Profesa Ibrahim Lipumba, Abdul Kambaya.
Kambaya ni Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Lipumba.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema upelelezi wao umekamilika na jalada la mashtaka hayo lipo kwa wakili wa serikali.
Sirro ameyasema hayo leo Ijumaa katika mkutano na waandishi wa habari.
Chanzo: Mwananchi