Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,633
- 29,506
Wakuu,
Hapo awali RC wa Dar es Salaa bwana Makonda akiwa na RPC wake Kamanda Sirro walitoa orodha ya Watu wanaodhaniwa au kutuhumiwa uuzwaji wa dawa za kulevya wakiwemo baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi pamoja na wasanii mbalimbali wa maigizo na waimbaji maarufu hapa nchini. list hii ni ile iliyowahusisha Wema Sepetu, Petiman, TID, Mr. Blue, Recho(kizunguzungu) etc
Tena RC Makonda akaja na orodha ya pili yenye ajina 65 iliyowahusisha Askari watatu Mudy Zungu, Fadhili na Beny. Pia Video Queen Tunda pamoja mwanamuziki maarufu hapa nchini Vanessa Mdee nao walikuwepo kwenye hivyo list. Wengine ni Wanasiasa Philemon Mbowe, Iddy Azan etc. Pia walikuwepo Omary Sanga, Kashozi, Amani na wengineo wengi tu ambao wote hawa walikua kwenye list ya pili.
Mwishowe ikaja list ya tatu ambayo hii majina yake yapatayo 97 yalikabidhiwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Bwa. Rogers Sianga. List hii tulipata tu kusikia majina kama Chiddy Mapenzi na yule mwengine
Ukichukua majina ya mwanzo, ukajumlisha majina ya pili 65 na list ya tatu majina 97 ni wazi jumla yake itafika au hata kuzidi majina 200. Katika majina haya wapo ambao wamefikishwa mahakamani wakapewa dhamana, wapo abao bado wanahojiwa makao makuu ya polisi (Central) na wapo ambao inasadikiwa hawajariport bado.
Sasa hapo Juzi RPC huyu wa dar es salaam alisikika akimtaka Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mheshimiwa Freeman Aikael Mbowe ambaye alitajwa kwenye majina 65 ya watu wanaojihusisha na Mihadarati kuripoti yeye mwenyewe Polisi kabla hatua za kijeshi hazijachukuliwa.
Je Kamanda Sirro anaweza kutusaidia wengine ambao nao kama Mbowe walikua hawajaripoti ni kina nani?? Kwa idadi na majina yao ili tuwajue nao??
Je nao walipangwa kuchukuliwa hatua kwa kutafutwa na Polisi kama ilivyo kwa Mh. Mbowe??
Je nao walipangwa kutangazwa kama ilivyo kwa Mh. Mbowe alivyotangazwa??
Je ni rahisi kumtafuta mtu ambae anafahamika na watu wengi kama Mh. Mbowe au hao wengine ambao wanafahaika labda vijiweni kwao tu??