Kamanda Sirro tuhakikishie Usalama wa Raia wema wakati wa mapokezi ya Tundu Lissu

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
wana JF,

Mikakati ya kumpokea Tundu Lissu imeiva akiwa anarejea kutoka ughaibuni, kwa vile Lissu ni kipenzi cha wengi, hakuna haja ya kuvalia uniform kuonyesha kuwa wewe ni wa chama fulani, bali tunavaa kawaida sana nguo za nyumbani.

Kwa vile wenye mapenzi naye ni mchanganyiko wa vyama vyote Serikali iweke ulinzi apokelewe salamu tusije kutumia nguvu pasipostahili tukakuta tunawaumiza wapiga kura wetu au kuumiza wasio husika kama ndege atakayopanda inawezekana ikawa na watalii wa nchi mbalimbali, wasafiri wa aina nyingi, wafanyabiashara na wawekezaji.

Kamanda Sirro haya mapokezi usiyachukulie ya kisiasa, ni kwa mapenzi tu ya mtu kwani ikiingiza siasa, hata huko CHADEMA kuna maadui na mahasimu wake, hata CCM kuna maadui na mahasimu wake lakini pia kuna marafiki wake nje ya game, ndio maana kwenye familia yake , kuna ambao ni CCM kindakindaki lakini linapokuja suala la udugu vyama tunaweka pembeni.

Wengine wanakuja kumsagaa Lissu ni mzimu unaotembea au vipi, haiwezekani mtu akapigwa risasi 18 alafu akapona kirahisi hivi.

Kingine kwa kuwa mgombea huyu anaweza kupitishwa na chama kwa sasa angeachwa atulie aje kwa amani ili asiongezewe stress ili ajumuike na wenzie katika ushindani.
 
mtapigwa mchakae tunamsiba mnataka kuleta utani huo ni utani huyo bwege aje kimya kimya tu aende nyumbani kama atafanikiwa maana mahakamani nako anahitajika soon akishuka
 
mtapigwa mchakae tunamsiba mnataka kuleta utani huo ni utani huyo bwege aje kimya kimya tu aende nyumbani kama atafanikiwa maana mahakamani nako anahitajika soon akishuka
achaka mtu sisi wapenda amani tutabeba maji tuuuu
 
Mapokezi ya Raisi Mtarajiwa Tundu Antipas Lissu haitaji mwongozo wa Polisi. Chadema na wananchi tumejipanga vizuri, tutampokea kwa amani bila shida yeyote kama alivyopokelewa Hussein Mwinyi Unguja na Pemba majuzi hapa.
 
mtapigwa mchakae tunamsiba mnataka kuleta utani huo ni utani huyo bwege aje kimya kimya tu aende nyumbani kama atafanikiwa maana mahakamani nako anahitajika soon akishuka
Nenda utubu ndugu yangu maana moyo wako umejaa kila aina ya uchafu .Yesu anakushauri ungali una nguvu na pumzi

20 Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.
Marko 7:20

21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,
Marko 7:21

22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.
Marko 7:22

Screenshot_2015-09-15-10-11-57.jpg
 
n
Mapokezi ya Raisi Mtarajiwa Tundu Antipas Lissu haitaji mwongozo wa Polisi. Chadema na wananchi tumejipanga vizuri, tutampokea kwa amani bila shida yeyote kama alivyopokelewa Hussein Mwinyi Unguja na Pemba majuzi hapa.
i kweli lakini hawa polccm wanaweza kuanzisha yao
 
Bavicha mnavyojidanganya hapa utafikiri mnakwenda kweli kumpokea hahahahaha
 
n

i kweli lakini hawa polccm wanaweza kuanzisha yao

Huyo IGP haangalii weledi, bali anatii chochote anachoagizwa na anayemlipa mshahara. Usitegemee asikilize ushauri wako. IGP yeye na jeshi lake watafanya watakavyoagizwa na viongozi wa ccm.
 
Back
Top Bottom