Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,858
Tangu asubuhi ya leo kumekuwa kukiripotiwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro ameagiza kuwa pikipiki ziishie saa tano usiku. Ndiyo kusema kuwa usafiri wa pikipiki utasita muda huo
Tunakubaliana kuwa ulinzi na usalama ni lengo kuu la kinchi huku Jeshi la Polisi wakilisimamia vyema lengo hilo. Tunakubaliana pia kuwa Jeshi la Polisi linafanya kazi ya kutukuka katika kulinda watu na mali zao. Ipo wazi kuwa Kamanda Sirro ametoa agizo lake kwakuwa ana sababu zake
Kwa kuzingatia mazingira ya jiji la Dar,pikipiki hazipaswi kupigwa marufuku kuanzia saa tano usiku. Yapo mabasi ya mikoani yanayowasili Dar hadi saa sita usiku. Pikipiki huwa msaada. Wapo wananchi wanaorejea makwao hadi kuanzia saa sita usiku. Pikipiki huwasaidia sana wananchi hao.
Tafadhali Kamanda Sirro,tafakari upya katazo lako. Kinachopaswa kufanyika ni kuimarisha ulinzi na utaratibu mzuri katika nia ya kuzuia pikipiki kutumika katika uhalifu.