Kamanda Sirro: Sungusungu marufuku kukaa vituo vya Polisi wala kukamata Bodaboda

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Heshima kwenu wakuu,
boda4.jpg

Kamanda Sirro wa Kanda maalum ya Dar e Salaam yupo kwenye Ziara Kinondoni. Kwa sasa yupo hapa Kijitonyama kwa Ali Maua.

Anasema watu wa Mkoani waje wafanye kazi halali na watakaa kwa Amani. Lakini wakija na bunduki kuiba na kufanya uhalifu hawatarudi salama. Tutawagonga kwa mjibu wa Sheria.

Siku hizi watu wanaosumbua ni Bodaboda. Biashara gani ambayo hulali? wewe ni mwanga?. Nimewambia Vijana wangu wakimuona bodaboda wamkamate wamlete kituoni halafu asubuhi wamuachie aendelee na kazi. Siku hizi mtu akiibiwa utasikia bodaboda. Bodaboda mwisho saa sita.

Mlisikia mambo yametokea Kibiti? Kama unamua Askari, viongozi halafu unamwambia mwananchi njooni mchukue mkaa na wananchi wanaenda kuchukua mkaa kwa wale wauaji, hii ni mbaya sana. Haya mambo ndo nayasikia hapa Tanzania.
boda1.jpg

Kuna watu Makanisani na Misikitini baada ya kuhubiri Yesu na Quruan, wanafundisha kung fu. Wengine wanawatoa watoto shuleni wanaenda kuwafundisha kupiga bunduki.

Kuna watu wachache wanadhani wapo juu ya Sheria. Tutakugonga tutakurudisha kwenye mstari. Mahali pa ibada pawe pa ibada.

Sisi ni watumishi wa uma tufuate sheria za utendaji kazi. Tuwaheshimu waliotuajiri, Sisi ni Polisi Ofisa sababu sheria ndo imesema. Usipokwenda sawasawa na jeshi la Polisi tutakufukuza na utaenda Uraiani.

Ukiona kuna ofisa hakutendei haki, usivumilie, tupigieni simu. Hakuna Askari aliye juu ya Sheria.

Lakini wale wasiopenda kushiriki kwenye ulinzi shirikishi. Jirudi. Jambazi akija haulizi wewe chamaa gani, rangi gani wala dini gani. akija ni kukutoa roho. Wasiochangia ulinzi shirikishi ndo wa kwanza kupiga simu wakivamiwa. Kuna sheria ndogo ndogo. Wapelekeni mahakamani washitakiwe wale wote wasioshiriki ulinzi shirikishi.

Kwa wale wanaotaka kuonana na Mimi njoo pale central nipo friendly kabisa tutapiga stori na hata kama huna nauli ntakupa

Maswali;

Seleman Saidi ansema;

Unapokuja kwenye maeneo yetu tunaomba uwahi. Swala la ulinzi shirikishi ni ni gumu sana. Unawapa siri askari unalikuta kwa jirani.

Bodaboda ni ajira, simama tena na wanahabari ulifafanue vizuri.

Tuache siasa katika maswala ya Ulinzi. Hapa ali maua tunashida ya kituo kingine.

Ulinzi shirikishi tunazijua. Unatuletea sungusungu, je jeshi lako halina watu? Sungusungu unawakuta kwenye defender. Hawa sungusungu wanafanya kazi gani?

Majibu:
Afande Sirro anasema: Mwaswala ya Ulinzi shirikishi sio hiali ni lazima sababu sheria imeshatungwa kuhusu ulinzi shirikishi.

Ni kweli wapo askari hawana siri. mtafute mtu ambaye unamwamini njoo kwangu kama vipi ila na wewe uwe na siri. sio unasema siri wakati umemwambia mkeo au mumeo.

Wewe unayefanya bodaboda hadi saa kumi mwanao unamuona saa ngapi? Wezi wengi wa usiku wanatumia bodaboda hata wao wenyewe bodaboda wanatafutwa.

Kituo cha ali Mau sijui. Tulisema kila kata kuwe na kituo kimoja. Wingi wetu ndo ubora wetu. Bora vituo vichache askari wengi kuliko vituo vingi askari mmoja hatakusaidia chochote.

Sungusungu hawatakiwi kukaa kwenye vituo vya Polisi.

Tambaza ndo wanafanya kazi ya ukamataji wa Pikipiki. Hawa sungusungu wanaokamata Pikipiki hawaruhusiwi.

Sungusungu mumekatazwa kukaa kwenye vituo vya Polisi, tafuteni kazi nyingine. Sasa tutaanza kukamatana, ngoja nianze kuzunguka.

Askari wanaofanya vizuri tutawapa zawadi.

Dereva bodaboda anauliza:

Usiku bajaj na bodaboda tunaitwa kubeba wagonjwa, ni utaratibu gani tutumie ili tutambulike tusisumbuliwe?
 
Kweni kunatofauti gani Kati ya sungusungu na police hawa wa sasa waonezi hawana ueledi ni makatili hawana huruma hakuna watu wanaochukiwa kama mapolice
 
Sungusungu wapo hapa ubungo darajani kituo cha mabasi karibu na songas wanakula hela za bajaji tu kila ikipakia inaacha elfu moja na wanashirikiana na polisi na wenyeviti wa mtaa na wanapewa hadi pingu za kukamata bodaboda na wahalifu wengine je polisi hawawezi kazi nao wanaajiri watu kama wanaupenda upolisi si wangeenda mafunzoni kwanza wanakera sana siyo kidogo
 
Hilo swali la mwisho la bodaboda natamani nijue lilijibiwa vipi maana bodaboda kaweka swali kisomi aise kumbe na bodaboda ni noma
 
Back
Top Bottom