Kamanda Sirro: Nimeona watu kwenye mitandao wakisema kwamba Polisi wamekuwa kama TRA

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,658
15,784
Jana amesikika kamanda wa kanda maalum DSM akijibu mapigo baada ya taasisi anayoisimamia kushutumiwa kujigeuza na kuwa tawi la TRA.

Amesikika kwa hoja dhaifu akijibu tuhuma hizo lakini picha ya mapato aliyokusanya kwa kipindi cha kama wiki moja kinaonesha kuwa mapato ya Polisi-TRA yameshuka kwa kasi kubwa kutoka kwenye milioni mia nane na ushee mpaka milioni mia sita na ushee!

Nawashukuru JF ana kuwapongeza wale wote walioshiriki kupinga vikali dhuluma zinazofanywa na polisi wa usalama wa barabarani za kushurutisha madereva walipe faini hata kwa vikosa vidogo vidogo.
TRA Ruangwa na Polisi Wanalazimisha Kukusanya Mapato kwa Kamata Kamata

Dhana ya polisi kuwa wakusanya mapato

======

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro April 5, 2017 ameeleza sababu za Jeshi hilo kufananishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ katika utendaji wao wa kazi hasa katika ukusanyaji wa mapato.

Kamanda Sirro ametoa ufafanuzi huo mbele ya Waandishi wa Habari akisema kumeibuka maneno sehemu mbalimbali hasa mitandaoni wananchi wakidai kuwa Jeshi hilo limeacha kazi yake ya kulinda raia na mali zao na kufanya kazi ya kukusanya mapato ambayo hufanywa na TRA.

“Nimeona watu wengine wanazungumza kwenye mitandao kwamba Polisi wamekuwa kama TRA. Mimi niliweke vizuri, sheria zipo. ukiangalia katika sheria ya Usalama barabarani iko vizuri. Na kama umekamatwa na kosa ambalo tunaamini umekiuka makosa ya Usalama barabarani hatukulazimishi wewe kulipa ile faini. Kuna mawili; kama hauko tayari kulipa ile faini, utaratibu upo tunakupeleka Mahakamani.” – Kamanda Sirro.
 
Hizi nazo ni tuhuma za kujibu?

Sasa ndio uone wabongo walivyokuwa ni watu wa ovyo. Tuhuma nyepesi kama hizi ambazo kimsingi ni kejeri wala sio tuhuma, tayari wameshajibu.

Alafu tuhuma nzito za mtumishi wa ngazi ya juu kabisa za kufoji vyeti, wanaita ni tuhuma za kipuuzi na hazistahili kujibiwa kivyovyote.
 
Police pigeni kz, haijalishi vikosa vidogo vidogo wala makubwa. Piga fine!!
Is either hujawahi kuendesha gari au huna mpango wa kununua gari but once you have it then you will see it. Hata kama wewe ni mkubwa au mtoto wa mkubwa, remember PANGA haliijui SHINGO ya ALIYELITENGENEZA; uliwahi kufikiria kwamba in 2 years time Nape angeweza kutishiwa bastola!?
 
Tufuate sheria tu ndiyo la maana,na magari yetu mengi mabovu tunanunua used,wanaonunua zero km ni Serikali na baadhi ya NGO na Taasisi.

Na issue ya kufuata sheria ya usalama barabarani kwa madreva wa Tanzania ni zero kabisa wengi utasikia wanawahi tu sijui huwa wanawahi wapi.kafoleni kidogo tu basi service road zote zimejaa!!

Zebra cross hakuna anayeziheshimu,kufunga mkanda ni kama adhabu kwa dreva.Leseni kila mmoja amesahau nyumbani.Road license boss anashughulikia basi makosa kila kona.

Wind screen cracks,taa za break haziwaki.

Tukipigwa faini tunalalamika.Traffic wafanyaje hapo??
 
Back
Top Bottom