Kamanda Sirro: Kama kuna kiongozi alitaja siku watakayopatikana akina Roma, mulizeni yeye

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,179
2,940
Habari wakuu,

Leo kamanda wa polisi mkoa wa Dar es Salaam, Simon Sirro pamoja na mambo mengine ikiwemo watu kukaa kwenye maeneo salama na ulinzi shirikishi, mauzo ya CD's kwenye nyumba za ibada ambazo kwa madai yake zinahamasisha mambo ya vita, ugaidi na vurugu. Sirro amesema watafanya operesheni na kuwataka wanaouza wakazichome ikiwemo za Al-Shabab na watamtaka awapeleke Al-Shabab alipozipata.

Kuhusu Ibrahim Mussa Almaarufu Roma Mkatoliki amesema walipata taarifa Noah yenye rangi ya Silver ilienda maeneo ya Masaki kwenye studio za Tongwe Records ikiwa na watu watano na wameondoka na TV(Sony), Computer na Camera moja.

Amedai ndani ya studio pia kulikuwa na vijana watatu pamoja na Ibrahim wa nne na wenyewe wamechukuliwa, baada ya hio taarifa, Haifa Shabani alitoa taarifa polisi Oysterbay siku inayofuata. Amesema upepelezi haujakamilika na wameunda timu ya Cyber na upelelezi unaendelea vizuri.

Sirro amesema hawezi kusema wamefikia wapi na yeye huwa hapendi kutoa majibu ya haraka haraka, ishu iko polisi na amewataka watu waache polisi ifanye kazi kwani kuna watu wanakuwa zaidi ya polisi kwa kutaka kuwazungumzia polisi na kujifanya Kamishna Sirro kwa kuzungumzia habari ya upelelezi.

Sirro amesema kama kila tukio la uhalifu likitokea watu wanakutana na kushinikiza hajui itakuwaje hivyo anataka wapewe muda.

Swali: Tukio la aina gani, kigaidi au la aina gani? Usalama wa mwananchi wa kawaida ukoje kwa haya mambo ya kutekwa?

JIBU: Suala la watu kutekwa halijaanza leo, ni tukio kama matukio mengine. Ni hali ya kawaida sana, watanzania tuko wangapi na tukio limetokea kwa hawa vijana. Huwezi ku-conclude hali ni mbaya kwa sababu tu hao vijana wametekwa.

SWALI: Moja ya kiongozi kwenye ngazi ya juu ya mkoa amesema mpaka Jumapili atakuwa tayari ameshapatikana. Pili watu wanafananisha tukio hili na la Ben Saanane ambalo pia jeshi la polisi lilisema linafanyia uchunguzi na bado uchunguzi wake watu hawajaambiwa ameenda wapi, Pengine lini tutapata taarifa kamili?

JIBU: Niseme kama kamishna ambae ni police officer na nipo kisheria, nachosema upelelezi ndio utakaonisaidia kujibu haya mnayoniuliza, Ni lini watapatikana? Siwezi kukujibu, Investigation siwezi kusema lini, mimi ni professional police officer. Kama kuna kiongozi kasema simsemei yeye, yeye ndie ungemuuliza, kama kuna kiongozi kasema, yeye ndio atakuw na hayo majibu.

 
Hiyo gari hivi hawakufanikiwa kunasa namba zake? maana wanasema hapo nyumbani palikuwa na watu wengine!
 
Bashita alisema mpaka kabla ya jumapili watakuwa wamemrejesha Roma na wenzake !
 
Sirro huwa namkubali lakini sijui kwa nini wakati mwingine huwa anapenda kujidhalilisha mwenyewe kiasi kile? Hapo kajibu kipolisi kabisaaaa, tena polisi mwenye elimu yake nzuri tu ila namhurumia sana anabishana na Daudi Albert Bashite? Watamtumbua muda si mrefu!
 
Roma amepatikana yuko kituo cha Polisi Oyster bay. Amepatikana kabla ya J2 kama alivyoahidi RC. Mi naona RC anafaa kwa upelelezi, Sirro tembea huwezi kazi
 
mtu anayeweza tengeneza video ya kumchafua mtu na ku force ionekane kwenye tv anaweza hata kutoa roho za watu
 
Wakati mgumu ni nini?
Wakati mgumu ni pale unapopata taarifa kwamba unaowategemea wamekugeuka.
 
Ni wazi sasa issue yote bashite alikuwa anaijuwa, haiwezekani aseme Roma atapatikana kabla ya j2, na iwe hivyo, huyu itakuwa alimficha kule kwa masogange maana hats kamanda sirro amezidiwa na mbinu za bashite, hivi kweli huyu alizungusha?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom