Kamanda Sirro atangaza oparesheni maalum kwa wenye vyeti vya kugushi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,490
54,884
13615388_1214900298542839_5012187694660680714_n.jpg


Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro amewataka wale wote waliyo na vyeti vya kugushi (vyeti feki) wajisalimishe mapema kwa jeshi hilo kabla ya kuanza kwa oparesheni maalum utakaowabaini na kuwachukulia hatua za kisheria.

Kamanda Sirro ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar na kuongeza kuwa, watuhumiwa wamekuwa wakibanwa na kuwataja baadhi ya vigogo wa seriaklini kuwa ndiyo wanaohusika kuwatengenezea vyeti hivyo na kwamba huvitumia vyeti hivyo walivyotengenezewa kwa kuajiriwa serikalini na taasisi nyingine.

===================

Watu watatu wanaosadikiwa kuwa vinara wa kutengeneza vyeti bandia pamoja na nyaraka mbalimbali za Serikali wamekamatwa eneo la Buguruni wakiwa na mitambo yao.

Kukamatwa kwao kulitokana na msako mkali uliofanywa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam hivi karibuni na hatimaye watuhumiwa walinaswa wakiwa nyumbani wanakoishi eneo la Buguruni Ghana wakitengeneza nyaraka bandia.

Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Ashraff Maumba (37) mkazi wa Buguruni Ghana, Mwamba Seif (38) mkazi wa Mnyamani, na Mahmudu Zuber (24) mkazi wa Buguruni.

Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba Julai 8, saa 4.00 usiku walifanya upekuzi katika nyumba wanayoishi na kukuta nyaraka mbalimbali vikiwamo vyeti bandia vya kidato cha nne 50 na vyeti vya vyuo vya uuguzi.

Kamanda huyo alisema nyaraka nyingine bandia zilizokamatwa ni stika 20 za Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), vyeti vya kuzaliwa 10 na vya Chuo cha Ufundi (Veta).

Nyaraka nyingine zilizokamatwa, kwa mujibu wa Sirro ni leseni za biashara, stika 100 za bima za magari, mitambo na vivuli 10 bandia vya vyeti vya Chuo cha Biashara (CBE).

Katika upekuzi huo pia walikamata mihuri mbalimbali ya ofisi za Serikali na binafsi ukiwemo muhuri wa Bibi na Bwana.

“Tulifanikiwa kukamata vifaa mbalimbali vya kutengenezea nyaraka zikiwamo karatasi maalumu zilizo na nembo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa ajili ya kutengeneza zaidi ya kadi 500 za vyombo vya moto, kompyuta nne na mashine moja ya kuchapisha,” alisema Sirro.

Kamanda Sirro alisema watuhumiwa wanashikiliwa na Jeshi la Polisi huku upelelezi ukiendelea na ukikamilika watafikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka yanayowakabili.

Katika hatua nyingine, Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Cassian Chibogoyo alisema Serikali haitakubali kuhujumiwa na watu wachache hivyo itachukua hatua kali kwa wote wanaojihusisha na utengenezaji vyeti bandia vya Serikali.


“Tunashukuru jeshi la polisi kuibua shina ambalo lilikuwa linatusumbua sana kutambua ni wapi wanatengeneza vyeti hivi vya bandia na tumepata taarifa za mawakala wanaofanya ujanja huo,” alisema Chibogoyo.
 
Nasubiri kuona hii Vita Ikianza maana ni kubwa kuliko Vita ya ufisadi maana kuna watu wanasema hapa kazi tu kwa sababu ya vyeti feki Mimi naona waandae kitengo maalum najua kuna vijana wengi watapata ajira kama watumishi hewa ni elfu kumi Na je wenye vyeti feki
 
Anasema "wakiwabana husema kuna wakubwa huwatengenezea hivyo vyeti"
Sasa pa kuanzia mbona ni hapo????

Polisi akiwa mjinga ni hatari, si mnaona alichokisababisha yule wa marekani.
 
Anasema "wakiwabana husema kuna wakubwa huwatengenezea hivyo vyeti"
Sasa pa kuanzia mbona ni hapo????

Polisi akiwa mjinga ni hatari, si mnaona alichokisababisha yule wa marekani.
Hapo intelijensia huwezi kuisikia!
 
Back
Top Bottom