Kamanda Sirro atangaza oparesheni maalum kwa wenye vyeti vya kugushi

Wale ma Dr. siku hizi hawatumii tena title ya Dr. Kumekucha. Tanzania kuchele!
 
Yule mkurugenzi wa nida aliyetumbuliwa aliwahi kutamka wakati wa mchakat wa vitambulisho vya uraia kuwa ndani ya jeshi la polisi kuna askari wengi wana vyeti vya kubumba. Sasa tusubir tuone
 
Sasa hao referees kwenye hizo CV sasaaaa!!!maana na wao ni wahusika wa kugushi,sijui itakuwaje
 
View attachment 365614

Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro amewataka wale wote waliyo na vyeti vya kugushi (vyeti feki) wajisalimishe mapema kwa jeshi hilo kabla ya kuanza kwa oparesheni maalum utakaowabaini na kuwachukulia hatua za kisheria.

Kamanda Sirro ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar na kuongeza kuwa, watuhumiwa wamekuwa wakibanwa na kuwataja baadhi ya vigogo wa seriaklini kuwa ndiyo wanaohusika kuwatengenezea vyeti hivyo na kwamba huvitumia vyeti hivyo walivyotengenezewa kwa kuajiriwa serikalini na taasisi nyingine.
Hilo zoezi ni gumu sana kwani ukiingia wizara ya elimu ndiyo utachoka kabisa maana wamejazana kibao
 
Na siyo polisi hata JW wapo wengi. Ila itabid kuwa makin vinginevy tutatengeneza jeshi la waasi
 
Kwa hili nampa hongera kila mtu ale kwa jasho lake.Hapa kazi tu hivi kwanini zoezi la vyeti feki liachelewa na kususua sua siliunganishwe na uhakiki wa wafanyakazi hewa.
Ange anza na ma wilayani hasa walimu na manesi huko ndiyo balaa kabisa
 
Anajishosha tu bure maana... jeshi la polisi magereza na wanajeshi ndo wanaongoza kwa Vyeti vya kugushi na mikopo wamechukua tena mikubwa tu
 
Jeshi la polisi lina ujuzi gani kutambua vyeti feki? Au watashirikiana na NECTA kuvibaini?.Itakuaje watu wamejiendeleza mpaka kupata Phd na ni watu waliobobea kwenye fani zao na michango yao ni mikubwa kwa Taifa?
 
Hivi hilo la kukagua vyeti ni moja ya jukumu la polisi?

Heee!!! Sekta ya polisi ambayo jukumu lake kuu na la msingi ni ulinzi na usalama wa Raia na Mali zao limebadilika na kuwa katika sekta au wizara ya elimu????
Tafadhali mnisaidie hili to me is very incredible as I see ni kama interaction of responsibilities,roles & accountabilities.

mamlaka, wizara au taasisi zinazosimamia elimu ndio zina majukumu ya kuhakiki vyeti...

polisi ni idara inayopelekewa taarifa za uhalifu na kuchunguza kabla ya kupeleka mahakamani.
 
Back
Top Bottom