Kamanda Simon Sirro ameidhalilisha taaluma yake mbele ya miguu ya Paul Makonda, ajitafakari!

Hao watu walioajiriwa tena wakiwa na vyeo vikubwa hivyo hawana ujanja wa kujiajiri labda wafukuzwe kazi. Hapo alipo hata apigwe vibao na huyo Rc kijana ataendelea kuvumilia kwani hapo ndio mahali anaweza kutoka kimaisha. Hizo porojo unazosikia wakiwa maofisini watu wajiajiri eti kuna fursa kibao ni danganya toto. Kama ingekuwa kujiajiri ni rahisi hivyo usingeona wakiwatafutia watoto na vimada wao kazi za ajira serekalini ama kwenye taasisi na makampuni yanayolipa vizuri
Excellently said
 
Na jana Kamanda Siro alitangaza kuwa Wema mi miongoni mwa watakuwepo mahakamani. Lakini ghafla baada ya shinikizo la makando Wema hakuoetwa na inasemekana alitaka ateswe kwani alimsema na alikataa kusaini bond ambayo itamyima haki yake ya kumshtaki makonda kwa udhalilishaji.
 
Eti Wema ataarifiwe leo kufika Polisi kesho na akaelezwa kuwa tuhuma yake ni madawa ya kulevya kisha siku ya tatu apekuliwe na kukutwa na msokoto wa bangi , it doesn't make sense. Lazima wazo la mtu kupandikiziwa kielelezo lishike hatamu.
 
Hakuna anayebisha kuwa kitendo cha wasanii kukamatwa, kuhojiwa, kufikishwa mahakamani na hatimaye kuachiwa huru kwa wepesi kiasi kile na hasa ikizingatiwa uzito wa tuhuma ni cha kisanii na kilichopeleka kilio kwa taaluma za watu hasa Simon Sirro mkuu wa jeshi la polisi kanda maalum ya kipolisi Dar es Salaam.

Pengine ni ukweli kuwa kufanya kazi chini ya Paul Makonda ni mzigo mzito sana. Ukifanya kazi na aina ya watu wanaoibukaibuka na madai lukuki huku wakikosa nyenzo muhimu kiakili kwenye madai yao basi uamue moja kati ya mawili. Ama kukubali udhalilike mara kwa mara au uachane na hiyo biashara ya kufanya kazi chini ya Makonda.

Simon Sirro ni miongoni mwa watu waliokutana na dhahama za Paul Makonda mfano ni lile sakata la shisha na hili la madawa ya kulevya la wasanii na usanii wa Makonda.

Tunapinga madawa ya kulevya lakini tunapinga zaidi usanii unaofanywa na Paul Makonda ambao unapelekea taaluma nyingine kudhalilishwa.

Jeshi la polisi limejiingiza kwenye mambo ambayo kimsingi yanaleta ukakasi mkubwa.

(1) Kwanini walienda kukagua nyumbani kwa msanii mmoja pekee wakati waliotuhumiwa ni wengi?

(2) Nini kinachoendelea kati ya Wema Sepetu na Paul Makonda? Nini hasa hatima ya tuhuma alizotoa Wema Sepetu kwa Paul Makonda mbele ya polisi na kusambaa kila kona kwenye mitandao mbalimbali?

(3) Ni kwanini mtu muhimu na mwenye ushahidi wa tuhuma ambaye ni Paul Makonda hajaitwa mbele ya mahakama ili kuthibitisha tuhuma zake kwa hao wasanii?

(4) Mahakama imejiridhisha vipi na tuhuma zilizotolewa bila hata kuwepo kwa kiashiria chochote kile cha ushahidi kwa hao baadhi ya wasanii na kisha kutoa hukumu?


Kamanda Sirro ameingia kwenye kuwa mtu wa kusikiliza kile anachosema Paul Makonda na kukifanyia kazi hapohapo bila hata ya kutafakari kwa kina jambo ambalo limehsaanza kujionyesha waziwazi.

Tufikie mahala tuache na kuheshimu taaluma za watu ili nchi iwe kwenye mkondo wa sheria na utawala wenye hadhi. Kama tutaendelea hivi basi kuna hatari ya kuupandikiza "Umungu mtu" kwa baadhi ya wakubwa hivyo kupelekea taifa kukosa dira madhubuti ya kiuongozi.

Zipo taarifa nyeti kuwa hata amri ya kukamatwa Tundu Lissu na kusafirishwa usiku wa manane kutokea Dodoma hadi Dar es Salaam ni amri toka kwa Paul Makonda! Kama kawaida jeshi la polisi likaingia tena mazima na kutekeleza amri pasipo hata kujiuliza.
Kwani Tanzania kula jeshi la polisi au nikitengo tu cha CCM?
 
Huyu bwana si ni Mkuu wa Mkoa wa Mikoa yote Tanzania bara? Sasa unachoshangaa ni nini? Aliposema kupanda Miti Siku ya Sept. 01,2016 Siku ya UKUTA mbona ilitekelezwa? Haiitaji akili kufikiri kuwa yeye ndie Boss mtoto kwa sasa
 
Hivi kazi ya Mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa mkoa ni pamoja na kupeleleza, kushtaki na kuhukumu? Huyu mungu wa dar ashauriwe aangalie job description yake. Yeye sio officer wa polisi wala msemaji wa jeshi la polisi. Unless aajiriwe na jeshi la polisi kwa mujibu wa sheria ili afanye majukumu ya polis kwa weledi.
 
Nilichokigundua ni watu wengi wanaomshambulia makonda kuwa ni mkurupukaji wao ndo wakirupukaji wakubwa hawadadavui mambo kwa kina
 
Je shisha ni madawa ya kulevya?hili swali naombamajibu kama jibu ni ndio sigara je ni dawa ya kulevya hali kadhalika ugoro.halafu nimwage facts au ni kuwapigia polisi miruzi mingi tu.
Mkuuu makonda hakusema shisha ni madawa ya kulevya hiyo weka akilini, alisema wanaouza shisha wanawachanganyia drugs watumiaji bila wao kujua kwa mujibu wa maelezo yake na TFDA,unataka ushahida unaweza omba wakupe, je hujawahi sikia kuwa kuna maeneo ya primary school wauza icecream walikuwa wanamix drugs kwenye icecream za watoto wa shule ya msingi! Kama ikiwa kweli kitu kama hicho kilikuwa kinafanyika je ni haki? Vitu vingine huwezi kuvijua kwa undani kama haupo kwenye field
 
Back
Top Bottom