G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Hakuna anayebisha kuwa kitendo cha wasanii kukamatwa, kuhojiwa, kufikishwa mahakamani na hatimaye kuachiwa huru kwa wepesi kiasi kile na hasa ikizingatiwa uzito wa tuhuma ni cha kisanii na kilichopeleka kilio kwa taaluma za watu hasa Simon Sirro mkuu wa jeshi la polisi kanda maalum ya kipolisi Dar es Salaam.
Pengine ni ukweli kuwa kufanya kazi chini ya Paul Makonda ni mzigo mzito sana. Ukifanya kazi na aina ya watu wanaoibukaibuka na madai lukuki huku wakikosa nyenzo muhimu kiakili kwenye madai yao basi uamue moja kati ya mawili. Ama kukubali udhalilike mara kwa mara au uachane na hiyo biashara ya kufanya kazi chini ya Makonda.
Simon Sirro ni miongoni mwa watu waliokutana na dhahama za Paul Makonda mfano ni lile sakata la shisha na hili la madawa ya kulevya la wasanii na usanii wa Makonda.
Tunapinga madawa ya kulevya lakini tunapinga zaidi usanii unaofanywa na Paul Makonda ambao unapelekea taaluma nyingine kudhalilishwa.
Jeshi la polisi limejiingiza kwenye mambo ambayo kimsingi yanaleta ukakasi mkubwa.
(1) Kwanini walienda kukagua nyumbani kwa msanii mmoja pekee wakati waliotuhumiwa ni wengi?
(2) Nini kinachoendelea kati ya Wema Sepetu na Paul Makonda? Nini hasa hatima ya tuhuma alizotoa Wema Sepetu kwa Paul Makonda mbele ya polisi na kusambaa kila kona kwenye mitandao mbalimbali?
(3) Ni kwanini mtu muhimu na mwenye ushahidi wa tuhuma ambaye ni Paul Makonda hajaitwa mbele ya mahakama ili kuthibitisha tuhuma zake kwa hao wasanii?
(4) Mahakama imejiridhisha vipi na tuhuma zilizotolewa bila hata kuwepo kwa kiashiria chochote kile cha ushahidi kwa hao baadhi ya wasanii na kisha kutoa hukumu?
Kamanda Sirro ameingia kwenye kuwa mtu wa kusikiliza kile anachosema Paul Makonda na kukifanyia kazi hapohapo bila hata ya kutafakari kwa kina jambo ambalo limehsaanza kujionyesha waziwazi.
Tufikie mahala tuache na kuheshimu taaluma za watu ili nchi iwe kwenye mkondo wa sheria na utawala wenye hadhi. Kama tutaendelea hivi basi kuna hatari ya kuupandikiza "Umungu mtu" kwa baadhi ya wakubwa hivyo kupelekea taifa kukosa dira madhubuti ya kiuongozi.
Zipo taarifa nyeti kuwa hata amri ya kukamatwa Tundu Lissu na kusafirishwa usiku wa manane kutokea Dodoma hadi Dar es Salaam ni amri toka kwa Paul Makonda! Kama kawaida jeshi la polisi likaingia tena mazima na kutekeleza amri pasipo hata kujiuliza.