Kamanda Nzowa ajitokeza, ataja mchungaji anayejihususha na dawa za kulevya

...ndio maana Mkuu ameagiza watumishi wa kiroho wakemee!



...well said!



...Loh, hukuiona hii?




RAIA wanne wa kigeni, Dennis Okechukwu na Paul Obi wote wa Nigeria, Stani Hycenth wa Afrika Kusini na Shoaib Muhammad Ayaz kutoka Pakistan wakitoka kusomewa mashitaka ya kula njama na kuingiza nchini dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya sh. bilioni 2.8, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam

Source: Habarileo
Wageni wadaiwa kuingiza Heroin za bilioni 3/-

na hapa; Home


hapa ukiangalia picha na origin zao unaona kabisa hawa jamaa ni matapeli na mtandao wao kupush mzigo kutoka pakistan-tz-south(mzigo unatua), tatizo ni uhamiaji utamruhusu vipi mtu humjui aingie nchini kufungua kanisa private, ingekuwa kiongozi wa katoliki, kkkt,nglican na madhehebu makubwa yanayojulikana tz sawa jk angekuwa na point lkn sio hawa wahuni
 
hapa ukiangalia picha na origin zao unaona kabisa hawa jamaa ni matapeli na mtandao wao kupush mzigo kutoka pakistan-tz-south(mzigo unatua), tatizo ni uhamiaji utamruhusu vipi mtu humjui aingie nchini kufungua kanisa private, ingekuwa kiongozi wa katoliki, kkkt,nglican na madhehebu makubwa yanayojulikana tz sawa jk angekuwa na point lkn sio hawa wahuni

...Tupo ukurasa mmoja. Hilo (penye red) pia linaangukia kwenye sera ya 'Uwekezaji?'
Kama jibu ni ndio, then rudia tena kumsoma '007' hapa;

... the core of the Nigerian drugs dealers cum 'born again faithful of churches of later day evangelism' can squarely be traced back into the gates of the Nigearian Commission in Dar in the form of dirty diplomats facilitating their relatives, kin and friends in such lucrative get rich quickly schemes by taking into adavantage, vivid porousity and other loopholes in our systems!

...Tanzania bado tupo nyuma kwenye hizi Background checks. Hata hivyo, haliondoi juhudi nzuri za maofisa wa usalama wanaofanya kazi usiku na mchana kurekebisha pale penye kasoro.
Hii habari inaifuatia ya huyu mama mgeni pia;

cocaine--300x198.jpg
Cocaine


Eight suspects including two Kenyans alleged to be drug dealers were yesterday charged with trafficking 5 kilogrammes of cocaine worth Sh225 million.The Kenyans, Ben Ngare and Anthony Karanja, were charged along with six Tanzanians including three women at the Kisutu Resident Magistrate’s Court.


The eight were arrested on Wednesday night in Dar es Salaam’s Mbezi suburb in the house of Mwanaidi Ramadhani Mfundo, who is believed to be a drug kingpin who has been black listed in many countries over her alleged involvement in the illicit business.
Charged along Ms Mwanaidi who is also identified as Mama Leila, were Sara Munuo, Alma Said, Yahya Ibrahim, Aisha Kungwi and Rajabu Juma. The accused were not allowed to enter any plea because the court does not have jurisdiction to hear the case.
State Attorney Patric Marogoi alleged that the accused were on June 1, this year, at Mbezi Beach area within Kinondoni District, arrested while trafficking 5kgs of cocaine worth Sh225 million.

...Tutafika tu.
 
kamanda nzowa wa kikosi cha kuzuia madawa ya kulevya amejitokeza na kumtaja mch. Kuchupu denis okechuku wa kanisa moja la 'kiroho' lililopo maeneo ya kinondoni biafra, kuwa ni mmoja wa wachungaji wanaotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya. Amesema akiwa pamoja na watu wengine mchungaji huyo alikamatwa na kilo 81 za cocaine mapema mwaka huu, na kuwa katika pile ya watuhumiwa wa matukio mbalimbali ya madawa ya kulevya, wapo pia viongozi wengine kadhaa wa kidini, ambao watatajwa baadae.

Source; channel ten (kipindi cha baragumu leo asubuhi)
wanafahamika kama anavyodai na wako wengine wengi kwa mujibu wa kauli yake,je ushahidi upo ?nakama upo wamechukuliwa hatua gani na lini?nakama hawajachuliwa hatua kwa nini?nakama wameanza kuchukuliwa hatua baada ya marumbano ya jk na viongozi wa makanisa je sheria hapa zinafuatwa kutokana na amri ya ris au ni nia ya kutaka kumsafisha kwa kauli yake?nakama hayo yalikua yanafahamika mapema kwanini hatua hazikuchukuliwa?huyo kamanda nzowa kama mambo yenyewe ndio hivyo nafasi aliyopo hapashwi kua katika nafasi hiyo kama ilivyo kwa boss wake.magamba yapo,mafisadi wapo,vigogo wauza unga wapo,viongozi wazembe wapo.wajiondoe wenyewe mlalahoi akiiba kilo moja ya mahidi akainusuru familia yake weke ndani!."jk futa mahakama zisizofanyakazi kupunguza matumizi na tutegemee huruma au fadhili ya waharifu kujisalimisha ktk vyombo vya sheria"MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Nzowa aende ITV akataje orodha ya wafanyabiashara wa Madawa ya kulevya.
 
Wana JF, mimi naliangalia swala zima la tuhuma hizi za madawa ya kulevya kuunganishwa na wakuu wa Dini/Maaskofu ni la kisiasa zaidi. Kwangu mimi hii ni saikolojia nyepesi sana. Imelenga kudhoofisha makali ya viongozi wa dini katika jitihada zao za kukemea uchafu mwingi ambao umekuwa ukifanywa na huu uongozi wa kifisadi. Hii ni mikakate ya kuwaogopesha wakuu wa dini ili wasijitokeze kukemea maovu ya hawa viongozi kwa hofu ya kubambikizwa kesi kama hizi. Ijapokuwa ni kweli kuwa biashara hii haramu ipo humu nchini lakini kuhusisha Maaskofu ni kisiasa sana. Huyu Mchungaji waliye mtaja nina mashaka sana kama kweli ni Mchungaji, na wala kama ni Mtanzania, jina lenyewe limekaa kigeni sana, na hata kama ni mchungaji huwezi ukatumia neno Maaskofu kwa kosa la mtu mmoja. Nina mashaka sana na kusudi la habari hii kuunganishwa na Maaskofu. Kwa Rais ambaye teyari amekuwa akitoa matamko ya kuwepo udini wakati hakuna kitu kama hicho, ndiye awe wa kwanza tena kuwataja Maaskofu kuhusika na madawa ya kulevya, kisha jinsi Ikulu ilivyo jibu ovyo ovyo, na jinsi kamanda Nzowa alivyo toa taarifa hii yenye jina la mgeni. Kwa kweli sioni lolote hapa zaidi ya mikakate ya kisiasa tu.




Kamwe hatutafumba macho safari hii bali tutayaona yote mpaka mwisho.
 
Mch. = Mchungaji Kuchupu Denis Okechuku wa kanisa.

Umewashuka shuuuuu!

Jina lenyewe linajulikana ni la mtu wa Nigeria. Nigeria inajulikana duniani kote kwa watu wake kujuhusisha na deal chafu kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo kujificha kwenye nyanja ya kidini.

Mtu mpuuzi tu kama FaizaMbwamwitu ndo anaweza shabikia ujinga huu kama ni suala la kuchafua wachungaji wa ukweli! Tulikwisha sikia mara kadhaa makontena ya madawa yamekamatwa lakini hatujasikia mienendo ya kesi hizo!
 
Kamanda Nzowa wa kikosi cha kuzuia madawa ya kulevya amejitokeza na kumtaja Mch. Kuchupu Denis Okechuku wa kanisa moja la 'kiroho' lililopo maeneo ya Kinondoni Biafra, kuwa ni mmoja wa wachungaji wanaotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya. Amesema akiwa pamoja na watu wengine mchungaji huyo alikamatwa na kilo 81 za cocaine mapema mwaka huu, na kuwa katika pile ya watuhumiwa wa matukio mbalimbali ya madawa ya kulevya, wapo pia viongozi wengine kadhaa wa kidini, ambao watatajwa baadae.

Source; Channel ten (Kipindi cha Baragumu leo asubuhi)

Huyu Nzowa ndiyo yule anedaiwa kutaka kumbambikia dawa za kulevya mtoto wa Mengi? Sijui anadhani tumesahau kuwa nae alishatuhumiwa uhalifu!
 
Siku hizi tuna madaktari (dkt) wa phd wengi sana - wa kweli na wasio wa kweli. Akitokea Mhe. Dkt. Pangupakavu akakamatwa na madawa ya kulevya, je itakuwa ni haki Rais kwenda Chuo Kikuu na kuwapa nasaha Ma-Dkt wa UDSM kuwa waache kijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya???:confused2:
 
Polisi wamnasa muuza dawa za kulevya wa kimataifa
Monday, 06 June 2011 21:03

Fidelis Butahe
JESHI la polisi nchini limewakamata watu wanane wakiwa na dawa za kulevya aina ya cocaine huku mmoja wa watuhumiwa hao, Mwanaidi Mfundo anayejulikana pia kwa jina la Naima Mohammed Nyakiniwa au Mama Leila aliyetajwa pia na Rais Barack Obama wa Marekani kama mtu hatari kwa biashara hiyo.

Kwa mujibu wa polisi, Leila ambaye ni raia wa Kenya amekatwa nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar es Salaam akiwa na wenzake saba. Alikutwa na hati sita za kusafiria zikiwa na sura tofauti tofauti.Wiki iliyopita Rais Obama alitangaza watuhumiwa saba wa biashara ya dawa za kulevya waosakwa zaidi ambao wamezuiliwa kuingia Marekani.

Kwa mujibu wa gazeti dada la Mwananchi, Daily Nation la Kenya, Mwanaidi ambaye ni mama wa mabinti watatu, waliokulia eneo la majengo lenye historia ya uhalifu na ufuska, ana makazi mengine katika eneo la matajiri la Kitisuru, jirani na makazi ya matajiri ya Westlands, Nairobi.

Gazeti hilo lilieleza pia kwamba Nyakiniwa alitajwa kuwa miongoni mwa vigogo wa dawa za kulevya wa kimataifa na Rais Obama Jumatano iliyopita kwenye Baraza la Congress. Pia katika orodha hiyo walitajwa Mbunge wa Kilome, John Haroun Mwau, mwenye biashara za aina mbalimbali nchini Kenya.

Kwa mujibu wa Wizara ya Fedha ya Marekani, Mama Leila anashughulika na biashara ya dawa za kulevya aina mbalimbali ikiwamo heroin ambayo huisafirisha Kusini Magharibi mwa Asia na cocaine anayoisafirisha kwenda Amerika ya Kusini.
Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Godfrey Nzowa alisema watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani Juni 3, mwaka huu.

Pia Jeshi hilo limetoa orodha ya kiasi cha dawa za kulevya aina ya heroine na cocaine zilizokamatwa tangu mwaka jana na idadi ya dawa hizo kwa mwaka huu inazidi idadi ya mwaka jana.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Nzowa alisema watuhumiwa hao walikamatwa na kikosi kazi cha udhibiti wa dawa za kulevya, Juni mosi, mwaka huu saa nane usiku huko Mbezi Beach.

"Walikamatwa wakiwa na kilo tano za cocaine na lita 3 za chloroform. Wote wamefikishwa mahakamani, walikuwa katika harakati za kusafirisha kwa kuwa walikuwa wameshazifunga dawa hizo katika mifuko ya kahawa," alisema Nzowa.Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Antony Arthur na Ben Machania kutoka Kenya pamoja na Sarah Munuo, Almas Said, Yahya Haroun, Rajabu Mzome na Aisha Kungwi ambao wote ni Watanzania.

Nzowa alisema Mfundo, maarufu kwa jina la Naima Mohammed Nyakiniwa ni mfanyabiashara wa kimataifa wa dawa za kulevya na kwamba alikuwa akisakwa na nchi mbalimbali duniani."Inawezekana walikuwa na kilo nyingi za dawa za kulevya ambazo walikuwa wameshazisafirisha, hizi dawa tulizozikamata zinaweza kuwa na thamani ya Sh200 milioni," alisema Nzowa.Alisema kuwa Mfundo pia alikutwa na hati sita za kusafiria ambazo zilikuwa na jina moja lakini sura tofauti: "Sura zake sita tofauti ambazo zilikuwa katika hati hizo za kusafiria zilimfanya ashindwe kutambulika kirahisi katika nchi alizokuwa akienda," alisema Nzowa.

Juni 3, watu watuhumiwa hao hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa shtaka la kuingiza nchini kilo tano za dawa za kulevya aina ya cocaine zenye thamani ya Sh225 milioni.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu Mustapher Siyani, Wakili wa Serikali, Patrick Malogoi alidai kuwa Juni Mosi, mwaka huu maeneo ya Mbezi Beach washtakiwa hao kwa pamoja kinyume na kifungu cha 16 (1) b (i) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya sura ya 95 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009, waliingiza nchini dawa hizo za kulevya.

Baada ya kuwasomea shtaka hilo, Hakimu Siyani aliwataka washtakiwa hao kutojibu chochote kwa sababu Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza shtaka linalowakabili hadi Mahakama Kuu ya Tanzania. Hakimu huyo aliiahirisha kesi hiyo hadi Juni 15, mwaka huu itakapotajwa tena.
Kuhusu mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya tangu mwaka jana, polisi imesema wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya waliokamatwa tangu kipindi hicho wote ni raia wa kigeni.

Nzowa alisema mwaka 2010, kilo 190 na gramu 780 za heroine zilikamatwa na washtakiwa walikuwa 496, wasafirishaji 10, watumiaji 480 na wafanyabisahara 12 huku watu sita wakikamatwa, wanne raia wa Iran na wawili wa Afrika Kusini.
"Cocaine zilizokamatwa zilikuwa kilo 64 na gramu 966, washitakiwa walikuwa 528, wasafirishaji watatu, watumiaji 521. Waliokamatwa walikuwa watu wanne ambao ni raia wa Liberia, Guinea, Ghana na Msumbiji."

Alisema bangi zilizokamatwa zilikuwa kilo 22,904 na gramu 905, watuhumiwa walikuwa 9,739, wasafirishaji 400, watumiaji 9,329 na wafanyabishara wakubwa 10 na kwamba ekari 296 za mashamba ya bangi yaliteketezwa huku watuhumiwa wanne wakikamatwa.
Alisema mirungi iliyokamatwa ilikuwa kilo 10,317 na gramu 502 na watuhimiwa walikuwa 1,351, wasafirishaji 200, watumiaji 1,146 na wafanyabiashara wakubwa watano.

Alisema mwaka 2011, dawa za kulevya aina ya heroin zilizokamatwa zilikuwa kilo 182 na gramu 402.39 na kwamba watuhumiwa walikuwa 1,080, wasafirishaji watatu, watumiaji 1,075 na wafanyabiashara wakubwa waliokamatwa walikuwa raia wawili wa Pakistani.
Alisema Cocaine zilizokamatwa zilikuwa kilo 91 na gramu 906, watuhumiwa walikuwa 1,070, wasafirishaji 15, watumiaji 1,048.

"Wafanyabiashara wakubwa waliokamatwa walikuwa saba, watatu Wakenya, wawili Wanigeria na wengine ni kutoka Pakistani na Afrika Kusini," alisema Nzowa na kuongeza:"Bangi zilizokamatwa ni kilo 17,257, watuhumiwa 1,000, wasafirishaji 20, watumiaji 970 na wafanyabiashara wakubwa 10. Mirungi iliyokamatwa ni kilo 15, watuhumiwa 40 na watumiaji 40."

Awali, Nzowa alisema mwaka 2009, kilo 9 za dawa za kulevya aina ya heroine zilikamatwa na kwamba walioshtakiwa walikuwa watu 122, wasafirishaji watano na watumiaji 117."Cocaine zilikamatwa kilo nne, washtakiwa walikuwa 108, wasafirishaji wawili na watumiaji 106.

Mirungi iliyokamatwa ilikuwa kilo 22,904, watuhumiwa waliokamatwa ni 365, wasafirishaji 20 na watumiaji 345. Bangi zilizokamatwa ni kilo 56,197, watuhumiwa 3382, wasafirishaji waliokamatwa walikuwa 200 ila watano ni raia wa Comoro na watumiaji walikuwa 3,182."
Alisema kuwa ekari 79 ziliteketezwa na watuhumiwa wenye mashamba waliokamatwa walikuwa tisa.

Pamoja na kuwa na nia njema, lakini Mheshimiwa Rais alikosea mahali pa kutolea ujumbe huo maana ingawa alizungumzia viongozi wa dini, ilichukuliwa kama vile amewalenga wakristu peke yao. Sasa huyu mheshimiwa mwingine kwa kumtaja mtu anayejifanya kuwa mtumishi wa Mungu wa kinaijeria ndio ameharibu kabisa. Ukiangalia habari yenyewe ni kuwa wote tumo, waislamu na wakristu. Mbaya zaidi ukiangalia watuhumiwa wa kitanzania wengi wao ni wenye majina ya kiislamu. Mheshimiwa angeitoa rai hii nje ya shughuli za kidini wala yasingetokea yote haya. Ni kama vile baadaya wale mabondia kukamatwa Mauritius, angeomba uongozi wa wana masumbwi wabanane. Hii vita ni yetu sote, wenye dini na wasio na dini. Na ni kweli inawezekana kuwa katika hao wanaotuongoza kuna baadhi ambao wanajihusisha na biashara hii ya kiovu. Ni wajibu wa vyombo vyetu vya usalama kuwachukulia hatua bila kuangalia dini, rangi, jinsia, uraia au kitu kingine.

Kitu kingine kinachonisikitisha katika hii taarifa niliyoiweka hapo juu ni utata unaozidi kujitokeza. Hivi kweli haramia aliyebobea atabeba pasi yenye jina moja na sura mbali mbali? Bendera nyekundu si huwa inastuliwa na jina na sio sura? Zaidi ya hapo, si rahisi zaidi kubadilisha jina na kubakiza sura? Kingine, mhalifu huyu hodari anachukua Cocaine bongo na kuisafirisha Amerika ya kusini! na heroin anaipeleka Asia! Ni kama vile ununue mafuta ili uyapeleke Saudi Arabia. Au ni hawa waandishi wetu feki ndio waliokosea kuleta habari?

Amandla....
 
Kamanda Nzowa wa kikosi cha kuzuia madawa ya kulevya amejitokeza na kumtaja Mch. Kuchupu Denis Okechuku wa kanisa moja la 'kiroho' lililopo maeneo ya Kinondoni Biafra, kuwa ni mmoja wa wachungaji wanaotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya. Amesema akiwa pamoja na watu wengine mchungaji huyo alikamatwa na kilo 81 za cocaine mapema mwaka huu, na kuwa katika pile ya watuhumiwa wa matukio mbalimbali ya madawa ya kulevya, wapo pia viongozi wengine kadhaa wa kidini, ambao watatajwa baadae.

Source; Channel ten (Kipindi cha Baragumu leo asubuhi)

Kwa hiyo huyu Mchungaji baada ya kukamatwa alipatiwa dhamana au kesi yake inaendelea? Kuna haja ya kuipitia tena sheria inayohusiana na usafirishaji na usambazaji wa mihadarati.
 
Subirini hayo arobaini na nane!Mmeyasikia ya Mkapa nayo hoko kwny Jubilee ya 50yr mbona hamsemi amepewa masaa mangap?Ila wazee hamna mshipa wa noma!Haya jamaa ameshatajwa na ametajwa huyo ili watu wajue wapo.Mmekua wadogo kama piritoni. Hv mnahc viongoz wa dini ni malaika au mitume kwamba hawana madhambi? Mbona wanawatoto kibao na wanabaka pia!Kwahyo wakiambiwa waelimishe watu madhara ya ubakaj pia mtaleta tabu!dah dini hz Dah ndo Mana akaleta Wajumbe wake kwe2 wamuabudu only 1 god. Isayah 43. 10-11
 
Mpaka juzi...Dr. Mokiwa alikua ni mmoja wa viongozi niliokuwa nikiwakubali, umakini wake na uwezo wake wakujieleza. Ni faswaha wa lugha na bila shaka ni mweledi kwenye taaluma na imani yake.

Nimeshtushwa mno na nikiri kama ameni-disapoint sana. Lugha na uslubi alioutumia kuomba ufafanuzi kwa mkuu wa nchi, Raisi imeonyesha dharau ya hali yajuu. Ultimatum aliyoitoa na kumuamuru Raisi afuate matakwa yake imeshangaza wengi. Kama kiongozi mkubwa angeweza kufikisha ujumbe wake na maoni yake nahata maombi yake katika hali ya adabu zaidi na akaeleweka.

Lakini kusema kama '' ikiwa Raisi hataweza kututajia viongozi wa dini wanaohusika na biashara ya madawa ya kulevya....basi tutamdharau na tutaona kama amekurupuka''. Hizi ni kauli za kifedhuli sana kulekezwa kwa kiongozi mkuu wa nchi.

After-all watu wanalazimisha kama mbona mafisadi walitajwa basi na Raisi nae alipaswa wataje hapo viongozi wa dini. Jibu nikuwa JK hajawahi kuwataja mafisadi ila wametajwa na CDM pale Tandika na PCCB kupitia kwenye kesi zinazoendelea.

Kamanda Nzowa leo kupitia Channel Ten amemtaja Mchungaji, mtumishi wa Mungu aliyekamatwa na shehena ya madawa. Kuna watu humu wamesema kama yule si Mtanzania. Jibu nikuwa ni kiongozi wa dini, anaendesha ibada zake Tanzania na wafuasi wake ni wa Tanzania na ameshikwa Tanzania.

Kikwebo.
Amekudisapoint kwani babako huyo au ulijua ni Mtakatifu au kaokoka?
Huyo Raisi alisha wahi adaa watu kipindi chake cha kwanza cha uraisi kuwa amekusanya majina ya watumia Unga na wauza Unga hadi leo miaka mitano na ushee hajataja hata mmoja kisa sheria zinamlinda.

Raia tu wakawaida ukisema unajua muuza madawa haramu Polisi watatia timu fasta kukushinikiza uwaelekeze (Nguvuni kwa kuisaidia Polisi)

Penginehiyo Kauli ya Mokiwa Itamsaidia Raisi kuacha Ukilaza wake na kufanya kuhifadhi majina ni mtaji wa Kisiasa.

Mpongeze zaidi ulitaka nae atumie njia ya ukilaza kuzunguka zunguka kukwepesha ukweli kama siasa zilivyo watu wa dini wanakupa live kuna vilaza na wasio vilaza..

Kama wewe ulitaka atumie njia nyingine na wewe ni Kilaza
 
kubambika nini wakati kweli wanauza unga... JF bwana ata hitler mngemtetea kama JK angemtaja. Watu kuweni na akili basi ata kidogo angalau..khaaa! Sio huyo tuu wako wengi wachungaji-UNGA
 
Mbona Fundi Maumba aliwahi kukamatwa akivila vitoto vya shule ya Mtendeni na hatujawahi kumsikia huyu jamaa akiwataka Wakw ere waache kuvila witi vitoto!

Kumkamata mjinga mjinga mmoja kwa kosa lake haku-justify kwamba watu wote wa jamii hiyo ni watenda dhambi hiyo.

Na dawa ya Mtendamaovu ni kumkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria hata awe nani na si kuanza kuwatukana na wengine wote waliopo kwenye jamii ile kwamba ni waalifu,

Mkuu huyo ndio maana yake, Kwani sasa hivi Watanzania wote mnajulikana kama waua Maalbino
Kana Nigeria inavyojulikana kwa utapeli
 
hapa ukiangalia picha na origin zao unaona kabisa hawa jamaa ni matapeli na mtandao wao kupush mzigo kutoka pakistan-tz-south(mzigo unatua), tatizo ni uhamiaji utamruhusu vipi mtu humjui aingie nchini kufungua kanisa private, ingekuwa kiongozi wa katoliki, kkkt,nglican na madhehebu makubwa yanayojulikana tz sawa jk angekuwa na point lkn sio hawa wahuni

issue wana wafuasi tanzania
 
Hivi Tanzania ni "Guilty until proven innocent" au "Innocent until proven guilty"? Sifahamu vizuri yanayojiri, lakini kwa nini mara karibu zote maelezo yanayotolewa huwaga ni ya upande mmoja? Kwa nini hatusikii maelezo ya upande wa pili (watuhumiwa)? Kwa nini maelezo ya watuhumiwa hayana fursa kabisa?
 
Back
Top Bottom