Kamanda Nkulila auawa kwa mapanga

Mahesabu

JF-Expert Member
Jan 27, 2008
5,972
3,830
Kamanda Nkulila auawa kwa mapanga


na Stella Ibengwe, Shinyanga


amka2.gif
KUNDI la watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia nyumbani kwa aliyekuwa mkuu wa kituo cha polisi cha uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam, Andrew Nkulila (64), na kumuua kwa kumkatakata mapanga.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Charles Nyanda, alisema tukio hilo lilitokea Novemba 24 mwaka huu saa mbili usiku katika eneo la mtaa wa majengo mapya Manispaa ya Shinyanga.
Kamanda Nyanda, alisema watu hao walipovamia na kuingia ndani ya nyumba hiyo, walimkuta marehemu akijiandaa kupata mlo wa usiku ndipo walipoanza kumkatakata kwa mapanga hadi kufa.
Ilielezwa kuwa kabla ya kuanza kumshambulia kwa mapanga watu hao walimuamuru mke wa marehemu awapatie bunduki iliyokuwa inamilikiwa na marehemu na baada ya tukio hilo walitokomea kusikojulikana wakiwa na silaha hiyo.
“Watu hao waliiamuru familia ya marehemu kuingia ndani na kuwa chini ya ulinzi huku wengine wakiendelea kumshambulia kwa mapanga marehemu bila kupata msaada wowote,” alisema. Enzi za uhai wake, Nkulila aliwahi kuwa mkuu wa kituo cha polisi Shinyanga, mkuu wa kituo cha polisi Newala na kuhamishiwa kituo cha polisi cha uwanja wa ndenge cha Dar es Salaam ambako alistaafu kazi ya polisi na kurudi nyumbani kwake mjini Shinyanga. Hakuna aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo.


SILAHA ZINAZIDI ZAGAA MTAANI...... POLISI JAMII INAZIDI KUFELI (kwa polisi wenyewe kuvunja mahusiano mema na raia kwa uonevu,ulaji rushwa n.k) NINI KIFANYIKE? TUSHAURIANE KUOKOA JAMII YETU
 
RIP Nkulila.

Poleni familia.

Tulaani vitendo hivi kwa pamoja uku tukihimiza serikali kuweka mikakati stahimilivu kupambana na vitendo hivi vya kiharamia vyenye kuchukua roho za Watanzania na wageni.
 
MOKOYO....TUHIMIZANE NA SISI WENYEWE SI SERIKALI PEKEE JUU YA KUPAMBANA NA UHALIFU WA KILA NAMNA... tunawajuwa...tunaishi nao.....WAUZA UNGA...MAJAMBAZI...VIBAKA...MAKAHABA...WALA RUSHWA.....WAONEVU N.K....kwa nini mimi na wewe tunawakalia kimya? je tumechukua hatua gani kudhibiti hali tete katika jamii yetu?
 
Jamani hii bongo yetu inaelekea wapi? Kidogo tutakuwa kama ndugu zetu sasa!
 
RIP kamanda, poleni wafiwa: nadhani ni visasi: nadhani kamanda shamsi vuai nahodha atalifanyia kazi tupate suluhisho la kudumu.
 
Namfahamu marehemu alikuwa OCS Mafia kabla hajahamishiwa airport Dar
 
Back
Top Bottom