Kamanda mwandamizi wa Hezbollah auawa na Israel nchini Syria

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
5,480
6,833
_89680778_89680777.jpg


Kamanda mwandamizi na mtaalamu wa Milipuko wa kundi la Hezbollah Mustafa Badreddeen ameuawa juma lililopita kufuatia mlipuko mkubwa unaoonekana kuwa ni shambulizi la anga la Israel katika jiji la Damascus.

Badredden pia amekuwa mshauri mkuu wa Kiongozi wa Hezbollah Haasan Nasrallah na mmoja ya watu watano wenye ushawishi mkubwa katika kundi hilo.

Marekani imekuwa ikimtuhumu mara kadhaa kuongoza mapambano ya wanamgambo wa Hezbollah nchini Syria dhidi ya vikosi wanaompinga Rais Assad.

Badredden ni binamu na shemeji wa aliyekuwa kamanda wa Hizbollah bwana Imad Mughniyeh aliyewahi kuvisumbua vyombo ulinzi Israel kwa miaka mingi (ingia Mtu aliyewasumbua majasusi wa Mossad kwa miaka zaidi ya 20 kufanikiwa kumuua ).

Pia alikuwa mwanafunzi wake mkuu katika masuala ya mapambano na hivyo ni pigo kubwa kwa Hizbollaah.

Badreddeen pia anatuhumiwa kuwa mshirika mkubwa wa Mughniyeh katika kutekeleza mauaji dhidi ya raia, wanadiplomasia na wanajeshi wa Israel, Marekani, na baadhi ya nchi za ulaya nchini Lebanon miaka ya 80

Mossad wameshafanya yao
 
Back
Top Bottom