Kamanda Muroto: CHADEMA wamepata kipigo cha "Mbwa kachoka" kwenye sanduku la kura, wakiandamana tutawapa kipigo cha "Mbwa koko"

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,874
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma mzee Muroto amesema jiji lake liko lipo shwari na wamejipanga vilivyo kuwalinda wageni wote wanaokuja kwenye sherehe za kuapishwa Rais Magufuli.

RPC Muroto amewataka CHADEMA wasijaribu kuandamana kwani baada ya kupata kipigo cha Mbwa kachoka kwenye sanduku la kura wao watawapa kipigo cha Mbwa koko endapo watajaribu kuingia barabarani kuandamana.

Kamanda Muroto amewataka wafanyabiashara wa Dodoma kujiandaa kuupokea ugeni huo mkubwa utakaopelekea kukuza uchumi wao.

Source: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
:D:D:DNimesoma aliyosema, mbavu zangukuuuu. Nimeona itakuwa msemo mpya nchini.

 
Ukweli mchungu
 

Attachments

  • Screenshot_20200518_071225.jpg
    Screenshot_20200518_071225.jpg
    78.1 KB · Views: 1
Andika majina yao na makazi, na kila kitu hadi tarehe na dakika hadi sekunde ya matukio...

Hata watu wakipigana wao kw wao.. au kulewa na kujiumiza.. na juu kubeba picha za mitandao ya duniani.. mnataka tu kusingizia..

Rais ndio tayari na tano tena.. muache uvivu mkachukue vya 20K.. wivi hakuna tenaaaaa.. lia tena na hizi

Huoni matundu ya risasi kwenye hiyo miili? kwanini hayo matukio yatokee yote kwa pamoja kwa wakati mmoja?

Mmechoma moto mpk nyumba ya bibi wa watu kwa bomu la kurusha, mkamuunguza na yeye mwilini, halafu unaleta utani kwenye maisha ya ndugu zetu na kiswahili chako cha Congo, uwe na adabu.
 
CCM wamechukua dola kwa njia haramu, hakuna propaganda itakayoweza kuubadili ukweli huo.

Waukubali ukweli turudie uchaguzi tuwe na maisha baada ya uchaguzi badala ya sintofahamu baada ya uchafuzi.
 
CHADEMA hawaamini wanagombea viti maalum sasa,

Siasa za Twitter hazijawahi kumuacha mtu salama.
 
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma mzee Muroto amesema jiji lake liko lipo shwari na wamejipanga vilivyo kuwalinda wageni wote wanaokuja kwenye sherehe za kuapishwa Rais Magufuli.

RPC Muroto amewataka Chadema wasijaribu kuandamana kwani baada ya kupata kipigo cha mbwa kachoka kwenye sanduku la kura wao watawapa kipigo cha mbwa koko endapo watajaribu kuingia barabarani kuandamana.

Kamanda Muroto amewataka wafanyabiashara wa Dodoma kujiandaa kuupokea ugeni huo mkubwa utakaopelekea kukuza uchumi wao.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Kwa maneno hayo huyu polisi fake anakosa sifa za kuwa Polisi
 
Back
Top Bottom