Tamu chungu
Member
- Dec 20, 2015
- 85
- 64
Imekua ni kawaida kwa daladala zinazopiga route ya Mbezi kwenda Kariakoo kujiongezea kiholela nauli toka Tshs 600 iliyopangwa na serikali hadi Tshs 1000 katika kituo cha kariakoo kuanzia majira ya saa tisa alasiri na kuendelea.
Kama mtu amegeuka na gari nauli hiyo kwake ni sahihi lakini si sahihi kwa abiria ambaye yupo kariakoo mwisho zinapogeuzia daladala kumtoza nauli ya Tshs 1000 eti tu kwakua amekalia siti.
Kitendo hiki si chakiuungwana kabisa sababu kinatuumiza sana sisi watanzania wa kipato cha chini hasa ukizingatia kwamba si wote watakaoweza kumudu kiasi hicho nauli inayopandishwa kiholela.
Tunaomba kamanda Mpinga uwe unatuwekea walau askari wawili wa kuweza kuzuia upandishwaji huu wa nauli ambao unatuumiza sisi wa kipato cha kubaingaiza.
Ninaamini kwa nafasi yako utakwenda kulishughulikia hili suala ambalo ni kero kwetu sisi walalahoi.
Asante