Kamanda Mpinga mchukulie hatua kali msanii Ali Kiba kwa kuvunja sheria za barabarani

Kwani lowassa huwa hasimami na kuonekana kichwa open roof?
Video ya huyo Kiba iliyoonyeshwa inaonyesha siyo open roof, bali jamaa wamekaa kwenye paa ya gari kama waliokaa kwenye mkeka.

Na ya mheshimiwa sana, haikuwa kusimama kwenye open roof, ila kuruka toka juu ya gari na kurukia chini.

Vile vile, kwa kuwa umeonelea uongezee mfano wa Lowassa, hata kama kusimama ndani ya gari open roof ingekuwa kosa na hakuchukuliwa hatua, basi inawezekana ingekuwa sababu ya "umaarufu wake"
 
Huyu nae yote hiyo ni kutaka kwenda sawa na Diamond,kitu ambacho hakipo na hakiwezekani katika dunia hii ya leo!
 
4fb3ebbaf8f27f6a0b2042d7cd5509d2.jpg
hizo zilichukuliwa mwaka mmoja tu mueshimuni sana mondi
 
Akiitwa kule atalipa faini tu na watapiga nae selfie nyie endeleeni humu
 
Mbona sioni mashabiki wamejipanga kwa road..alikua na ulazima gani wa kukaa juu ya roof kuonesha tuzo kwa mashabiki ambao hawajajitokeza
 
Kumbuka na kwenye kampain 2015. Magufuri alikuwa akitembelea juu ya gari. Vx . Tena akiwa kabeba mtoto .
 
Kwako Kamanda Mpinga,



Msanii Ali Kiba amefika nchini leo akitokea Afrika Kusini. Baada ya kufika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere alipokelewa na mashabiki wake.

Katika hali ya kushangaza msanii huyo amepanda juu ya gari na kushikilia tuzo yake kujigamba kwa mashabiki wake.

Kitendo hiki kinahatarisha maisha yake na maisha ya wengine wanaotumia barabara. Hatari hiyo ni zaidi ya kutofunga mkanda, kuendesha gari lisilo na breki, tairi lenye kipara etc.

Sheria za usalama barabarani haziruhusu ujinga huu hivyo msanii huyu achukuliwe hatua kali sana.

Kitendo alichokifanya ni zaidi ya dereva wa Itigi au Diamond Platnumz.

Jela inamnukia.

Hahaha akina dada wa madela kw wivu pole ni huyo ndio king Kiba pop in town sasa unaambiwa mfalme anaguswa bwn ndio ulivyo tunw
 
Hili tatizo linaendekezwa na mwenyewe Kamanda Mpinga. Alishindwa kumchukulia hatua Diamond, akafanya ushkaji na kumtoza faini sasa akimchukulia hatua Kiba ataonekana anamuonea. Kazi ameitaka mwenyewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom