Elections 2015 Kamanda Mawazo: Tumepigwa tena, mwenzetu anaweza kufa wakati wowote!

Sep 10, 2013
335
471
"Tukiwa kwenye mkutano wa hadhara maeneo ya kibo Sombetini mwenzetu mmoja amepigwa na kukatwa katwa mapanga,tumejitahidi kumwokoa lakini wenzetu walijiandaa vilivyo kwa silaha za jadi.

Niko na makamanda central na tayari kapewa PF3. Mi nimebaki ili kufungua jalada lakini OCD anakataa kwa kusema mi siyo eye witness.

Kinachoniuma ni ukweli kwamba majeruhi tukiwa ndani ya gari la police alimwona mshambuliaji wake na kuwataka police wamkamate lakini walikataa na kututaka tufungu jalada kwanza, kingine ni gari la police kutishiwa kugongwa na gari la CCM huku wakiimba TUNAMTAKA MAWAZO na wao kukaa kimya.

Tumekabidhi mapanga, nyundo, nondo name silaha nyingine tulizoshambuliwa nazo
 
Poleni sana makamanda; Mungu yuko nanyi.
Tunawaombea Majeruhi wapone haraka.
Aluta continua
 
Itabidi serikali iseme kama kunampango wa kuua raia wakati rais hajafa, je atakuwa rais wa nani???
 
Hakika hii damu inayomwagika, haitapotea bure. Mwenyezi Mungu awaongezee ujasiri katika magumu haya mnayokabiliana nayo.
 
Kwa mtindo huu inawezekana kabisa hata yale mauaji ya Tarime Musoma yamefanywa na CCM kwa kusingizia ni Jambazi kwani ni vema tukafahamishwa waliouawa ni watu wa aina gani maana unaweza kuta walikuwa wafuasi wa CHADEMA.
 
Hakuna kitu kibaya kama kuto jitambua. Huo moto wanao uwasha wajuwe hautawaunguza chadema tu, poleni sana makamanda.
 
Naichukia CCM kwa sababu ya matendo kama haya ya kigaidi. Lakini pia nanyi CHADEMA, mmekuwa dhaifu mno. Mnaonewa sana. Kama police hawawezi kuwasaidia kwa nini na nyie msipige? Uvumilivu unamwisho wake makamanda. Waswahili walisema,"ukishikwa shikamana" Wachache wabinafsi watasema ninafanya uchochezi, lakini ninachohimiza hapa ni kupambana na waonevu na si vinginevyo.
 
Magamba lengo lao wavuruge uchaguzi. Kama msajiri wa vyama hawezitoa onyo vijana Sombetini wachukue hatua za kujilinda na kulinda viongozi wa cdm. Hao vijana ni vibaka wa ccm, wadhibitiwe haraka!

Kamanda Mawazo pole and take care, we need you.
 
Mtu akitaka kufa sharti ajifaraguwe kwanza ndo maana akitaka kufa macho lazima yatoke pima na mwili ukakamae. Kifo cha CCM kimetimia.
 

Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom