Kamanda Mambosasa: Vigodoro haviendani na ustaarabu wa Dar, tutawashughulikia kabla hawajaanza kucheza

NGolo Kante

Member
Feb 28, 2017
80
131
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewaomba wadau mbalimbali wa amani kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi ili kuendeleza hali ya ushwari iliyopo sasa katika Jiji la Dar es Salaam.

> Tunaendelea kuwatahadharisha wazazi katika kipindi hiki cha sikukuu kila mmoja atimize wajibu wake wa kuhakikisha anajilinda yeye mwenye na watoto wake kwa kufanya hivyo sikukuu hii haitakuwa na madhara kwao

> Ktk sikukuu hii hatutarajii kuona Disco Toto, kwani mpaka sasa hatujapokea taarifa yoyote ya kuomba kibali hicho, kwahiyo Disco Toto ni marufuku katika Jiji la Dar es Salaam na tunataka watu washerekee maeneo yenye utulivu na salama zaidi kwao." Lazaro Mambosasa.

"Ngoma za vigodoro haziendani na ustaarabu wa Dar es Salaam na niseme tu kwamba tutakushugulikia kabla hata haujaanza kucheza ngoma hiyo" Lazaro Mambosasa.

Lazoro Mambisasa - Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam amepiga marufuku kusherekea sikukuu za mwisho wa mwaka kwa kulipua fataki pasipo kuwa na kibali cha kutumia fataki hizo kwenye maeneo maalumu.

Kwa msaada wa Kwanza TV
 
Vingekuwa vimeletwa na wazungu mngevishangilia lakini kwakuwa ni utamaduni wa Mzaramo mnaleta vitisho
 
Kubalini kwamba mmevamia jiji lao na sasa mnataka kuua utamaduni wao. Hilo ni jiji la wazaramo, wana tamaduni zao ikiwemo hicho kigodoro
Hata kama ungekuwa utamaduni wa kabila fulani lakini kama una elements mbovu tusiukubali kwenye jamii ya sasa ya kistaarabu. Kuna jamii yenye utamaduni wa kukeketa wanawake lakini imepigwa marufuku kwa sababu una madhara. Hivyo hivyo utamaduni wa kinamama kujidhalilisha kwa kucheza uchi wa mnyama siyo mzuri.
 
mambo Sasa,jiwe,mmewakuta wazaramo,ni sawa na kukataza nyama ya nguruwe isiliwe PERAMIHO
 
SASA TUCHEZE CHAGULAGA

Mbona chagulaga mpaka leo inaendelea kutamba
 
Hata kama ungekuwa utamaduni wa kabila fulani lakini kama una elements mbovu tusiukubali kwenye jamii ya sasa ya kistaarabu. Kuna jamii yenye utamaduni wa kukeketa wanawake lakini imepigwa marufuku kwa sababu una madhara. Hivyo hivyo utamaduni wa kinamama kujidhalilisha kwa kucheza uchi wa mnyama siyo mzuri.
mambosasa yupo sahihi, vigodoro ni upuuzi
 
Kwanza Siku hizi hakuna vigodoro au mambosasa amesahau ........
 
mambo Sasa,jiwe,mmewakuta wazaramo,ni sawa na kukataza nyama ya nguruwe isiliwe PERAMIHO
Vigodoro sio wazaramo vigodoro ni mikesha ya taarab usiku na ilishapigwa marufuku kitambo!! Siku hizi tunafagia uwanja jua kaliii 😉😉😉😉😉 ikifika SAA kumi na mbili jion kila mtu kwao. Labda ndio anamaanisha
 
Hata kama ungekuwa utamaduni wa kabila fulani lakini kama una elements mbovu tusiukubali kwenye jamii ya sasa ya kistaarabu. Kuna jamii yenye utamaduni wa kukeketa wanawake lakini imepigwa marufuku kwa sababu una madhara. Hivyo hivyo utamaduni wa kinamama kujidhalilisha kwa kucheza uchi wa mnyama siyo mzuri.
kucheza uchi ni akili ya mtu binafsi sio sheria ya kigodoro.
 
Back
Top Bottom