Kamanda Mambosasa: Upelelezi wa kesi ya wafuasi 27 wa CHADEMA wakiwemo viongozi wanaodaiwa kufanya fujo gereza la Segerea umekamilika

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,567
2,000
‪LIVE: Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM Lazaro Mambosasa anazungumza kuhusu kilichotokea juzi Segerea wakati Freeman Mbowe akisubiriwa kutoka gerezani

=====

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA


TAARIFA KWA UMMA.
KUKAMATWA KWA WAFUASI WA CHADEMA 27 KWA TUHUMA ZA KUFANYA FUJO KATIKA GEREZA LA MAHABUSU SEGEREA.

Mnamo tarehe 13.03.2020 majira ya saa 07:00 mchana Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilipokea taarifa kutoka kwa maofisa wa Gereza la Mahabusu Segerea kuwa kuna kundi la wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) likiongozwa na wabumbe wawili ambao ni Halima James Mdee, Ester Amos Bulaya na Meya wa Ubungo Boniface Jacob limekusanyika katika geti la kuingilia gerezani hapo huku likiandamana na kufanya fujo kutaka kuingia kwa nguvu ndani ya gereza kwa lengo la kwenda kumtoa mwenyekiti wa chama chao Mhe.Freeman Mbowe.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum baada ya kupokea taarifa hizo lilituma askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) na askari wa kituo cha Polisi Stakishari na ambapo walipofika eneo hilo waliwakuta askari magereza wakiwa wanaendelea kuwadhibiti wanachama hao na ndipo Polisi walipowakamata watuhumiwa 27.

Baada ya watuhumiwa hao kukamatwa askari wa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la magereza waliwachukua na kuwapeleka kituo cha Polisi Stakishari kwa mahojiano na baada ya mahojiano watuhumiwa wote 27 walidhaminiwa kwa mujibu wa sheria na watafikishwa mahakamani hivi karibuni kwani upelelezi wa shauri hili umeishakamilika.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa onyo kali kwa kikundi chochote cha siasa,dini,au mtu yeyote kuacha kabisa kuchezea maeneo nyeti kama magereza,makambi ya Majeshi yote au maeneo yoyote ambayo ni nyeti kwa taifa.

Hivyo atakayejaribu kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

WATU 03 WAPOTEZA MAISHA KWA AJARI YA BARABARANI.

Mnamo tarehe 15.03.2020 majira ya 04:30 alfajiri huko barabara ya kawawa mataa ya veta gari namba T 530 DNW aina ya EICHER daladala linalofanya safari za Mbangara- Makumbusho likitokea Mbagala kuelekea Makumbusho liligongana na gari la kubebea nyama lenye namba T 744 DET lililokuwa likitokea Tazara kuelekea katikati ya Jiji na kusababisha vifo vya watu watatu ambao ni wanaume wawili na mwanamke moja na kusababisha majeruhi ya watu nane.

Chanzo cha ajari ni daladala kutaka kuwahi kupita kwenye taa nyekundu.

LAZARO MAMBOSAS– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
15/03/2020

 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
41,780
2,000
Huyu siwezi kumuamini hata kidogo.

Kwenye hiyo kesi,wanaolengwa hapo ni Mdee na Bulaya, ila haya mambo mwisho wake ni kuwafanya viongozi wa upinzani na wafuasi wao kwa ujumla kuzoe Jela na hali hii ikitimia,basi tujiandae kwa maandamano na ghasia za kisiasa haya yakiwa ni matokeo ya watu kutoogopa jela na zaidi kuwa desperate hivyo kujiona hawana cha kupoteza kukaa/kwenda jela.
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,970
2,000
Huenda itakuwa anawajengea hoja ya kesi nyingine, kwanza ilitoka taarifa huko Dodoma, pili ilitoka taarifa Dar na hii sasa ni ya tatu! Wanausongo na Chadema.

Wafungwa wako nchini ya magereza siyo polisi ambao jukumu lao liliisha siku ya hukumu.
 

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
11,704
2,000
Duh, bonge la porojo. Yaani eti walikwenda kumtoa Mbowe kinguvu gerezani bila ya kufuata taratibu? Hao ni watu wa aina gani?

Ameanza kwa kusema watu wanaosemekana kuwa ni wafuasi wa CHADEMA halafu anaendelea kusema kwamba ni wafuasi wa CHADEMA.

Anaposema hakuna ushujaa kwa kutoka kwa kulipa dhamana, ilikuwaje Chakubanga Polepole alipokwenda na wana CCM mbona wao hawakupewa onyo la hivyo wala kukumbana na vurugu hizo.

Uwepo wa hao wabunge waliotajwa ulizingatia taratibu zote na ndiyo maana majina yao yapo kwenye daftari pale getini au tutoe register inayoonyesha majina yao kwamba walifuata taratibu?
 

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,138
2,000
Eti walikuwa wamekwenda kumtoa kwa nguvu kabla taratibu za kumtoa hazijakamilika, wakati taratibu zote zilishafanyika mahakamani na walichokuwa wamekwenda kukifanya ni kumpokea Mbowe wakati anatoka gerezani.
Mahakamani kuna taratibu zake, na magereza kuna taratibu zake. Eneo la Magereza siyo public toilet kwamba unaingia tu unavyojisikia wewe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom