Kamanda Mambosasa: Tapeli aliyekwamisha ununuzi wa nyumba za Lugumi, alitumwa na Lugumi ingawa sina fact

Akizungumza na Mwananchi leo (Ijumaa), Novemba 10, Kamanda wa Kanda polisi Dar, Lazaro Mambosasa amesema mazingira ya mnada na jinsi alivyokuwa akifika bei ya kununua nyumba hizo yamelifanya jeshi hilo lihisi ametumwa kukwamisha uuzaji huo.

“Aliwekwa na Lugumi mwenyewe ili mnada usifanyie ingawa sina fact (vielelezo) za kudhibitisha hilo, ila alichokuwa anakifanya kinatufanya tuamini hivyo. Alikuwa ana top (anapandisha) bei kila nyumba ili washiriki wengine wasinunue,

Ila jinsi alivyo, kwa maana ya uvaaji na kuongea kwake watu walitia mashaka kama ataweza kununua ndipo akatakiwa kutoa asilimia 25 na kushindwa kulipa. Tunaendelea kumshikilia kwa mahojiano,” amesema Mambosasa

Mwananchi lilipotaka kujua iwapo mtuhumiwa huyo amemtaja Lugumi katika mahojiano ya awali, Kamanda Mambosasa amesema upelelezi unaendelea na umma utapewa taarifa utakapokamilika.


Chanzo: Mwananchi
Amegeuka mpiga ramli?
 
Kamanda Mambosasa ni wa kuhurumia tu hakuna namna tena kwa maana SIASA ikishaingilia WELEDI mambo huwa shaghala baghala!!

Ninachokishangaa na kujiuliza ni "...hafanani hata na shilingi milioni moja!!!" Ndio ninajiuliza ikiwa Dr. SHIKA KWA MUONEKANO WAKE WA MAVAZI HAFANANI HATA NA SHILINGI MILIONI MOJA JE WALE ASKARI WALIOSHINDWA KUBAINI KABLA YA TUKIO LILE WANA THAMANI IPI?

JE KUWEKWA NDANI KWA DR. SHIKA MUDA MFUPI BAADA YA TUKIO HAKUSABABISHI MLENGWA KUONESHA KWAMBA ALIVURUGWA NA SI KWAMBA HAKUWA NA UWEZO?

JE NANI ANAWEZA KUTOA MAMIA YA MILIONI KWA MUDA MFUPI ULE AU KUHAMISHA FEDHA PASIPO KUANGALIWA SUALA LA UTAKATISHAJI? Pamoja na yote kuna mambo yamejificha juu ya suala hili. Waarabu wa pemba...

MINADA INGALI INAENDESHWA KAMA YA MITUMBA PALE KARUME!! UTENDAJI KAZI KIZAMANI UTAENDELEA KUTUGHARIMU.
 
Unless udoctor wake ni wa uganga wa kienyeji, lakini kama ni mtu msomi kutumwa na mtu na kukubali kufanya upumbavu ule anastahili pia institution ya kusimamia madaktari kumfungia kuendelea na professional hiyo ili asije kuuwa wagonjwa. Atibiwe kwanza looks to be mentally sick.
 
Huyu nae ni mpuuzi kweli. Hata kama ni kweli kama huna uthibitisho unaongeaje hivyo hadharani mtu mwenye cheo chake?






Kadri siku zinavyozidi naendelea kuamini kuwa hakuna wa maana serikali hii yote wote ni kama wana minyoo+funza kwenye bongo zao!
 
Huyu Mambo sasa....anaakili zotesawa sawa....?? Naona ana shida sana huyu Mambosasa mambo leo!! Anaropoka bila ushahidii
 
Back
Top Bottom