Kamanda Mambosasa: Tapeli aliyekwamisha ununuzi wa nyumba za Lugumi, alitumwa na Lugumi ingawa sina fact

11.jpg
 
Hivi siku hizi tumekuwaje? RPC kabisa unasema ingawa huna fact za kuthibitisha! sasa kama huna facts kwa nini unaongelea na kuhisi watu. Weledi weledi weledi. Hi ina imply kwamba basi kuna baadhi ya vitu watu wanakamatwa pasipo kuwa na facts. Aibu kabisa hii...
Ngoja Lugumi naye aubuke kudai fidia kwa kudharirishwa bila facts. Haki ya nani tena hiyo fidia yake watamlipia kodi
 
According to gazeti la mtanzania la leo Dr shika ni rais wa kampuni inatojishugulisha na masuala ya kemikali za viwandani ambayo makao makao yake makuu yapo URUSI,pia kamapuni iyo ijulikanayo kama LANCEFORT ilianzishwa mwaka 1999 na pia ina matawi ujerumani,uingereza na hispania na wana mpango wa kufungua matawi hapa nchini
We dada mrembo ...kama hiyo picha lakini
 
Polisi wetu pasua kichwa. Jitu halina facts ila bado linabwabwaja na kumrushia mtu mwingine serious allegations. Huyu mwekezaji wa viwanda 30 angeachiwa huru tu.
 
View attachment 628051

Katikati ya wiki hii kiliibuliwa kituko cha mnada wa nyumba za Mfanyabiashara Said Lugumi.

Kituko hicho kilifanywa na aliyedaiwa mfanyabiashara msomi Dkt. Luis Shika ambaye baadae alibainika ni tapeli na hatimaye kuzua gumzo mitandaoni

Kwa tunaojua kutafakari kwa kina kama great thinkers tunafahamu kwa nini kituko hiki kimekuja wakati huyu

Ikumbukwe kwamba hoja za kuyumba kwa uchumi na mahusiano mabaya na jirani zetu Wakenya zilipamba moto kuanzia mwanzoni mwa wiki. Hoja hizi ambazo nyingi ziliibuliwa na mbunge Zitto Kabwe na kushindiliwa na wabunge Hussein Bashe huku zikipata kuchochewa na makamanda mitandaoni

Pamoja na serikali kufurukuta kujibu lakini walishindwa kufanikiwa kutokana na majibu kushindwa kushabihiana na uhalisia wa mtaani

Wadau tunajua mbinu zinazotumiwa kubadilisha upepo hususani kwa jamii dhaifu kama ya watanzania waisojua kusimamia jambo mpaka mwisho....Ishu ya Dr Tapeli ni game changer

Tunakumbuka matukio mengi ya ajabu ajabu ambayo huletwa mahsusi kubadili upepo wa kisiasa. Kulikuwa na Babu wa Loliondo kwa wale wasiokumbuka
Lakini wote warefu
 
Kama ni kweli kasema hivyo basi hajui maana ya innocent until proven guilty,mimi nahisi huyo mnunuzi feki ni mtumishi wa wizara nyeti na anatumika kummaliza fisadi,kamanda ametuthibitishia.
 
Akizungumza na Mwananchi leo (Ijumaa), Novemba 10, Kamanda wa Kanda polisi Dar, Lazaro Mambosasa amesema mazingira ya mnada na jinsi alivyokuwa akifika bei ya kununua nyumba hizo yamelifanya jeshi hilo lihisi ametumwa kukwamisha uuzaji huo.

“Aliwekwa na Lugumi mwenyewe ili mnada usifanyie ingawa sina fact (vielelezo) za kudhibitisha hilo, ila alichokuwa anakifanya kinatufanya tuamini hivyo. Alikuwa ana top (anapandisha) bei kila nyumba ili washiriki wengine wasinunue,

Ila jinsi alivyo, kwa maana ya uvaaji na kuongea kwake watu walitia mashaka kama ataweza kununua ndipo akatakiwa kutoa asilimia 25 na kushindwa kulipa. Tunaendelea kumshikilia kwa mahojiano,” amesema Mambosasa

Mwananchi lilipotaka kujua iwapo mtuhumiwa huyo amemtaja Lugumi katika mahojiano ya awali, Kamanda Mambosasa amesema upelelezi unaendelea na umma utapewa taarifa utakapokamilika.


Chanzo: Mwananchi
"....ingawa sina fact..." sijaelewa hapa,Kamishna anaweza kusema hivyo wakati mtuhumiwa yuko naye?
 
Hana fact kakili mwenyewe lakin anakwambia katumwa na Lugumi halafu anaongoza taasisi nyeti huyo viongozi wa ajabu sana hawa.
Huwa wananishangaza wanavyojifanya akina mfalme njozi, hv kweli unaweka hisia zako kwenye mambo ya kisheria, hii ni hasara kwa taifa,
 
Aiseeeh yani MTU huna facts na unakili kuwa huna facts halafu unatuaminisha Mzee Tajiri ametumwa na Lugumi...


Aiseeeeh
 
“Aliwekwa na Lugumi mwenyewe ili mnada usifanyie ingawa sina fact (vielelezo) za kudhibitisha hilo, ila alichokuwa anakifanya kinatufanya tuamini hivyo. Alikuwa ana top (anapandisha) bei kila nyumba ili washiriki wengine wasinunue,

Kama polisi huyu ataendelea kuyafuata mawazo yake wala sio vielelezo nadhani atapotea na kupoteza wengi. Huenda ana biff na Lugumi.
Hata ikijapatikana baadaye kuwa jamaa alitumwa na Lugumi huoni tiyari ushahidi ushaingiwa mdudu? Nilimsikia alivyo jieleza kwa waandishi kuwa huyu katumwa na Lugumi. Huo sio utaratibu wa uchunguzi.
 
Back
Top Bottom