Kamanda Mambosasa: Saruji ipo ya kutosha jijini Dar, wanaopandisha bei ni wahujumu uchumi tutawashughulikia!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
39,958
2,000
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP), Lazaro Mambosasa amewataka wafanyabiashara kuuza cement kwa bei iliyowekwa na serikali vingiinevyo watashughulikiwa kisheria.

Mambosasa amesema jiji la Dar es Salaam lina cement ya kutosha hivyo yoyote anayeongeza bei ni muhujumu uchumi.

Chanzo: Channel ten

Maendeleo hayana vyama!
 

MZEE MKUBWA

JF-Expert Member
Jun 24, 2017
3,810
2,000
Bongo.com kila kitu kinafanyika kwenye media. Hizo cement anazosema zipo Dar es Salaam zipo wapi. Mara ya mwisho nimenunua mfuko mmoja Kwa elfu kumi na Saba tena Kwa kuelekezwa na wadau, badala ya bei elekezi ya elfu kumi na tano Mia tano.

Hapo kashamaliza kazi yake. Uzuri hiyo bei ni Kwa wote wanaopinga na wanaosifu juhudi. Wacha tuisome namba.
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
3,975
2,000
Sasa si wafungulie hio ya kutosha huko ilipo ili hao wapandisha bei wabaki nayo kama mapambo ?
 

Bupa2009

Member
Sep 15, 2020
61
125
Hekima na BUSARA vitumike katika kuliendea jambo hili, maguvu ya mabunduki na kutengenezeana kesi za UHUJUMU UCHUMI hakutatatua tatizo, badala yake kutupatia maumivu sisi wanyonge wa hali ya chini ya maisha.
 

Chibolo

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
4,376
2,000
Polisi wameanza kuingilia biashara tena duh!!! Mbona hii hatareee tena!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom