Kamanda Mambosasa aeleza jambazi Komando kutoka Burundi wa wenzake wawili walivyouawa na Polisi

Nijuavyo mimi, watuhumiwa wa ujambazi, wakienda kuonyesha silaha, au kutoka popote nje ya mahabusu, huwa wamefungwa pingu na ulinzi mkali, watu wenye pingu, wataroka vipi, kwa distance ipi kushindwa kuwa destabilize kwa kuwapiga risasi za miguu?!.

Naamini huu ni utekelezaji wa agizo hili,na askari hao wanasubiri kupandishwa vyeo!.
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...

IGP Kamanda Sirro, Usiruhusu Vifo Vya Uzembe Kama Huu Kuchafua Jeshi Letu Safi la Polisi!.

Karma is for real.

Paskali[/QUOTE)
Ila kwa komando pingu sio kitu kwake.
 
Tatizo siku moja atakamatwa mtu asiye na hatia akauwawa kwa maelezo ya kuwa ni jambazi na sisi raia kama.kawaida tutalipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi nzuri.
 
Ukiwaua unapataje full network yao sasa maana hawa jamaa lazima wapoa wengi na ukiua wote wengine ni furaha yaoe kuwa wamesalimika?
 
Hii ya kuua wahalifu haitatui tatizo la uharifu dunia nzima spwcially hapa nchini tuwakamate na kuwahoji tujue network yao alafu tunawaua tena kwa kuwapiga mawe hadi kifo
 
Jamani story hiu mbona ina plot holes nyingi mno,hata wangenipa mie kazi ya kutengeneza story ningetunga nzuri zaidi.
 
Katika kitu polisi wetu wanashindwa kufanya huwa ni kuwahi hospital kabla majeruhi hajafariki.

Sijui huwa wanakwama ktk mataa foreni??
 
Nijuavyo mimi, watuhumiwa wa ujambazi, wakienda kuonyesha silaha, au kutoka popote nje ya mahabusu, huwa wamefungwa pingu na ulinzi mkali, watu wenye pingu, wataroka vipi, kwa distance ipi kushindwa kuwa destabilize kwa kuwapiga risasi za miguu?!

Naamini huu ni utekelezaji wa agizo hili,na askari hao wanasubiri kupandishwa vyeo!.
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...

IGP Kamanda Sirro, Usiruhusu Vifo Vya Uzembe Kama Huu Kuchafua Jeshi Letu Safi la Polisi!.

Karma is for real.

Paskali

Maswali mazuri
 
Hii ya kuua wahalifu haitatui tatizo la uharifu dunia nzima spwcially hapa nchini tuwakamate na kuwahoji tujue network yao alafu tunawaua tena kwa kuwapiga mawe hadi kifo

Kwa nnavyojua Mimi, ,huwa kwanza wanahojiwa aswa na kikosi kazi maalum,,, baada ya hapo sasa safari inaanza iwe ya kheri au shari,,, Ila police ukiona hadi wamewaua hao jamaa,,,basi asilimia kubwa ni majambazi kweli 90%,, ila kwenye suala la ugaid mi ndio huwa wananikeraga ,,aswa kama mahuaji ya yule mtoto kule mikumi juzi kati,,, yaani mtu akiwa mashika dini sana,,,au mcheza karate,,basi we ni gaidi.

Kwa upande wa majambazi wanajitaidi sana kuvuruga mtandao wao nakuwapoteza kabisa
 
Warundi Ni watu hatari sana.
Nguvu nyingi ielekezwe mkoa wa Kagera na kigoma kuanzia kalenge-Ngara kagera, Kakonko-kigoma. Pori LA nduta-Kibondo, Pori LA malagarasi-kibondo to Kasulu road. Mubondo-kasulu.
Maeneo haya Ni hatari sana sanaaa. Warundi wanamiliki silaha nzito.
 
Kamanda Mambosasa aeleza jambazi komando kutoka Burundi wa wenzie 2 walivyouawa na polisi

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limewauwa majambazi watatu akiwemo raia wa Burundi ambao walikuwa wakifanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo na nchini kwa ujumla.

Hayo yameelezwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ambapo amesema kuwa katika majambazi hao watatu waliouwawa kwenye oparesheni maalum ya jeshi hilo, iliyofanyika kuanzia Novemba 11 hadi 30, 2017 alikuwepo raia mmoja wa Burundi aliyejulikana kwa jina la Fanueli Luchunda Kamana ambaye ana mafunzo ya kijeshi na kufikia ngazi ya Komando.

“Baada ya kuwakamata na kuwafanyia mahojiano walikubali kuonyesha silaha moja aina ya AK 47 pamoja na Magazine mbili zenye jumla ya risasi 57 ambazo zote walikuwa wameficha kwenye vichaka maeneo ya Ubungo Mawasiliano” amesema Kamanda Mambosasa.

Aidha Mambosasa ameeleza kuwa raia huyo wa Burundi ndio alikuwa kiongozi wa kundi hilo ambapo alikuwa anakwenda Burundi kila baada ya kufanya tukio. Ameongeza kuwa baada ya kwenda kuonesha silaha walizokuwa wameficha katika eneo jingine, Mburundi huyo alimvamia askari kwa lengo la kumshambulia ili wajinasue.

“Baada ya kumvamia askari wetu majambazi wale wawili walianza kukimbia lakini askari wetu walifanikiwa kuwadhibiti kwa kuwafyatulia risasi na baadae kuwafikisha katika hospitali ya Mwananyamala ambapo walibainika kuwa wamefariki”, amesema..

source: Mpekuzi
Kazi nzur
 
Back
Top Bottom