Kamanda Mambosasa aeleza jambazi Komando kutoka Burundi wa wenzake wawili walivyouawa na Polisi

claytonx

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
1,846
2,000
Kamanda Mambosasa aeleza jambazi komando kutoka Burundi wa wenzie 2 walivyouawa na polisi

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limewauwa majambazi watatu akiwemo raia wa Burundi ambao walikuwa wakifanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo na nchini kwa ujumla.

Hayo yameelezwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ambapo amesema kuwa katika majambazi hao watatu waliouwawa kwenye oparesheni maalum ya jeshi hilo, iliyofanyika kuanzia Novemba 11 hadi 30, 2017 alikuwepo raia mmoja wa Burundi aliyejulikana kwa jina la Fanueli Luchunda Kamana ambaye ana mafunzo ya kijeshi na kufikia ngazi ya Komando.

“Baada ya kuwakamata na kuwafanyia mahojiano walikubali kuonyesha silaha moja aina ya AK 47 pamoja na Magazine mbili zenye jumla ya risasi 57 ambazo zote walikuwa wameficha kwenye vichaka maeneo ya Ubungo Mawasiliano” amesema Kamanda Mambosasa.

Aidha Mambosasa ameeleza kuwa raia huyo wa Burundi ndio alikuwa kiongozi wa kundi hilo ambapo alikuwa anakwenda Burundi kila baada ya kufanya tukio. Ameongeza kuwa baada ya kwenda kuonesha silaha walizokuwa wameficha katika eneo jingine, Mburundi huyo alimvamia askari kwa lengo la kumshambulia ili wajinasue.

“Baada ya kumvamia askari wetu majambazi wale wawili walianza kukimbia lakini askari wetu walifanikiwa kuwadhibiti kwa kuwafyatulia risasi na baadae kuwafikisha katika hospitali ya Mwananyamala ambapo walibainika kuwa wamefariki”, amesema..

source: Mpekuzi
 
claytonx

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
1,846
2,000
Mimi nachowapendea askari wetu siku hizi ni hiyo tabia ya kutowakamata majambazi na sijui kuanza kuendesha nao makesi. Huu utaratibu wa kuwalaza chini umekaa vizuri sana.
Na hawajisumbui kutafuta story kuubwa ya kutangazia umma" just simple and clear" walikua wanataka kutoroka tukawajeruhi.....kufika hospitali walikua teyari washakufa....hata wakiwa kumi ni hivohivo...hakibadilishwi kitu
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,969
2,000
Ameongeza kuwa baada ya kwenda kuonesha silaha walizokuwa wameficha katika eneo jingine, Mburundi huyo alimvamia askari kwa lengo la kumshambulia ili wajinasue.
“Baada ya kumvamia askari wetu majambazi wale wawili walianza kukimbia lakini askari wetu walifanikiwa kuwadhibiti kwa kuwafyatulia risasi na baadae kuwafikisha katika hospitali ya Mwananyamala ambapo walibainika kuwa wamefariki”, amesema..(.source mpekuzi)
Nijuavyo mimi, watuhumiwa wa ujambazi, wakienda kuonyesha silaha, au kutoka popote nje ya mahabusu, huwa wamefungwa pingu na ulinzi mkali, watu wenye pingu, wataroka vipi, kwa distance ipi kushindwa kuwa destabilize kwa kuwapiga risasi za miguu?!.

Naamini huu ni utekelezaji wa agizo hili,na askari hao wanasubiri kupandishwa vyeo!.
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...

IGP Kamanda Sirro, Usiruhusu Vifo Vya Uzembe Kama Huu Kuchafua Jeshi Letu Safi la Polisi!.

Karma is for real.

Paskali
 
Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
9,892
2,000
Tumewadhibiti kwa risasi. Baada ya kuwapeleka Mwananyamala, tukaambiwa wameshafariki. Sounds familiar? Modus operandi ya police wetu. Kwanini huwa hawawachapi risasi za viunoni au miguuni ili waje wawahoji vizuri majeruhi? Jamaa wanatupia za kichwani tu au kifuani. Shoot to kill and interrogate maiti later.
 
bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,675
2,000
Na hawajisumbui kutafuta story kuubwa ya kutangazia umma" just simple and clear" walikua wanataka kutoroka tukawajeruhi.....kufika hospitali walikua teyari washakufa....hata wakiwa kumi ni hivohivo...hakibadilishwi kitu
Yaani hawapatagi taabu siku hizi...
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,762
2,000
Nijuavyo mimi, watuhumiwa wa ujambazi, wakienda kuonyesha silaha, au kutoka popote nje ya mahabusu, huwa wamefungwa pingu na ulinzi mkali, watu wenye pingu, wataroka vipi, kwa distance ipi kushindwa kuwa destabilize kwa kuwapiga risasi za miguu?!.

Naamini huu ni utekelezaji wa agizo hili,na askari hao wanasubiri kupandishwa vyeo!.
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...

IGP Kamanda Sirro, Usiruhusu Vifo Vya Uzembe Kama Huu Kuchafua Jeshi Letu Safi la Polisi!.

Karma is for real.

Paskali
Huu ni uchambuzi wenye sifa zote za mtu mwenye weredi na uzoefu mkubwa katika mambo mbalimbali, hapa ametoa majibu yote.
 
bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,675
2,000
Nijuavyo mimi, watuhumiwa wa ujambazi, wakienda kuonyesha silaha, au kutoka popote nje ya mahabusu, huwa wamefungwa pingu na ulinzi mkali, watu wenye pingu, wataroka vipi, kwa distance ipi kushindwa kuwa destabilize kwa kuwapiga risasi za miguu?!.

Naamini huu ni utekelezaji wa agizo hili,na askari hao wanasubiri kupandishwa vyeo!.
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...

IGP Kamanda Sirro, Usiruhusu Vifo Vya Uzembe Kama Huu Kuchafua Jeshi Letu Safi la Polisi!.

Karma is for real.

Paskali
Nikupendeacho Pascal Mayalla: huwa unaweka evidence/link katika post zako...kimsingi mimi binafsi huwa nakuelewa sana brother!

"auaye kwa upanga atauliwa kwa upanga pia"
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
38,326
2,000
Nijuavyo mimi, watuhumiwa wa ujambazi, wakienda kuonyesha silaha, au kutoka popote nje ya mahabusu, huwa wamefungwa pingu na ulinzi mkali, watu wenye pingu, wataroka vipi, kwa distance ipi kushindwa kuwa destabilize kwa kuwapiga risasi za miguu?!.

Naamini huu ni utekelezaji wa agizo hili,na askari hao wanasubiri kupandishwa vyeo!.
Hili la Polisi kuruhusiwa 'kuwanyanganya' silaha majambazi na kupandishwa vyeo limekaaje?
Vifo vya Mahabusu Mwanza, IGP Mangu, Usikubali Kudanganywa ...

IGP Kamanda Sirro, Usiruhusu Vifo Vya Uzembe Kama Huu Kuchafua Jeshi Letu Safi la Polisi!.

Karma is for real.

Paskali
Mkuu kuna uzi umetoka kuwasifia hawa polisi, now umewageuka tena?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom