Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!

Kwa niaba yake asante
Wanabodi, mimi nilidhani Lissu hatarejea
Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!


Final Update
Tundu Lissu leo amerejea nyumbani Tanzania, hivyo naomba kuthibitisha humu kuwa Tundu Lissu ni Jasiri na Shujaa Kuliko Nelson Mandela.

Hivyo sasa, kufuatia kurejea huku, ule ushauri wangu nilioutoa kwake kabla hajashambuliwa, sasa utekelezwe.

Uchaguzi 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

Shujaa Kamanda Tundu Lissu, karibu nyumbani.
Mungu ni mwema amekutendea muujiza, hivyo endelea kutimiza ndoto yako, Mungu aliyekuponya ni Mungu mwenye uwezo, anaweza kabisa kulifanya "Jiwe Walilolikataa Waashi, Likafanywa Jiwe Kuu la Pembeni"

I wish him all the best.
Paskali
 
mkuu wa kitengo cha watu wasiojulikana (Bashite) anapita na kusoma hapa kimyakimya huku udenda wa tamaa za mauaji unamtoka!!.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hivi waliompiga risasi Tundu Lissu bado hawajapatikana?

Na je wakipatikana na kupewa adhabu stahiki baadae wanaweza kusamehewa?


ttps://www.jamiiforums.com/threads/kikwete-awaachia-huru-polisi-waliomuua-jenerali-kombe.181478/
 
Paskali kwa uzi huu uliopost sahau kabisa uteuzi! Maana unauma huku na kule!

Mtanzania halisi wewe

Nyie ndio wabaya kuliko wasiojulikana au ccm

Mawazo yako ni machafu

Nenda kwa mama yakonakuwekee mkono kwenye ulimi na ubongo wako

Katika maisha usisemee mioyo ya wengine ni DHAMBI

Yote hapo juu nitayafuta ikiwa una uthibitisho pas na shaka kuwa pasko anatafuta uteuzi

Tunaomjua miaka yote hata kabla ya JF yuko hivyo, anaongea anachokiamini

Wewe mwenye ID fake na bado unauza karanga za kuchemka umebaki kuangalia...mwanaume gani anateuliwa nani hateuliwi, ili hali hata wewe ungependa uteuzi bisha!!!!!
 
Mkuu naona umerejea baada ya ndoto yako kuzima ghafla.

Tusikate tamaa, Mheshimiwa rais mama yetu Mama Samia Suluhu Hassan ni mtu muungwana sana, mweledi, asie mdini wala mbaguzi.

Nakuhakikishia kama unastahili uteuzi basi utaupata tu wala usiwe na fikra zile za kwamba ungepata uteuzi kwa kuwa wewe ni msukuma na sasa huwezi pata tena. Laaa hasha!

Karibu tena jukwaani uandike yale ambayo yalikutambulisha wewe na kukujengea heshima kuu ambayo tungekukumbuka kwayo baada ya kuondoka kwako.

Ni matumaini yangu kuwa utajiengua mapema Sana kwenye kundi la kuimba sauti ya kwanza (sauti ya mapambio).

Kijana wako,
Relief Mirzska.
 
Naona Mayala karejea JF baada ya kifo cha Ngosha.
Nashindwa kusoma codes hapa.
Kitupi tu, huenda kibarua cha Msigwa kikaota mbawa muda mfupi ujao maana leo anaapishwa mama Samia.

Pasco hii awamu jipange kutoboa fresh ikiwa utacheza karata zako fresha.
 
welcome back bro,
kabla ya yote nikupongeze kwa kujipa likizo na kupata pumuziko la kutosha,nina uhakika kuwa sasa uko fit kuendeleza pale ulipoachia kwenda mbele.
Lisu arudi home,asamehe,asahau yaliyopita asiendelee kugombana na marehemu,kwani hakimu wa haki yupo mbele yao amwachie ahukumu,kuendelea kugombana na marehemu sio mila na destuli zetu waafrika nahata naweza kuthubutu kusema sio kawaida ya binaadamu kugombana na walio kwisha nyamaza huwa tunawaombea heri tu kazi ya hukumu tunamwachia Mungu.
Mwambieni LISU anapaswa kuonyesha kuwa anajua kusamehe, kama hawezi kusamehe hafai kuwa kiongozi,kwani hatutaiona tofauti yake na anaemchukia.
 
Dah! Kumbe huyu mwamba wa JF bado yupo!?
Kweli watu wabaya sana, brother ulishazushiwa mengi sana humu kama Corona ilishafanya yake wengine wewe ndio yule KIGOGO nk.

Ila Mungu mkubwa leo umeonekana tena humu
 
welcome back bro,
kabla ya yote nikupongeze kwa kujipa likizo na kupata pumuziko la kutosha,nina uhakika kuwa sasa uko fit kuendeleza pale ulipoachia kwenda mbele.
Lisu arudi home,asamehe,asahau yaliyopita asiendelee kugombana na marehemu,kwani hakimu wa haki yupo mbele yao amwachie ahukumu,kuendelea kugombana na marehemu sio mila na destuli zetu waafrika nahata naweza kuthubutu kusema sio kawaida ya binaadamu kugombana na walio kwisha nyamaza huwa tunawaombea heri tu kazi ya hukumu tunamwachia Mungu.
Mwambieni LISU anapaswa kuonyesha kuwa anajua kusamehe, kama hawezi kusamehe hafai kuwa kiongozi,kwani hatutaiona tofauti yake na anaemchukia.

Lissu ni mnyama

anagombana na maiti na bado anashindwa
 
Wanabodi,
.
Hitimisho
Kwa maoni yangu, namshauri Kamanda Tundu Lissu, kama ni kurejea tuu nyumbani, arejee tu nyumbani Tanzania wala asisubiri jibu la barua zake kwa IGP Sirro kuhusu kumhakikishia ulinzi na usalama wake, kwasababu kwanza just his survival tuu alone, is beyond human beings ability and capabilities, it's a miracle from The Devine intervention hivyo Aliyemlinda na shambulio lile baya la kutisha na kusikitisha hadi kubakia hai mpaka leo, Yupo!, Aliyemsimamia matibabu akatibiwa hadi akapona Yupo!, Aliyeyafanya yote hayo ni YEYE Mwenye Aweza, awezaye yote! Namhakikishia YEYE Awezaye yote, Ataendelea kumlinda. Na usikute yote hayo Lissu aliyopitia na anayopitia, ni mapito tuu ili YEYE kuonyesha Uweza Wake kwa watu wa mataifa, na hata katika ukombozi wa Ulimwengu huu, ni kwa Kupigwa Kwake, sisi tuliponywa, hivyo at this juncture, Tundu Lissu hatakiwi tena kuendelea kutegemea uwezo wa binaadam katika ulinzi wa uhai na usalama wake, amtegemee YEYE. Tundu Lissu Atamke maneno haya, "NAYAWEZA YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE NGUVU"

Welcome Back Home, Kamanda Mdogo wangu Lissu (mimi ni kaka yake kule shuleni Ilboru)

Mwacheni Mungu Atwe Mungu
Welcome back home Kaka Mdogo Tundu Lissu.
Mimi Kaka yako Mkubwa
Karibu Nyumbani.
Paskali.
Wanabodi,
hii nchi drama will never end!. Kama enzi za JPM, Lissu aliandika barua kwa IGP Sirro kuomba kuhakikishiwa usalama wake, na hakujibiwa lakini akarejea na kubaki salama, kisha akaikimbia nchi tena.

Nilidhani baada ya kifo cha JPM, wakimbizi wote wa kisiasa akiwemo mwandishi mwenzetu wa habari, wangerejea.

Leo asubuhi kupitia Amka na BBC nimemsikia Lissu akisema anatamani kurejea nyumbani, hivyo amemuomba Mama Samia amuhakikishie usalama wake!. Kiukweli this is a joke!. Yaani Lissu enzi za JPM alirudi na kujiondokea, leo ndio mtu wa kuomba kuhakikishiwa usalama!.

Kiukweli kabisa kama mimi ni Mama, atakuwa alimjibu pale pale rudi nyumbani sisi hatuna issue yoyote na wewe na hao wakimbizi wenzako, rudini tuu nyumbani.

Lissu hakusema kuwa tayari ameisha kuhakikishiwa usalama, hivyo amesema hivyo ili Mama Samia aseme in public Lissu njoo nyumbani utakuwa salama as if waliomdhuru ni serikali, tunawajua, hatuta kudhuru tena!.

Ushauri wangu wa bandiko hili kwa Lissu still stands.

Lissu kama ni kurudi nyumbani, wee jirudie tuu, wala usisubiri hakikisho la Samia, hakuna mtu wa kuhangaika na wewe,
ubaya Yule Mlinzi Mkuu!.
P
 
Wanabodi,
Kuhusu wale wasiojulikana waliokushambulia, according to postulates na theories mbalimbali kuwahusu wasiojulikana hao, japo malengo yao kwako, yalikuwa ni malengo fulani ambayo hayakutimia, hivyo unawasiwasi ukirejea, watakamilisha, nakuhakikishia kuwa hata ukirejea sasa bila hakikisho la IGP Sirro, wale wasiojulikana wako, hawawezi tena kuikamilisha ile kazi kwasababu kazi nyingine ni za only one try, iki fail, ndio basi tena, ni kama uchawi, mchawi ukiisha mshtukia, hakulogi tena.

Paskali.
P
 
nakuhakikishia kuwa hata ukirejea sasa bila hakikisho la IGP Sirro, wale wasiojulikana wako, hawawezi tena kuikamilisha ile kazi kwasababu kazi nyingine ni za only one try, iki fail, ndio basi tena, ni kama uchawi, mchawi ukiisha mshtukia, hakulogi tena.
Hii theory ina ukweli ?...
 
Back
Top Bottom