Kamanda Lema tia mguu hapa, nawe msomaji dondoshea japo tonge moja.

Nairobifly

Member
May 3, 2012
65
95
Wilaya ya Ngorongoro: Ndugu wana JF hasa wale wafuasi wa chama makini (cdm) nimebahatika kutembelea kwa ujumla ktk wilaya hii. Wilaya hii ina tarafa tatu(Loliondo, Sale, na Ngorongoro). Hakika ktk tarafa 2-Loliondo na Sale kiujumla wananchi wamefunguka na magamba-ccm hawana chao pale. Tatizo lipo kwa tarafa moja ya Ngorongoro ambapo wananchi wameshikwa na magamba isipokuwa kata 1 ya Endulen baada ya Mb wa karatu mhe. Ntase kuweka kambi na kuisambaratisha ccm. Nakuomba kamanda Lema kama upo huu pls naomba upita hapa na kuwakomboa wananchi hawa mikokoni mwa magamba. Kwa taarifa nilizopata from wananchi ni kwamba wamekuwa wakinyanywa na kunyimwa haki yao ya kuishi baada ya shirika la NCAA kukataza kilimo cha kujikimu. CCM imejewekea mizizi ktk shirika hilo baada ya JK kumteua gamba-papa Msekwa kuwa M/kiti wa bodi wa shirika hilo. Cha ajabu ni kwamba wananchi wa eneo hilo hawana mwakilishi baada ya aliyekuwa waziri wa maliasili Mwangunga kumwondoa mbuge wa eneo hilo ktk bodi ya mamlaka hiyo pale walipotofautiana kuhusu mgogoro wa Loliondo wa wananchi kuchomewa maboma. Ndugu mwana Jf changia kidogo kuhusu hili tuwakomboe wananchi hawa ambao wamekuwa wakinyanyaswa na serikali ya ccm. "Ukombozi wa nchi hii umewadia" Karibuni
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom