Kamanda kova soma hii na hali iliendelea itabidi wananchi tuchukue hatua? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamanda kova soma hii na hali iliendelea itabidi wananchi tuchukue hatua?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by luckman, May 23, 2011.

 1. l

  luckman JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Napenda nitoe rai kwa mheshimiwa Kova kwa vitendo ambavyo vimekuwa vikifanywa na vibaka pale maeneo ya ubungo karibu na kituo mita chache kutoka ENGEN Kuelekea kituoni,

  Kumekuwepo na uvunjifu wa amani na vijana ambao wamejichukulia ajira isiyo halali ya kukwapua sitemirror za magari, simu na vito vya thamani vya watu, nishashuhudia mara nyingi na jana nimeona vibaka wengi sana amabao washaona ni utaratibu wa kawaida kukwapua na kutokomea kwenye fensi nyuma ya kituo cha daladala cha ubungo ambapo inaonekana ndo kuna store zao!watu watano jana wameibiwa tupo folen na defender ya polisi iko pale na wanaona,gari namb T368AHW alikwapuliwa simu na sitemirror zote mbili na hawakuweza kumsaidia!je polisi hawajiui hivi vitendo na mapango ya hao vibaka?kama polisi wanalipwa ili kulinda raia na mali zao je wannafanya kazi yao kwa ufasaha??au wanakula nao??kama jeshi la polisi wameshindwa kuwadhibiti semeni tuchue hatua ili sisi tunaliweza, mateja polisi wameshindwa kuwaondoa pamoja na wito wote uliotolewa,

  Mheshimiwa Kova, sisi hatuwezi kuendelea kuumia hali watu wanaofanya hivi vitendo wapo na wanajulikana wanaficha wapi hizo mali zetu,

  Naomba jeshi lako lifanye msako wa hao vibaka na watokomezwe, na hali hii sio ubungo tu hata sehemu nyingi haya mambo yanafanyika lakini hatuoni jitihada za makusudi kukomesha hali hii!hata ufisadi ulianza hivi kimchezo mwisho wa yote limekuwa gonjwa sugu ndani ya jamii ya kitanzania!

  naomba kuwakilisha
   
Loading...