Kamanda Kova: Kufuatia mahojiano na Dr. Slaa kesi mbili zimefunguliwa

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,796
12,239
Kamishina Kova amesema baada ya kumuhoji Dr. Slaa, polisi wamebaini kesi mbili ambazo tayari zimepelekwa mahakamani! Mashtaka hayo ni:
1. Njama za kutaka kudhuru maisha ya Dr. Slaa;

2. Utekaji na kumjeruhi mlinzi wa Dr. Slaa, Bw. Kagenzi.

============

1Bdj3pt

JESHI la Polsi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lipo katika hatua ya mwisho katika kukamilisha ushahidi ili kumfikikisha mahakamani Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa pamoja na makada wa Chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa Habari mda huu Jijini Dar es Salaam Kamishna wa Polisi Kanda maalum Dar es Salaam Suleimani Kova ametaja sababu ya kumfikisha mahakani katibu huyo wa Chadema na Makada wake inatokana na Vitendo vinavyodaiwa ni vya kinyama alivyofanyiwa mlinzi wake vya kumteka,kumpiga na kumlazimisha kutaja watu wanaomtuma kumuua Katibu mkuu wa Chadema.

Hivyo hivyo Jeshi hilo la Polisi limesema kwa sasa linawashikilia makada watatu wa Chama hicho kikuu cha upinzani nchini ambao ni Boniface Jacob miaka 32 mkazi wa ubungo kisiwani ambae pia ni diwani wa kata ya Ubungo kupitia chama hicho.

Sambamba na Hemed Ally Sabula miaka 48 mkazi wa Tandale kwa tumbo ambaye anadaiwa ni Afisa Usalama wa chama hicho Taifa.

Mbali na hao pia Kamishna Kova amemtaja Kada mwengine anayeshikiliwa kuwa ni Benson Mramba,miaka 30,mkazi Tabata Kisukulu ambaye ni Afisa Utawala wa Chadema.
Kamishna kova amebainisha kuwa Ushahidi wao utakapokamilika mafaili yao yatafikishwa kwa Wakili wa Serikali ili hatua zichukuliwe.

Aidha,Akizungumzia sakata la Mlinzi Kagenzi amesema kwa sasa wanamalizia kazi ya kukusanya ushahidi kutoka Chadema ambao wanamtuhumu bwana Kagenzi ambaye anafanya ushirikiano na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM bara Philip Mangula na Afisa Usalama wa Taifa Mkoa wa Kinondoni kwa kuaandaa mpango wa kutaka kumuwekea sumu Dokta Slaa.

Kesi hiyo kwa mala ya kwanza ilifika polisi tarehe 8 mwezi huu majira ya saa 11.jioni katika kituo cha Polisi cha Oysterbay kupitia kwa wakili wa Chadema anayetambulika kwa jina la john Malya akiambana na mtuhumiwa Khalid Kagenzi ambaye ni mkazi wa Tandale kwa tumbo ambapo Wakili huyo aliiambia polisi kwamba alimleta mtuhumiwa baada ya kuagizwa na Dokta Slaa ili kutoa malalamiko kwa niaba yake.

Ambapo Katika maelezo yake anadai Wakili huyo kuwa uongozi wa Chadema ulikuwa ulichukuwa hatua mbalimbali dhidi ya kugenzi ikiwemo kumbana na kujilidhisha kuwa nahusika na mipango ya kimauaji.

Kwa mujibu wa Kamishna kova anasema katika mahojiano wakabaini kunavitendo vya kinyama ambavyo mlinzi huyo wa Dokta Slaa amefanyiwa na Makada wa Chadema baada ya Jeshi hilo kumkuta akiwa na majeraha mbalimbali katika mwili wake.

Chanzo:Mtizamohuru
 
Haaa!!hapa kuna kazi, kwa hiyo kila upande kwa nafasi moja ni mlalamikaji na kwa nafasi nyingine ni mtuhumiwa.
 
Kamishina Kova amesema baada ya kumuhoji Dr. Slaa, polisi wamebaini kesi mbili ambazo tayari zimepelekwa mahakamani! Mashtaka hayo ni:
1. Njama za kutaka kudhuru maisha ya Dr. Slaa;
2. Utekaji na kumjeruhu mlinzi wa Dr. Slaa, Bw. Kagenzi.

Source: EA Radio.

Hapo kwa Utekaji wa kagezi kesi ilitakiwa isomeke,utekaji,kujeruhi na kutishia kumwua Kagenzi
 
Hahahaaaaa!! Majambazi wanapigwa then wanafunguliwa mashtaka...mbona wanaowapiga hawafunguliwi mashtaka? Sembuse huyu muuaji!?
 
ebwana nimesikia kuhusu njama za kutaka kumuua Dr.Slaa na hiyo ya kupigwa na kuteswa Kagenzi akiwa katika ofisi za chadema.
sasa nataka kujua kipindi kipigo hicho kinaendelea kagenzi alikuwa ashaondolewa nafasi ya bodigadi wa Dr.Slaa?
 
Ni sheria zaid kuliko, street justice!!

Hao waliompiga Kagenzi wametumia street justice na si sheria.Kisheria walitakiwa washauri aondolewe u-body guard na kama kuna kesi wakabidhi wanasheria wampeleke mahakamani.Namna walivyoshughulikia suala la Kagenzi unaona wazi kabisa kuwa hao ni mbumbumbu wa sheria na mambo ya ulinzi.Hawajui mambo ya kiulinzi wala ya kisheria.

Sasa kwa kutojua kwao wataumia bure kwenye hii kesi .Ushauri wangu mtu asikubali kushika nafasi kazi ya kitaalamu ambayo hajaisomea au kuijua.Ulinzi ni fani ya kusomea si ya kukurupuka na kuingia kienyeji ina mambo mengi.
 
Uko sahihi hizo zingine ni hisia tu kuwa alitarajia kuweka sumu sijui kwenye chai au uji lakini kumteka mtu na kumbonda ni kitu halisia.Hao waliombonda wana kesi mbichi kabisa ya kujibu tena nzito.
Yaani huwakujiuliza mbona hakuna viongozi katika hayo mahojiano "utekaji" wala mwanasheria yeyote wa chama??!!!
Wao wakajiona ndio "the chosen" sasa inakuwa habari ya mchumia janga. . . . . .
 
Hao waliompiga Kagenzi wametumia street justice na si sheria.Kisheria walitakiwa washauri aondolewe u-body guard na kama kuna kesi wakabidhi wanasheria wampeleke mahakamani.Namna walivyoshughulikia suala la Kagenzi unaona wazi kabisa kuwa hao ni mbumbumbu wa sheria na mambo ya ulinzi.Hawajui mambo ya kiulinzi wala ya kisheria.

We unadharau "intelijensia" sio??!!
 
Back
Top Bottom