Kamanda Kova anahusika kwa 100% uchomaji makanisa Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamanda Kova anahusika kwa 100% uchomaji makanisa Dar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nguvu ya Hoja, Oct 28, 2012.

 1. Nguvu ya Hoja

  Nguvu ya Hoja JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Jumapili hii nimekamilisha utafiti wangu wa awali kuhusu vurugu zilizotokea Mbagala hadi kufikia hatua ya kuvamia kituo cha polisi na hatimaye kuvunja makanisa,kuiba na kuchoma baadhi ya maknisa. Kwa vile nimeshirikiana na taasisi moja isiyo ya kiserikali na bado wanaendelea na utafiti wao ikiwa ni pamoja na kukusanya cd zote zenye maneno ya uchochezi,kwa upande wangu nimeishia kwenye utafiti wa awali ambao ulihusisha mahojiano na watu walioshuhudia tukio hilo,pamoja na kutembelea makanisa yote yaliyoathirika, na kuhojiana na wazazi wa watoto waliobishania kuran na majirani zao.

  Ni mambo mengi sana tumekutana nayo na ni mengi zaidi yatajitokeza ila kwa leo niongelee mawili tu. Moja ni kuhusika moja kwa moja kwa kamanda Kova,yeye alitaarifiwa mapema juu ya tukio hilo na uvamizi wa makanisa ila alichofanya akaongozana na wanasiasa kuuza sura kwenye TV,akitoka studio moja kwenda nyingine akiwahadaa wananchi kuwa hali ni shwari na kwa njia hiyo aliwahamasisha wahalifu ambao walikwisha iba vitu na kuvunja makanisa kurudi kuyachoma moto.

  Hakufika kabisa eneo la tukio hadi alipofika Kikwete saa 48 baaada ya tukio. Na hata alipopigiwa simu asbuhi ya saa 4 alikanusha vikali kuwa hakuna kanisa lililochomwa moto. Je kulikuwa na umuhimu wa kushindwa kufika kwenye eneo la tukio? Na badala yake anawahamasisha wahalifu kuwa hali ni shwari? Kwenye sakata hili vituko vya Kova ni vingi sana ila tuishie hapo kwa leo mengi mtayasikia baadaye.

  Jambo la pili tulilogundua ni kwamba hakuna hata mmoja aliyeshuhudia koran ikikojolewa,tulichoambiwa na kuthibitishwa na baba mzazi wa mlalamilkaji (aliyekuwa na koran) ni ubishi na maneno kuwa "naweza hata kuikojolea" na aliitemea mate.Tuliwatafuta hata watoto waliokuwepo na wote tulioongea nao hakuna aliyeona hicho kinachoitwa mkojo ila wao wanasema baada ya kuitemea mate walimchapa akakimbia.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huwa najiuliza sana Kova aliteuliwa kwa vigezo gani?
   
 3. Mwana Mtoka Pabaya

  Mwana Mtoka Pabaya JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 11,763
  Likes Received: 8,037
  Trophy Points: 280
  Kamanda aliyekomesha ujambazi mbeya
   
 4. m

  mdunya JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 765
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Eeeh! Ngoja nilale huku natafakari.
   
 5. Mzee Msemakweli

  Mzee Msemakweli Senior Member

  #5
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 159
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kigezo kikubwa ni Mwislam mwenzetu na si vinginevyo

   
 6. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #6
  Oct 28, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kanisa ndio takataka zipi mpaka zichomwe?
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Oct 28, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kova anapenda shirikisha media kila alifanyalo ndo maana akukwaa huo ukamanda ila kumbuka ata Mwema nae alipitia mbeya so MBY ina nyota kwa makamanda kupaa!
  but kumbuka pia ni mwenzetu
   
 8. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #8
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Ndo mana mkisha kojolewa mnakimbilia kuandamana...
   
 9. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #9
  Oct 28, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 180
  you shall know the trueth, and the trueth shall set you free
   
 10. Advicer

  Advicer JF-Expert Member

  #10
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 429
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  chukia like yangu mkuu
   
 11. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2012
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kova Msanii toka siku nyingi sana hata SILAHA amabzo huita waandishi wa habari akawaonyesha kuwa amezikamata katika opersheni maalum ni uongo mtupu.
   
 12. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  huyu kova nayeye pia inatakiwa apelekwe the heaque
   
 13. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Ndio hasara ya kuachia watu kujiteulia watendaji wa ngazi ya juu watakavyo. Huyu bwana sijui hata kiwango cha elimu yake ni kipi? The way anavyopenda sifa na kuuza sura runingani badala ya kupiga kazi kueleza ukweli wa mmbo yeye anaendekeza projo inashangaza sana!!.......:pop2:
   
 14. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,144
  Likes Received: 2,178
  Trophy Points: 280
  Watu wengi wenye makengeza ni waongo sana... fanya utafiti utanielewa
   
 15. C

  Concious Senior Member

  #15
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 105
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  simply bcoz ni muislam
   
 16. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  [FONT=&quot]CHRISTIAN MISSION FELLOWSHIP[/FONT]
  [FONT=&quot]P.[/FONT][FONT=&quot]O. Box 55024 Dar Es Salaam Tanzania, E-mail:[/FONT][FONT=&quot]info@cmftz.org[/FONT][FONT=&quot], website: [/FONT][FONT=&quot]www.cmftz.org[/FONT][FONT=&quot][/FONT]​
  [FONT=&quot] Tel: 0715200551, 0755200550 : Tarehe 28/10/2012[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]MAOMBI YA KUHAMASISHA AMANI NCHINI[/FONT]
  [FONT=&quot]Neno la Mungu limetuagiza katika 1Timotheo 2:1-2; kuwa, kabla ya mambo yote nataka DUA, SALA, MAOMBEZI NA SHUKURANI vifanyike kwa watu wote; kwaajili ya Wafalme na wenye mamlaka, tuishi kwa utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Tukiwa Kanisa la Mungu, tumechukua hatua hii ya kuanza kuliombea Taifa kwa kuugua mno ili Amani tuliyopewa na Mungu na kuenziwa na waasisi wa Taifa hili iweze kudumishwa.[/FONT] [FONT=&quot]Ndugu zangu Watanzania sote tufahamu kuwa, msimamo tuliyojiwekea katika Katiba yetu ya Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, ni kupiga marufuku kila namna ya ubaguzi ukiwemo wa kijinsia, rangi na kidini. Katiba Ya 1977 Ibara 13(5).[/FONT] [FONT=&quot]Kwa upande wa madhehebu ya Dini Tanzania tuna dini kubwa tatu na nyingine ndogondogo; Dini kubwa ni Ukristo, Uislamu na Dini za Kijadi. Wakristo na waislamu tumekuwa tukishirikiana pamoja katika misiba, sherehe mbalimbali, kuoleana, kuishi katika Nyumba moja na kufanya shughuli za Kijamii kwa pamoja bila kubaguana kabla na baada ya miaka hamsini (50) ya uhuru Nchi yetu. [/FONT][FONT=&quot][/FONT] [FONT=&quot]Ndugu zangu wakristo na watanzania wezangu kwa ujumla napenda kuwafahamisha kuwa, hakuna nchi yeyote katika bara la Afrika yenye idadi kubwa ya wakristo na waislam wanao ishi kwa amani na upendo kama Tanzania.Ila kwa sasa watu wasioitakia amani Nchi yetu wanataka kupenyeza chuki za kidini ili isiwe nchi ya amani bali vurugu.[/FONT] [FONT=&quot]Hivi karibuni, tumeshuhudia kuwepo kwa vitendo vinavyoashiria ubaguzi wa kidini kwa baadhi ya vikundi toka makundi ya dini kubwa kudai haki zao ambazo kimsingi wanaona wanastahili kuwa nazo sawa na Dini nyingine. Hali hii imefanya vikundi hivi vitumie vyombo vya habari; Mathalani: Redio, Magazeti na Machapisho mbalimbali kueleza hisia zao kwa Jamii, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa mgawanyiko katika Jamii iliyokuwa imeshikamana. Aidha, mgawanyiko huu unazidi kukua na kusababisha hali ya Chuki kwa mamlaka ya Nchi, na hatimaye Dini moja na nyingine. [/FONT] [FONT=&quot]Baada yakufanya utafiti wa kina kwanini kuwe na Chuki baina ya makundi ya Dini na Serikali tumeona kuwa, makundi haya ya Dini yanaiona serikali inawanyima haki zao na inapendelea Dini moja na hivyo kutumia mfumo wake katika utawala. Hata hivyo, Madai ya kundi hili yanawapelekea kuwafanyia Vurugu waumini wa kundi wanalosadiki kuwa linapendelewa na Serikali, jambo ambalo linawafanya (wanaofanyiwa vurugu) wasitumie uhuru wao wakufanya ibada ambao kimsingi wamepewa Mungu na kuandikwa katika Katiba ya Nchi Yetu.[/FONT] [FONT=&quot] [/FONT][FONT=&quot]Tukiwa Kanisa la Mungu, hali hii inatupelekea kuona kuwa bado serikali yetu haijawajibika ipasavyo katika kuelekeza sera na shughuli zake kwa lengo la kuhakikisha kuwa sheria za Nchi zinalindwa na kutekelezwa. Kimsingi, haki na uhuru wa watu wengine au maslahi ya umma vinapaswa kutoathiriwa kabisa na matumizi mabaya ya uhuru wa haki za watu binafsi. [/FONT] [FONT=&quot] Hivyo, Kanisa baada ya Kumlilia Mungu kwa machozi na maombi mengi, tumeamua kuchukua mwelekeo wa uwajibikaji usio wa maneno tu; kwani suala la kutoa matamko ya kulaani limefanywa na Dini na Serikali kwa mkazo mkubwa. Kwa upande wa Serikali, watawala wa Nchi yetu wamekuwa wakilaani na kukemea, ubaguzi wa Dini, rushwa na ufisadi katika Taifa hili bila mafanikio na hata leo tunawaona vijana wanatwangana hadharani kutokana na kushamili kwa rushwa ,hii yote ni kwa sababu hii ni vita ya kiroho na inapaswa kukemewa na viongozi wa dini na watawala wanapaswa kuchukua hatua. Kwa jinsi hii, Kanisa limelitazama jambo hili kiroho zaidi kwa kutambua kuwa chuki na rushwa ni roho kamili inayotoka kwa Shetani; hivyo watu wa kiroho tunalo jukumu la kuziopinga hila za Shetani kwa DUA, SALA NA MAOMBI ili kuleta amani ya kudumu katika Taifa letu, ambalo linasifika kuwa ndiyo kitovu cha amani Afrika na Duniani. Ndugu zangu wakristo na viongozi wa dini; ikumbukwe na izingatiwe kuwa nyumba za ibada ni sehemu ya kumwabudu Mungu, hivyo zitumike kuhubiri dini tuliyo amuriwa na Mungu na sio siasa, na pasiwe mahali pa kuandaa na kuchochea vurugu na chuki miongoni mwetu. Viongozi wa dini wanaaminiwa sana na waumini wao na lolote watakalo waambia waumini, huaminiwa kuwa limetoka kwa Mungu. [/FONT] [FONT=&quot]Aidha tukumbuke kuwa, tunafanya kila kitu vizuri zikiwemo ibada zetu kwasababu ya amani tuliyonayo. Amani isipokuwepo hakuna kitu kinaweza kufanyika katika Nchi; iwe kwa waumini na wasio wauimini, iwe kwa maskini au matajiri. Amani ikishaondoka, matajiri au wenye pesa watakimbia na kuwa wakimbizi wa Nchi zingine, huku masikini wakikosa mahali pa kwenda na kuishia kuuawa na kupoteza maisha. Kawahiyo ni vema kuitunza amani yetu na kuilinda; kamwe tusiichezee amani tuliyonayo katika nchi yetu; hii ni tunu tuliyopewa na Mungu na kuachiwa na waasisi wa Nchi yetu ili tuienzi, hivyo kila mmoja wetu ni mdau wa amani. Mkulima anahitaji amani ili aweze kupata mazao shambani mwake; daktari anahitataji amani ili afanye kazi zake vema Hospitalini, kadhalika mfanya biashara na mwanasiasa wote wanahitahi amani.[/FONT] [FONT=&quot]Nichukue fursa hii kumpongeza Kamanda Suleiman Kova kwa juhudi zake za kuifanya Dar-es-salaam iendelee kuwa bandari ya Amani; Kamanda Kova ameonyesha ushupavu na umadhubuti mkubwa katika kauli zake, kwani mchango wake umeleta heshima iliyotukuka katika vyombo vya dola nchini na kwa watanzania wote. Kanisa la Mungu ambao tumeitwa kw[/FONT][FONT=&quot]a Jina la BWANA, leo hii tunaomba na kuutafuta Uso[/FONT][FONT=&quot] wa BWANA tukiwakilisha zaidi ya makabila 120 ya Tanzania kwa Kutumia Lugha Zetu za Makabila kama alama ya Umoja na mshikamano wetu, tukimsihi Mungu aiponye Nchi yetu. Tunaitakia Nchi yetu amani na Utulivu, katika Jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, Amini.[/FONT]
  [FONT=&quot]NDIMI NDUGU YENU KATIKA KRISTO YESU [/FONT]​
  [FONT=&quot]……………………………………………….[/FONT]​
  [FONT=&quot] ASKOFU MKUU DKT. MGULU KILIMBA .[/FONT]
   
 17. E

  Etairo JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huu ndo utafiti? Pole saana kwa kuelemea mrengo wa kanisa kwa imani yako.
  Kova kuwepo kwenye tukio si lazima kwani anawanaomwakilisha na kumpa taarifa
  Kuwa hakna aliyethibitisha Kur'an kukojelewa bali kutemewe na kuchapwa bakola kwa mhusika-nani aliyemchapa? watoto wenzake au watu wazima? Utafiti wako ni butu na haina mashiko. Je uliona kanisa lililochomwa moto? Au uliona liliobomolewa vii na kisha baadhi ya vitu ndani ya makanisa kuunguzwa na unaowahita wauni? Kuwa huru kwenye moyo kabla ya kuandika mawazo yako ambayo kiwazi kabisa yanaonesha wewe unatatizo na kova -si utafiti huo. Rejea shule ukafundishwe utafiti unavyofanywa.

  Haya kova umeyasikia hayo? Jifanye mwenzao vipi bado wewe ni selemani tu. hawatakuwa radhi nawe hata ujipendekeze vipi. Yaliyo moyoni mwao ni makubwa zaidi kuliko yanayobainishwa na ndimi zao.:becky:
   
 18. A

  Ampex1 New Member

  #18
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Una uhakika na ulisemalo ndugu!!!!!
   
 19. Vijisenti

  Vijisenti JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Mkuu lazima utakuwa muislamu tu, sijawahi kuona hoja zenye akili
  zikiandikwa na asiyekuwa muislamu katika sakata hili humu jukwaani.
   
 20. HUGO CHAVES

  HUGO CHAVES JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 1,852
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Mmi ninachokiona hapo ni uzembe uliosababishwa na kova ,baada ya kupokea taarifa hakwenda kwenye tukio alienda studio kutoa matamko kitu hiki angeweza kutoa tamko hata akiwa eneo la tukio ,pili kumhusisha moja kwa moja inawezekana ama alijua kinachoendelea ama vinginevyo ila bado hatujachelewa kumuadhibu kwa hilo
   
Loading...