Kamanda Kenyela:Aliejeruhiwa haijulikani amejeruhiwa na nini huenda ikawa Jiwe ,Risasi etc.

Jana wakati akihojiwa na waandishi wa habari alikua anajichanganya na kutoa maelezo yasiyo na kichwa wala miguu."....Kijana mmoja amejeruhiwa(hakutaja kitu kilichopelekea jeraha) maeneo ya shavuni, na jopo la madaktari hospitali ya Mwananyamala wanahangaika kuhakikisha wanamtibu..."
 
....Akihojiwa kwa njia ya simu kamanda Kenyela amesema kijana aliejeruhiwa amejeruhiwa kwa subject Matter..huenda ikawa Jiwe,Risas au bomu la machozi...
Na mjeruhiwa yupo hoi wodini.
Amesema Police walitumia hekima sana la sivyo Mauaji yangekuwa Makubwa.

Source:Radio One

....Pumbavu sana hilo li-polisisiem. Nimelisikia hata mie likisema eti walitumia hekima kubwa na na njia za kistaarabu kushughulikia hilo tatizo. Busara gani wametumia kama sio ushuzi tu na kumwaga damu buree...
 
DOkta anasema ... kajeruhiwa vibaya sana kwenye paji la uso na meno mengine yametoa... kamanda anasema amejeruhiwa shavu!????
 
Kwa nguvu hizi zinazokuwa zinatumika kila mara Polisi wanatofauatina na raia, kiasi cha kusababisha mauaji na vilema, ina maana uhusiano wa raia na polisi itafika mahali uwe kama wa panya na paka. Kuna baadhi ya familia ambazo hazitapenda watoto wao kujiunga na kazi ya jeshi la polisi. Ikifikia hapo, kazi ya polisi itakuwa ngunu zaidi maana dhana ya polisi jamii haitafanya kazi. Mimi nikimwona polisi yeyote, huwa nawaza kuhusu kitu kizito, butu au chenye ncha kali.
 
......huenda ikawa Jiwe,Risas au bomu la machozi...

Huu utetezi wa Kenyella ndio mtaala mpya wa Police au imekuwa ikitokea coincidence tu? Ilianzia kwa Shilogile wa Morogoro, ikaendelea kwa Kamuhanda wa Iringa na sasa imejirudia kwa Kenyella wa Kinondoni!

Amesema Police walitumia hekima sana la sivyo Mauaji yangekuwa Makubwa

Huu ndio ujumbe mahsusi kwa wananchi toka jeshi la polisi kwamba, sasa ni mwendo wa kuua tu hakuna kingine, ndio maana wanalenga risasi za kichwani, kifuani na tumboni, kinyume na mafunzo ya polisi tunayoyafahamu ambayo yanaelekeza mahali pa kulenga risasi wakati askari polisi anapokabiliana na watu wanaofanya vurugu.

Na kwakuwa hapa kwetu polisi siku zote wanatumia risasi za moto kukabiliana na wananchi hata wanapokuwa wanaandamana kwa amani, huu ni ushahidi mwingine kwamba jeshi la polisi nchini limedhamiria kuwaua wananchi hadi liwamalize.
 
Hapo ndiyo ninaposhangaa,..lakini ninashindwa kuelewa tatizo liko wapi, wanaotoa majibu mepesi(rahisi/yasiyo na mantiki) au wale wanaoyapokea na KUYAKUBALI!!

Ki ukweli wananchi tunadanganywa sana na wepesi wa kusahau.
na WANAHABARI WETU nina wasiwasi na weledi wao kwa kuwa
wanachokiripoti kutoka field na utakachokikuta kwenye vyombo vya habari
esp.magazeti ni tofauti sana sijui wanahong.wa au ni uoga ..................
uko kwenye eneo la tukio umeona mtu kapigwa risasi kesho inaaandikwa kitu chenye ncha kali......................loh!!!
 
Kwa nguvu hizi zinazokuwa zinatumika kila mara Polisi wanatofauatina na raia, kiasi cha kusababisha mauaji na vilema, ina maana uhusiano wa raia na polisi itafika mahali uwe kama wa panya na paka. Kuna baadhi ya familia ambazo hazitapenda watoto wao kujiunga na kazi ya jeshi la polisi. Ikifikia hapo, kazi ya polisi itakuwa ngunu zaidi maana dhana ya polisi jamii haitafanya kazi. Mimi nikimwona polisi yeyote, huwa nawaza kuhusu kitu kizito, butu au chenye ncha kali.

Mimi jamaa zangu wote ambao ni mapolisi nimeshaamua kukaa nao mbali kabisa. Sasahivi sitaki urafiki nao kabisa tunakutana na kushirikiana nao yale mambo ya lazima tu, kama misiba na sherehe si zaidi ya hapo.
 
Hivi huyu kamanda alizaliwa kwa njia ya kawaida au kwa kupitia
tigo.jpg
....Akihojiwa kwa njia ya simu kamanda Kenyela amesema kijana aliejeruhiwa amejeruhiwa kwa subject Matter..huenda ikawa Jiwe,Risas au bomu la machozi...
Na mjeruhiwa yupo hoi wodini.
Amesema Police walitumia hekima sana la sivyo Mauaji yangekuwa Makubwa.

Source:Radio One
 
Hapo ndiyo ninaposhangaa,..lakini ninashindwa kuelewa tatizo liko wapi, wanaotoa majibu mepesi(rahisi/yasiyo na mantiki) au wale wanaoyapokea na KUYAKUBALI!!

Mkuu hippocratessocrates, hakuna mtu mwenye akili anayakubali hayo maelezo na majibu, ni kwa vile watu hawana la kufanya wanatulia tu. Lakini, uhusiano baina ya jamii na hilo jeshi unazidi kuwa mbaya. Kama huamini, mwambie polisi aje aombe lift kwenye Vitz yangu akiwa amevaa sare.
 
Haha..mkuu, hawezi kusogelea vitz yako, hata hivyo hii ni kwako tu(mtu mmoja), ila iwapo tungeungana tunaweza kufanya kitu.

Sidhani, kama watanzania hawana njia yeyote ile sehemu ya kufanya(out of options), ..
1.Maoni ya Katiba(kwani hili ni moja kati ya mengi)
2. Maandamano ya amani(kwa lengi moha tu la kupinga udhalimu)
3.Agency husika kushitaki na KUSIMAMIA HADI MWISHO kwa waonewa/wadhulumiwa/wanyanyaswaji.
4.Katika Chaguzi kuweka watu wenye uadilifu, wasio na maslahi yao n.k
 
Back
Top Bottom