Kamanda Freeman Mbowe kusimamia changisho la M4C leo serena hotel...

Status
Not open for further replies.

only83

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
5,343
2,525
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe, leo anatarajia kuongoza harambee ya kukusanya fedha kwa ajili ya kufanikisha mkakati wa vuguvugu la mabadiliko (M4C) katika jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam, mjumbe wa Kamati Kuu na aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, alisema harambee hiyo itafanyika kuanzia majira ya saa 1:00 usiku katika Hoteli ya Serena kwa lengo la kuwakutanisha wanamabadiliko wa daraja la kati.

Alisema katika harakati za vuguvugu la mabadiliko wana lengo la kukusanya kiasi cha shilingi bilioni tano kwa upande wa Dar es Salaam, wanatakiwa kukusanya asilimia kumi ya fedha hizo.

"Tulienda Mwanza pamoja na mwenyekiti na tulifanya hivyo, kuna dalili za mafanikio makubwa na kama watu watakuwa makini, basi kutakuwa na mafanikio na lengo la fedha hizo ni kununulia magari kwa ajili ya kuendesha kampeni nchi nzima," alisema Lema.

Naye Mwenyekiti wa M4C mkoa wa Dar es Salaam, Alex Mayunga, alisema wameandaa chakula cha jioni ambapo watu 500 kutoka katika kada tofauti tofauti, wamealikwa.

Alisema lengo lingine ni kukusanya rasilimali watu, fedha na vifaa vya kazi kwa lengo la kueneza chama katika vitongoji na mitaa ambako ndiko kunakoakisi maisha halizi ya Watanzania.

Alitaja lengo lingine kuwa ni kuweka mkakati wa kuendeleza mshikamano na umoja miongoni mwa wana-mabadiliko wa daraja la kati ili kutoa mchango kwa mabadiliko ya katika jamii.

Alisema, wanahakikisha chama kinakusanya rasilimali fedha kwa lengo la kununua vitendea kazi kulipa gharama za kupata rasilimali kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu mwaka 2015.

SOURCE : Tanzania Daima
 
Kwanini isiwe live on tv ili kaujumbe flani kawafikie wananchi wote?
 
Kwanini isiwe live on tv ili kaujumbe flani kawafikie wananchi wote?

lakini TV nyingi kwa bongo hazipo huru je zitakubari kurusha??

Nasikia TBC na ITV wamekatazwa kabisa kujihusisha na matangazo ya Chadema. Bosi Mkuu wa TBC inasemekana katishiwa kwamba amuulize Tido Muhando nini kilimfanya aondoke Tbc na ITV kwa upande wao wametishiwa kwamba watakuwa wamejiingiza katika vita na Serikali lazima wao watashindwa na inasemekana vitisho vyote hivi vinafanywa Orally
 
only83
Acha kupotosha lengo la harambee hiyo. Tunajua kuwa harambee hiyo inahusu kuandaa mapokezi ya ULIMBOKA ikiwa ni pamoja na kuchangia utengenezaji wa kanda yenye upotoshaji kuwa Serikali ndiyo iliyohusika na Utekaji.
 
Last edited by a moderator:
Acha kupotosha lengo la harambee hiyo. Tunajua kuwa harambee hiyo inahusu kuandaa mapokezi ya ULIMBOKA ikiwa ni pamoja na kuchangia utengenezaji wa kanda yenye upotoshaji kuwa Serikali ndiyo iliyohusika na Utekaji.

Akili kama hizi ni hatari kwa ustawi wa nchi yetu...hata hivyo, kwani kumpokea Ulimboka ni vibaya? au kuandaa film kuonyesha ushenzi wa serikali ni vibaya? Acha kuleta hoja zako matope hapa.
 
Hasa kuwaamsha watu waliolala for more than 50yrs si mchezo!!!!

Wadanganyeni wale wanaowachangia fedha kwa ajili ya kushibisha matumbo yenu bwana. Matumizi mabaya ya fedha za chama, Ukabila na sera kandamizi ndiyo moyo walio nao?
 
Akili kama hizi ni hatari kwa ustawi wa nchi yetu...hata hivyo, kwani kumpokea Ulimboka ni vibaya? au kuandaa film kuonyesha ushenzi wa serikali ni vibaya? Acha kuleta hoja zako matope hapa.
Yaani film ndo ziratibiwe na Wanaharakati, SAID KUBENEA na REGINARLD MENGI? nini kimejificha nyuma ya pazia? kwa nini wale waliokuwa wakiizushia Serikali kuwa ndiyo imehusika ndiyo hao hao wanaoandaa film hiyo na mapokezi ya Ulimboka? Watanzania wenzangu nadhani tuna jambo la kujifunza hapa. CDM si chama cha Siasa, Hellen Kijo Bisima siyo mkurugenzi wa Kutuo cha haki za binadamu, Ananilea Nkya siyo Mwenyekiti wa TAWLA. Hao ni hatari sana kwa mshikamano, amani na utulivu wa Taifa letu. Lazima tujifunge vibwebwe kuhakikisha hatuliingizi taifa katika machafuko kwa sababu tu ya uchu wa madaraka, wivu wa kishenzi na Ukabila ulioota mizizi. 2015 bila ZITTO, CDM ifie mbali huko.
 
Acha kupotosha lengo la harambee hiyo. Tunajua kuwa harambee hiyo inahusu kuandaa mapokezi ya ULIMBOKA ikiwa ni pamoja na kuchangia utengenezaji wa kanda yenye upotoshaji kuwa Serikali ndiyo iliyohusika na Utekaji.

Habari yako!
Umeamka salama?
Nawe unajihisi ni mmoja wa wanafamilia ya The Great Thinker?!
Kaomba ukurasa katika gazeti la Uhuru , Mzalendo ama hata Sauti Huru ukaendeleze upuuzi wako kwa uhuru zaidi.
 
lakini TV nyingi kwa bongo hazipo huru je zitakubari kurusha??

Pumba tupu, Reginald Mengi Chadema damu, halafu ITV imekatazwa kutangaza habari za CDM, Ufo Saro wa ITV alishakiri yeye ni CDM damu iweje asitangaze habari za CDM?
 
Habari yako!
Umeamka salama?
Nawe unajihisi ni mmoja wa wanafamilia ya The Great Thinker?!
Kaomba ukurasa katika gazeti la Uhuru , Mzalendo ama hata Sauti Huru ukaendeleze upuuzi wako kwa uhuru zaidi.
Mod fungia huyu analeta ukabila humu JF.
 
Habari yako!
Umeamka salama?
Nawe unajihisi ni mmoja wa wanafamilia ya The Great Thinker?!
Kaomba ukurasa katika gazeti la Uhuru , Mzalendo ama hata Sauti Huru ukaendeleze upuuzi wako kwa uhuru zaidi.

Hivi kweli wewe unajiona unafaa kuitwa great Thinker? au wewe ni Mshumbuzi nini?
 
Yaani film ndo ziratibiwe na Wanaharakati, SAID KUBENEA na REGINARLD MENGI? nini kimejificha nyuma ya pazia? kwa nini wale waliokuwa wakiizushia Serikali kuwa ndiyo imehusika ndiyo hao hao wanaoandaa film hiyo na mapokezi ya Ulimboka? Watanzania wenzangu nadhani tuna jambo la kujifunza hapa. CDM si chama cha Siasa, Hellen Kijo Bisima siyo mkurugenzi wa Kutuo cha haki za binadamu, Ananilea Nkya siyo Mwenyekiti wa TAWLA. Hao ni hatari sana kwa mshikamano, amani na utulivu wa Taifa letu. Lazima tujifunge vibwebwe kuhakikisha hatuliingizi taifa katika machafuko kwa sababu tu ya uchu wa madaraka, wivu wa kishenzi na Ukabila ulioota mizizi. 2015 bila ZITTO, CDM ifie mbali huko.

Sibishani na mgonjwa..endelea na hoja zako za kipuuzi.
 
Pumba tupu, Reginald Mengi Chadema damu, halafu ITV imekatazwa kutangaza habari za CDM, Ufo Saro wa ITV alishakiri yeye ni CDM damu iweje asitangaze habari za CDM?

@kumbe uwezo wako wa kufikiri bado upo vile vile? Reginald Mengi ni Mwanachama hai wa CCM na alishawahi kukiri, pia Ufo saro siyo ITV
 
Ni wazo zuri sana lakini kurusha kwenye TV napo ni grama kubwa sana...wajitahidi hata radio station ya maana irushe...
Siyo gharama , inadhaminiwa na wakubwa(Reginald mengi, Hellen Kijo Bisimba , Ananilea Nkya na Said Kubenea). Leo kuna kikao kule Serena Hoteli kwa ajili hiyo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom