Kamanda Chagonja amtisha na kumkejeli Dr. Ulimboka

Ni dalili za mwisho mwisho serikali kuanguka.
Mauaji, utekaji, utesaji ni viashiria vya serikal iliyoshindwa na hivyo kufanya hayo kutisha kama mbinu ya mwisho kubakia madarakan.
Historia inatufundisha wazi, Id amin, ghadafi, Obote, saddam, gbagbn nk waliitumia mbinu hii sasa wako wapi?
 
Hata kama ikitokea ni ukweli kwamba Dr. Ulimboka alifumaniwa na mke wa mtu lakini ukweli unabaki pale pale kwamba miongoni mwa watu waliomteka na kumtesa, alimtambua ACP Msangi.
Kwahiyo hapo ndipo tunapoanzia, tayari mtekaji na mtesaji ameshatambulika na kujulikana, kwahiyo Chagonja hana pa kutokea katika hili.
 
Kama anaona Dr.Uli kakosea kumtaja huyo, basi atutajie yeye. Maana inaelekea yeye anawajua vizuri kuliko muhusika aliyetendewa maovu haya yakutisha na yasiyoelezeka
 
Kamanda wa Operesheni maalum Paul Chagonja amemtisha Dr Ulimboka Stephen kwamba kauli zake juu ya kumtambua ACP Msangi kwamba alihusika kumteka zitamgharimu mwenyewe.

Kamanda Chagonja amesema hakuna hata mtu mmoja anayejua ni nani alimteka na kumpiga Dr Ulimboka na ndiyo maana tume maalum inafanya uchunguzi.

Katika kejeli na kiburi cha hali ya juu Kamishna Chagonja alihoji mbele ya waandishi ''NANI ANA UHAKIKA JE KAMA ALIKAMATWA NA MKE WA MTU NDIYO AKAPIGWA?''

Source: Mtanzania Jumamosi

: Mtanzania Jumamosi[/QUOTE]

1. Kamanda ameonyesha ufinyu wa kufikiri na hata kutafakari ... !! Dr Ully awe na kipi cha zaidi cha kumgharimu kumgharimu zaidi ya hicho kilichomfika? Amabcho hakimtisha kwani amejitolea kwa hali na mali kwa ukweli hata kama ikiwa kifo. Yeye kamanda ndio atadhmini kuwa ... anagojwa na hicho hicho kilichomtokea Dr ...awa tayari na wala asitie shaka kwani ..muda si mrefu atakuwa hapo and beyond!! Nothing is for free ..ok!?

2. Hakuna hata mtu mmoja anayejua aliyemteaka well ...Yeye Kamanda sio Mtu ...Nataka tumtambue kuwa ni mnyama? Kama yeye ni mtu ...then anaweza kuwa huyo mtu mmoja anyemtaja kwani ... ndio yeye...!! Ikiwa na maana lazima awe kwenye hilo tukio ili ...Kuweza kutuhakikishia kuwa ni kweli alikuwepo yeye peke yake . Na kama alikuwepo ..Basi ni Mtuhumiwa namba moja ...Kwa kuwa ni yeye peke yake aliyekuwepo.

3. Kama inawezekana kuwa kuna uwezekano wa kuwa mke wa mtu ...huo ni uwezekano tu ..na ni kweli inawezekana kuwa hivyo. Lakini hata kuwa Ni Msangi ..pia inawezekana kuwa ndio hivyo. Kwa nini anaondoa uwezekano wa Kuwa Msangi ndiye chanzo. Na pia ianwezekana ikiwa ..ni chanzo kingine nk! Yeye nini kinamsukuma kushikilia uwezekano wa Mke wa mtu na usiwe uwezekano mwingine ...!! Yeye kama Mwenye fani ..Ni aiubu kushikilia uwezekano mmoja wakati inawezekana kuwa na uwezekano hata milioni moji..! Hapo ndipo angeoyesha kuwa ..uchunguzi unahitajika!! Lakini kuropoka tu ...Ni ishara kuwa ... Anamsukumo anaukwepa na kuulazimishia ...na likely ni kuwa ni Msangi anahusika!!!
 
"If you only have a hammer, you tend to see every problem as a nail. Abraham Maslow". Kumbe hili halina ubishi. Kuwafunga madokta wote hao kwa sababu ya mgomo, lazima uwe na maguvu sana maana utatengeneza tatizo kubwa kuliko lile la kuyumba kwa uchumi baada ya vita vya Kagera
Ndahani you said it well my bro. kuna kitu ambacho watu wengi hasa watawala wanakisahau, siyo mara zote nguvu inweza kushawishi jambo hata kama ni baya sana. wakati mwingine ni busara tu ya ukweli na ya uwajibikaji. sasa wakisema mathalani wanawashtaki wanategemea nini yatakuwa matokeo? je serikali imesahau kuwa bado inaupungufu mkubwasana wa madaktari and wasipokuwa makini basi watatorokea nchi jirani. tunawaona wanaokwenda kufanya kazi botswana, nchi za magharibi kama uswis na south africa. so naona possibility ka kupoteza hawa watu na serikali ianze tena kufikiei namna ya kupata wengine
 
Last edited by a moderator:
Kamanda wa Operesheni maalum Paul Chagonja amemtisha Dr Ulimboka Stephen kwamba kauli zake juu ya kumtambua ACP Msangi kwamba alihusika kumteka zitamgharimu mwenyewe.

Kamanda Chagonja amesema hakuna hata mtu mmoja anayejua ni nani alimteka na kumpiga Dr Ulimboka na ndiyo maana tume maalum inafanya uchunguzi.

Katika kejeli na kiburi cha hali ya juu Kamishna Chagonja alihoji mbele ya waandishi ''NANI ANA UHAKIKA JE KAMA ALIKAMATWA NA MKE WA MTU NDIYO AKAPIGWA?''

Source: Mtanzania Jumamosi
.

Hapo kwenye Red watuhumiwa wanazidi kuongezeka......Ulimboka kamtambua Msangi kwa sura kuwa ni mmoja wa watekaji na watesi wake. mimi nimemtambua Chagonja kuwa yeye na Msangi walikuwepo katika tukio hilo kwa kauli zake.

Chagonja ana uhakika kuwa wakati wanamteka Ulimboka walikuwa wamefunika nyuso zao, na waliendelea kufunika nyuso zao kipindi wanamtesa na ni yeye Changonja aliyefunua mask yake baada ya kuwa na uhakika kuwa walishamuua Dr. Ulimboka ana uhakika kuwa si Msangi aliyefunua Mask katika mazingira yale, au anajisikia vibaya Msangi kutambuliwa kwa kuwa labda ni Msangi aliyekataa wazo la kummaliza Dr. Ulimboka kwa risasi kwa hoja kuwa kwa kufanya hivyo ni rahisi tukio hilo kuacha alama zikiongoza wafuatiliaji hadi ndani ya jeshi la Polisi kwa kuwa hawakuwa na silaha tofauti na za jeshi la Polisi, hivyo kwa ushauri wa Msangi wakaamua 'kumuua' kwa kumpiga na gongo zito kichwani, hali iliyopelekea kupoteza fahamu na moyo wake labda kusimama na walipomkagua hawakuhisi mapigo ya moyo na wao kuondoka zao.

Chagonja ni kama anaweweseka kwa kutoamini kuwa Dr. Ulimboka yupo hai, anapata shida sana kuongea, anahisi anahisi kuwa anatolea ufafanuzi tukio ambalo halipo, anahisi yupo ndotoni na anajitahidi sana kujifinya ili aamke na kuachana na 'ndoto hii mbaya' namhitaji Chagonja nimhoji kuhusiana na tukio la Dr. Ulimboka, naamini nitagundua mengi ambayo alikuwa anayajua kabla, wakati na baada, pia katika kumnyong'onyeza zaidi nitafanya ni kuagiza Polygraph iili na yeye ajilizishe.

Hapo penye kijani
Hapo anzidi kudhihirisha kuwa na uhakika wa mazingira ya tukio. Kwa kanuni za kiinteligencia napenda kumkumbusha Chagonja kuwa alitakiwa kujiuliza au kutuuliza swali hilo kama kungekuwa na third person anayedai kumtambua Msangi, lakini hapa ni mtendwa aliyemtambua mmoja wa watesi wake, yeye ni mtu sahihi kabisa kufanya utambuzi, najua Chagonja alitamani kusema kuwa"Kwa hali aliyo nayo Dr. Ulimboka na kwa namna alivyoumizwa anaweza akasema lolote, hivyo si sahihi kumtilia maanani," lakini kauli hii kwa bahati nzuri kwake Chagonja iliishia mdomoni baada ya kujing'ata ulimi.
Amini ninayo waambieni, Chagonja ni mtuhumiwa mwingine katika sakata hili, muda utafika na kila kitu kitakuwa wazi, nina uhakika hata acha kuweweseka kwa sababu kwa nafasi yake lazima kuna alama muhimu sana ameiacha ambayo inamuunganisha yeye moja kwa moja, na kwa sabau ya taharuki ya kumuaona 'Mfu' anaishi tena miongoni mwa walio hai hadithi ambazo mara ya mwisho alipata kuzisoma katika kitabu cha Biblia, kuwa huko Uyahudi kuna mtu aliwahi kukamatwa kuteswa na kuuawa, kuchanganyikiwa kwake kunatokana na kujaribu kukumbuka ni alama ipi inayomuunganisha yeye ambayo ameiacha.

Tusubirini.
 
Nilishawaeleza polisi ni genge la vibaka waliovalishwa sare tu. Hakuna kitu. Eti itamghalimu sasa imgharimu mara ngapi.....waache waseme hawajui kwamba mdomo unaponza kichwa.....si tunao mtaani tutakula sahani moja. Ipo siku 1 tu.
 
Chagonja umedhihilisha kuwa hamnazo kabisa. Na hii inaonyesha ulimbukeni wa viongozi wa polisi. Dr.Ulimboka ndiye aliyemtambua mtekaji wake, huyo fedhuli wako ACP Msangi wewe Chagonja unatuambia kuwa hakuna mtu anayemjua mtekaji, sasa hata hiyo tume mliyounda itampata je mtekaji; kama hakuna mahala pa kuanzia huo uchunguzi. Chagonja ulitakiwa kutuambia kuwa mtuhumiwa mmoja kapatikana naye ni ACP Mgonja. Kumbuka Dr.ni mlalamikaji na pia ni shahidi namba moja. Sasa wewe kama mmoja wa viongozi wa polisi unapoanza kutoa vitisho vya kijinga,kwa mlalamikaji ili iwe je!!! Au nawewe ni mmoja wao wa watekaji, unaanza kujihami? Chagoja kumbuka watanzania wa leo sio wa mwaka 47.
 
jeshi la polisi ni kweli halihusiki mbona dr.kwa kauli yake amesema tuhuma zinazosambazwa kuhusu kamanda msangi sio za kweli na yeye wala hajasema kuwa arudishiwe simu yake na wallet yake na kamanda huyo.

Amesema wapi?ww acha kuckiliza maneno ya vijiweni
 
Hivi lenyewe lajijuwa kama ni mbumbumbu wa sheria? Kuna siku nilimsikia akisema polisi wanaruhusiwa kuuwa na akataja kifungu cha sheria ya kanuni za Adhabu.

Nilikisoma kile kifungu na kugundua kuwa hakiwaruhusu kuuwa ila tu kama ni kwa kujitetea maisha yao yakiwa hatarini kuuwawa. Lakin tumeona polisi wakiuwa wananchi huku wananchi hao wakiwa hawana silaha zozote za moto, pengine mawe tu na fimbo. Wengine wameuwawa kwa risasi visogoni huku wakikimbia.

Wananchi hao wakiwa hawana silaha zozote za moto, ndo walomwua askari polisi kule Tegeta!
 
kweli walimwengu waongo, hakuna ACP anayeitwa chagonja, pili huna uhakikika na elimu yake, tatu soma public sercvice act ujue watu wanaoruhisiwa kugoma kisheria, nne usikurupuke kuandika mambo ambayo huyajui

Ukubwa jiwe,nilivumilia nimeshindwa naona unaendelea kupoza moto kwa petrol,sijui utauzima vipi na wakati simu yako haina salio na hivyo una-bipu faya,sijui itakuwaje na wewe ndio ulieunguliwa?for your information mnahangaika bure possiblelize impossible,mtake msitake wasaa wa ukombozi umewadia,wasaa wa kukataa dhuluma umewadia,wasaa wa kupinga unyama unaotendwa na polisisiemu umekwisha.tunajua propaganda zenu mnazozifanya kila siku katika utendaji wenu wa kazi,tunajua mnavyobambikia watu kesi,tunajua mnavyowalamba miguu wakubwa wenu dhaifu,ila mnahangaika bure pasi na mafanikio.leo unapolazimisha kupindisha ukweli mimi sikuelewi,haijalishi ni ACP au ASP what matters ni ujumbe unaomhusu Chagonja na vitisho anavyovifanya,na kama hujui siku hizi kila mnapopanga mambo yenu kuna watu wanapingana na dhuluma hizo na ndio maana tunajua taarifa nyingi.na wala usipindishe suala la kumteka nyara Dr Ulimboka mnahusika.vitisho mnahusika ila mkumbuke nyinyi mna silaha sisi tuna Mungu,na kila mnapoua mmoja au kujeruhi Mjue mnazidi kuwajenga watu kwenye ujasiri na mnaongeza ari,chachu ya kupigania haki.Rejea maneno ya dr Ulimboka leo wakati anaondoka kwenda kutibiwa ndio utajua huo ni mwanzo mzuri wa ukombozi
 
kweli walimwengu waongo, hakuna ACP anayeitwa chagonja, pili huna uhakikika na elimu yake, tatu soma public sercvice act ujue watu wanaoruhisiwa kugoma kisheria, nne usikurupuke kuandika mambo ambayo huyajui
Pole yako naona umeshikwa MAKALI.O yote mawili unaandika uharo mtupu,halafu ndio nyie form four failure mnakimbilia Police kizembe,service yenyewe imekushinda kuandika,pambaf zako wee
 
Back
Top Bottom