Kamala: Slaa muongo, aombe radhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kamala: Slaa muongo, aombe radhi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Safari_ni_Safari, Oct 26, 2010.

 1. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  BAADA ya kusisitiza kauli yake ya kuuza saruji kwa Sh 5,000 kwa mfuko mmoja akiingia madarakani, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chadema, Dk Willibrod Slaa, ametakiwa aache kujadili masuala ya uchumi kwa kuwa hayajui.

  Akizungumza kupitia ITV Jumamosi, Dk Slaa alisisitiza kauli yake hiyo ambayo amekuwa akiitumia kukampeni, akisema akiingia Ikulu ataondoa kodi kwenye saruji na mabati ili wanyonge wajenge nyumba.

  Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Diodorus Kamala, jana alisema kuwa , Dk Slaa katika uchumi ni ‘mweupe’ na inaonekana anazungumza kitu asichokijua na kudanganya wananchi.

  Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Dk Kamala alisema, ahadi hiyo ni ya uongo kwani Sh 5,000 ni gharama ya usafirishaji wa mfuko kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa njia ya reli na tani moja ya saruji ya mifuko 20 ni Sh 100,000 hivyo gharama kwa mfuko kuwa Sh 5,000 sawa na bei anayowaahidi Watanzania.

  Alisema, gharama za uzalishaji si chini ya Sh 7,000 kwa mfuko na kabla ya kuongeza gharama nyingine, mfuko wa saruji unapofika Mwanza gharama inakuwa zaidi ya Sh 12,000, hivyo kwa bei yake kuwa kubwa. Dk Kamala alisema hoja hiyo ni ndoto ambayo hata viongozi wa nchi tajiri duniani hawatarajii kuiota mbali na kuitekeleza na huko ni kudanganya wananchi.

  Akizungumzia hoja ya makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kwamba yanaumiza Watanzania, alisema Dk. Slaa anapotosha kwani msingi mkuu wa makubaliano hayo ni ushirikiano huo kujengwa hatua kwa hatua kulingana na ridhaa ya wananchi.

  “Serikali imekuwa ikizingatia msingi huu kikamilifu kwa kushirikisha wananchi, likiwamo Bunge ambalo Dk Slaa amekuwamo kwa miaka mingi, mfumo huu unaziwezesha nchi wanachama kupata fursa ya kujipanga vema katika utekelezaji na kuitumia ngazi moja kuwa msingi wa kupanda ngazi inayofuata ya utangamano,“ alisema Kamala.

  Kuhusu mfumo wa kodi katika jumuiya, alisema si kweli kwamba aliuanzisha yeye, kwa kuwa yalianza kabla hajawa waziri na haiwezekani ushuru ufutwe bila kujadiliana na kukubaliana nchi wanachama, hivyo akasema Dk.Slaa hawezi kufuta ushuru huo kwani ni lazima ajadiliane na viongozi wa EAC.

  Kuhusu viwango vya VAT alisema Dk. Slaa ameonesha hajui kuwa kodi hiyo si ya Afrika Mashariki na kiasi cha VAT anacholipa mlaji kinategemea bei ya bidhaa katika soko, huku akitolea mfano wa maji ya kunywa ya ujazo wa nusu lita, ambayo Tanzania yanauzwa Sh 500 na Kenya Sh 800 ingawa Mkenya analipa VAT ya asilimia 16 na Mtanzania asilimia 18; Mkenya analipa kiasi kikubwa kuliko Mtanzania.

  Alisema kabla Dk. Slaa kusema Tanzania imeliwa, kwa kuwa na kiwango cha juu cha VAT Afrika Mashariki, alitakiwa kuelewa kwamba, VAT si kodi ya Afrika Mashariki na katika uchumi, huwezi kulinganisha viwango vya VAT kabla ya kuangalia mfumuko wa bei kwenye nchi unazotaka kulinganisha, na kabla haujakokotoa, lazima uangalie viwango vya thamani ya kubadilisha fedha na gharama ya maisha.

  Pia, alimtaka Dk. Slaa kuwaomba radhi Watanzania kwa kuwadhalilisha akiwaita mbumbumbu, kielimu na katika kufanya biashara, huku akitaka kura zao, jambo ambalo si kweli, kwani miaka mingi Tanzania imekuwa kitovu cha elimu katika kanda hii huku viongozi wake wengi wakisoma hapa.

  Katika mkutano huo na waandishi wa habari alizindua Kamati Maalumu kutoka sekta mbalimbali kuangalia sheria zilizoko nchini zinazokinzana na makubaliano ya soko la pamoja, ili ziweze kufanyiwa marekebisho kwa maslahi ya nchi.

  Alisema, kazi ya kamati hiyo itakayokabidhi kwa waziri mapendekezo yao Novemba 30 ni kuangalia sheria zilizopo iwapo zinatoa mianya ya mtu asiye Mtanzania kumiliki ardhi kinyemela, kutokana na makubaliano ya soko la pamoja kuwa masuala ya ardhi yatakuwa chini ya sheria za nchi husika.

  Source?
  As usual.....Habari Leo

  Na haya ni maoni ya wasomaji wake Habari Leo

  Jumla Maoni (5)

  1. Nawashangaa sana Watanzania kama wanakubaliana na Huyu waziri wa Afrika ya Mashariki ambaye hana huruma na watanzania ambao umasikini umezidi kuwaandama na elimu ya kubaguzi ikizidi kushika kasi. Kwa mfano mwaka huu ukiangalia watoto wa masikini ndio kwenda vyuo vikuu ndio wanapata asilimia ndogo za mikopo kwa sababu hawachuchukui kozi za masomo ya sayansi kufuatana na shule za kata wanazosoma kutokuwa na Maabara na walimu wa Sayansi. Masomo ya sayansi yanabakia kuwa kwa watoto wa matajiri na ambao ndio wanaenda vyuoni kuchukua sayansi ambao wanapata asilimia 100%.

  Tutafakari taifa linakokwenda kwa kuendekeza uchama na si ukweli uliopo mpaka sasa.

  2. HApo Dr. kamala umepotea sana kwani si kigezo kujivunia kuwa viongozi wengi wa Africa wamesomea Tanzania,hii ni sawa na kujivunia wawekezaji wanaotuibia kila siku kwa kusema wawekezaji wengi wamekuja ilihali mtanzania anabaki maskini mali imeenda ulaya,wewe umesoma na sijui elimu yako imesaidia nini watanzania kama si kutuburuza kuingia shirikisho wakati wenzetu wakitucheka kila siku, tuombe msamaha watanzania kwa dhambi uliyofanya.

  3. We Kamala, hivi unausaka ubunge wa kuteuliwa? wewe unayeujua uchumi mbona hujaisaidia nchi kuondokana na mfumko wa bei? Wewe ni wale wale tu. Huna jipya na ndio maana hata kwenu hukubariki. Au ndo unajiandaa kugombea ubunge wa afrika mashariki? Tumia Phd yako kuwaza na kufukiri kabla ya kuropoka. Hufanani na hali hiyo. Hao wasio mbumbumbu wa uchumi wameisadiaje nchi hii? mbona hali ya maisha inaendelea kuwa mbaya pamoja na hazina ya maliasili tulizonazo? Kama waziri wa afrika mashariki, mbona hujashughulikia swala la madini ya Tanzanite kuuzwa kwa wingi Kenya badala la Tanzania yanakochimbwa? Wewe ni Fisadi tu, una tanga tanga baada ya kuukosa ubunge. Subiri zawadi ya kuteuliwa. SHIT.

  4. sijaelewa maelekezo ya kiuchumi wa huyu jamaa hata mi ambaye sijasoma siwezi kubaliana!

  5. Kwa mara ya kwanza ngoja tujaribu kuchagua uongo wa Dr Slaa maana tumechoka na huo mnaouita ukweli wa CCM unaotuzidishia umaskini tangu tupate uhuru miaka takribani 50 iliyopita.
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Sijui yeye uchumi anaujua vipi walahi huyu Dr wa kuchongesha Phd
   
 3. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyo bora angekaa kimya tu badala ya kuongea ongea, bahati mbaya zaidi juzi juzi wameagiza cement ishushwe bei sijui hana mawasiliano na katibu mkuu viwanda na masoko. Anyway, hayuko makini Kamala, CCM wanaendesha nchi kwa mazoea kuwa watanzania bado hawaoni wala haziwatoshi!!

  Lakini mwaka huu hata wakishinda kwa kuchakachua somo limewaingia, na adhabu iko mbioni inakuja kama si wiki hii basi kati kati ua miaka mitayo ijayo itakuwa balaa.
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,461
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Nawashukuru wapiga kura wake kwa kumbwaga...sasa anatafuta ubalozi labda....kama CCM ikishinda
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Ana kesi ya kujibu kwa msemakweli ya kuchakachua phd. Kuna jamaa kasoma naye secondary anadai ni mchovu hana upeo wa kutisha ni KAWAIDA TU.Huenda pia ni mdau wa "madesa"
   
 6. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wapiga kura wake walimbainii mapema kuwa ni MWEUPEE KIELIMU NDO MAANA ANA PHD YA KUCHONGAAAAA.......SHAME ON U!!!
   
Loading...