Kamachumu, Muleba: Moto wateketeza Mabweni ya shule ya Msingi St. Joseph Usiku

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Kagera: Taharuki imetanda katika shule ya msingi St Joseph Rutabo iliyopo Kamachumu, wilayani Muleba baada ya mabweni ya wanafunzi kuungua moto

Mabweni matatu ya wanafunzi shule ya msingi st Joseph Rutabo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Muleba yameungua moto usiku wa kuamkia leo na inadaiwa Mwanafunzi wa darasa la tano ameungua moto na kufariki. Wanafunzi wengine wanaendelea vizuri. Inasemekana moto huo umetokana na hitilafu ya umeme

Stay tuned..


9681f67b-4d60-48b5-94dc-95bc1dc13fde.jpeg

518d9637-7538-4100-a7f1-3fc192ad1b83.jpeg

57623337-8091-4ec6-ad2a-47631dc0ac1b.jpeg
 
Last edited by a moderator:
Kwao na Mzee Charles Mwijage. Bila shaka yeye kama mbunge wao atawasaidia kwa njia moja au nyingine
 
Bukoba. Taharuki imetanda katika shule ya msingi St Joseph Rutabo iliyopo Kamachumu Wilaya ya Muleba mkoani Kagera baada ya bweni la wanafunzi kuteketea kwa moto.

Bweni hilo limeteketea leo Alhamisi Julai 26, 2018 huku mashuhuda wa tukio hilo wakisema viongozi wa wilaya hiyo wapo katika kikao na walimu kujadili tukio hilo

Source. Mwananchi
 
Kwa wale walioko mkoani Kagera, nimepigiwa simu kuwa shule ya Rutabo inayoendeshwa na Kanisa Katoliki imeungua leo. Aliyenipigia alikuwa hana taarifa kamili bali kuna vijana wangu pale. Nawpigia waalimu simu hazipatikani, kama kuna mdau ana taarifa yeyote juu ya hili tafadhali anifahamishe inbox

Aksante
 
Back
Top Bottom